KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 15, 2014

Kiungo wa kweli kutoka Gor Mahia ya Kenya atua Coastal Union ya Tanga

Ramadhani Salum Mohamed
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya
Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini
Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.

Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union  akitokea nchini Kenya
na kusaini  mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja.

Rama aliyewahi kuicheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa
kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars
alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu
hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabu
hiyo barabara 11,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema
kikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana
na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta
upinzani mkubwa sana.

Aidha amesema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwa
sababu tunamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili
imara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile
Obina,Shabani Kado Sued Tumba ,Bakari Mtama, na wengine wengi walipokwenye kikosi cha timu hiyo

Amesema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha
kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi
kuu Tanzania bara msimu ujao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment