De Bruyne: Nataka kuondoka Chelsea.
De Bruyne kinda wa Chelsea mwenye
umri wa miaka 21 amesema kwasasa anafikiria kuondoka Stamford Bridge kwa muda
ili kusaka timu ambayo atapata nafasi katika kikosi cha kwanza wakati ambapo
uhamisho wa kueleka Werder Bremen kwa
mkopo ukitarajiwa kukamilika wiki hii
Kwa mujibu wa chanzo cha habari
kutoka Belgium na Germany mchezaji huyo huenda akatambulishwa mbele ya
waandishi wa habari kesho jumatano kabla ya kuanza mazoezi ka kikosi chake
kipya baadaye wiki hii.
Amenukuliwa De Bruyne akiongea na
Bild akisema
"kocha Roberto Di Matteo anaelewa
hali ilivyo , nataka kuelekea Werder ni timu nzuri"
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Belgium
alijiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni £7 mwezi January toka Genk lakini
aliendelea kuwepo kwa mkopo na klabu yake ya zamani mpaka kumalizika msimu.
Hivi karibuni ameichezea Chelsea
katika michezo miwili ya matayarisho ya msimu dhidi ya Seattle Sounders na Paris
Saint-Germain.
Mabingwa wa sola Ulaya Chelsea
kwasasa wamebadilisha kikosi chao kwa lengo la kukijenga upya wakiwasajili Marko
Marin, Eden ,Thorgan Hazard Oscar baada ya kuwaacha Didier Drogba na Salomon
Kalou.
Kundi la mashabiki wa United wagomea mpango wa kuuza hisa wa Glazers family
Wamiliki wa Manchester United
wamekuwa katika wimbi kubwa la ukosoaji baada ya kuonyesha kutaka kutumia nusu
ya mpango wao wa IPO kutumika kupunguza madeni makubwa ya klabu hiyo.
Glazer family wanamatumaini ya
kuongeza uwezo wao kifedha mpaka kufikia pauni milioni £200 kwa kuuza zaidi ya
asilimia 10% ya soko la hisa la New York lakini haitatumia pesa kupunguza
madeni ya United mbayo kwasasa yamefikia pauni milioni £437.
Endapo watakamilisha hilo Glazers wameonekana
wazi kutaka kutumia nusu ya kiasi hicho kwa ajili ya madeni ya klabu hiyo
ambayo yaliyotokana na malumbano makubwa ya wakati huo wakiichukua klabu kwa
pauni milioni £800 mwaka 2005, ambayo
sehemu kubwa ya fedha hizo walikopa.
Mashabiki wa United walikuwa katika
kampeni yao maarufu kama utamaduni wao wa 'green
and gold' katika msimu ulipiota wakibariki rangi zao za zamani kama Newton Heath, kuashiria
kutokufurahishwa na umiliki wa Glazers ndani ya Old Trafford.
Amenukuliwa Duncan Drasdo mtendaji mkuu wa mfuko wa
mashabiki wa Manchester United (MUST) akisema "mashabiki wanakasirishwa
sana na hili, Glazers wameigharimu United zaidi ya pauni milioni £550 kama deni
linahusiana na ada, na sasa wanatuingiza katika janga lingine ambalo wao ndio
watanufaika nalo kupunguza nusu ya mpango wa IPO”.
"ni wazi kabisa hili halina
faida kwa Manchester United zaidi ya kuipa Glazers njia ya kujipatia fedha kwa
mgongo wa matumizi ya klabu."
Ramires arejeshwa kikosini Brazil kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Sweden
Ramires Santos do Nascimento kifupi ‘Ramires’
ameitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil cha kocha Mano Menezes ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao
ya kombe la dunia 2014 dhidi ya Sweden.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25
alikuwa msaada mkubwa katika timu ya Chelsea ambao ni mabingwa wa kombe la FA na
vilabu bingwa ulaya msimu uliopita licha ya kutokuwepo katika kikosi cha Brazil
maarufu kama ‘Selecao’ tangu kuwepo katika kikosi hicho kwenye Copa America 2011.
Menezes ameamua kumkaribisha tena
kiungo huyo na atakuwa akiungana na wenzake wa timu moja David Luiz na Oscar
Dos Santos.
Timu hiyo inaonekana kama kikosi kile
kile kinachoshiriki michezo ya Olympic jijini London wakati ambapo Dede na David Luiz wakionekana kuipa nguvu katika eneo
la ulinzi wakati ambapo Marcelo akiwa mapumziko.
Kiungo wa gharama kubwa wa Corinthians
Paulinho pia ameitwa nah ii itakuwa ni kama kupata nafasi ya kuitumikia timu
hiyo kwa mara ya pili.
Mshambuliaji wa Valencia Jonas huenda
akapata nafasi ya kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipotoa huduma
katika kikosi hicho mara ya mwisho akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Bosnia
na Herzegovina mwezi February.
Mchezo dhidi ya Sweden utapigwa August
15.
Diarra:Nitacheza sehemu yoyote Mourinho atakayo nihitaji
Lassana Diarra amekanusha taarifa
kuwa hataki kucheza upende wa ulinzi wa kulia katika timu yake ya Real Madrid.
Taarifa ziliarifu kuwa mfaransa huyo
alimwambia kocha wake Jose Mourinho kuwa anataka kucheza sehemu ya kiungo tu
lakini kiungo huyo amekanusha juu ya hilo na kusema kwa yeye ni mwenye furaha
kucheza popote pale kocha wake atakapo taka.
amenukuliwa Diara kupitia mtandao wa
klabu akisema.
"nacheza popote Mourinho atakapo
mimi nicheze. mimi ni mfanyakazi nisiyechoka ambaye natumia uwezo wangu wote
kwa ajili ya timu".
Madrid haiko vizuri kwasasa katika
sehemu ya ulinzi ya kulia kufuatia kuondoka kwa Daniel Carvajal ambaye
ameelekea Bayer Leverkusen, wakati ambapo Sergio Ramos anatumika sehemu ya
ulinzi ya kati.
Kwasasa Alvaro Arbeloa ndiye chaguo
pekee la Mourinho sehemu ya ulinzi wa kulia.
Aidha , Diarra anaonekana kuwa tayari
kuziba nafasi hiyo endapo Mourinho atataka kumtumia kufuatia maoni yake hayo.
No comments:
Post a Comment