KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 14, 2014

Barcelona waacha vita kubwa baina ya Chelsea na Manchester United

Barcelona imeondoa nia yake ya kumsajili Juan Cuadrado
Manchester United na Chelsea zinajipanga kuingia vitani kwa ajili ya kunasa saini ya Juan Cuadrado baada ya Barcelona kujiondoa katika mbio za kusajili winga huyo wa Fiorentina.

Taarifa kutoka nchini Hispania hii leo zimedai kuwa klabu hiyo ya Katalunya imejiondoa katika mbio za kumsajili Cuadrado ambapo sasa wameelekeza mipango yao kwa mlinzi wa kushoto wa Sao Paulo Douglas kama mbadala wa Mcolombia huyo.

Taarifa za zimedai kuwa Luis Enrique anamfikiria zaidi mlinzi huyo wa Flamengo, Leo kama mpango wake mbadala ambapo unaacha vita vitani baina ya United na Chelsea huku kila mmoja akimtaka mlinzi huyo mwenye wasifu wa hali ya juu kwa sasa duniani, Cuadrado.