KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 31, 2012

Zidane kufundisha Real Madrid ya vijana (cantera)


Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amepata kazi ya kufundisha timu ya vijana ya Real Madrid (cantera) wakati akipata sifa ya kufundisha hizi zikiwa ni taarifa mpya toka kwamabingwa hao wa ligi ya Hispania ‘Liga’ klabu hiyo imetangaza.
Akiwa na umri wa miaka 40 kwasasa na akiwa ametangaza rasmi kustaafu soka mwaka 2006, sasa ameweka wazi dhamira yake ya kuingia katika uongozi akiwa tayari ameshajiunga na mafunzo ya kufundisha soka katika chuo kimoja alichokuwepo kocha wa zamani wa Ufaransa Laurent Blanc mwaka jana.
Tangu atundike daruga , Zidane amekuwa akifanya kazi ya kumshauri Rais wa Madrid Florentino Perez na kocha Jose Mourinho, na sasa atakuwa na nafasi yake katika academy ya klabu hiyo.
 Taarifa ya klabu hiyo imesema
"Zinedine Zidane ameanza mafunzo ya kufundisha wakati huo huo atakuwa akifundisha vijana katika academy Real Madrid"
"mwaka huu atakamisha kupata cheti cha team-management mafunzo ambayo alianza miezi michache iliyopita.
"hiyo itamsaidia kujenga uwezo na mafunzo ambayo yatamfanya kuwa kukamilisha kiu yake kama alivyotangaza katika mkutano na waandhishi wa habari wakati akistaafu kucheza soka mwezi April mwaka 2006"
Zidane anatarajiwa kumrithi Alberto Giraldez kama kiongozi wa kituo cha vijana na atakuwa na kazi ya kujenga upya idara hiyo.