KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 20, 2014

Bingwa wa tenisi Serena Williams akerwa kuitwa 'kaka'.


Bingwa wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia yaliotolewa na rais wa shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na dadaake Venus Williams.
Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili'' .
Hata hivyo afisa huyo alipigwa faini ya pauni 15,500 na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha.
''Nadhani matamshi hayo yamejaa ubaguzi na hayajali'' alisema Wiliiams.
''Sikuyapendelea hata kidogo na nadhani watu wengi pia hawakuyapendelea''.
matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa na shirikisho la mchezo wa Tenisi duniani WTA pamoja na shikisho la mchezo huo nchini marekani USTA.
Shamil Tarpischev

Hapa Serena na Venus wakiwa katika muonekana halisi wa akina dada achilia mbali umbile la misuli iliyokakamaa kumchanganya Shamil Tarpischev
Hapa walipokutana wenyewe kwa wenyewe
Akina dada hao licha ya kutajwa kama akina kaka lakini bado wana maumbile ya kuvutia wanaume

No comments:

Post a Comment