Pages - Menu

Tuesday, June 26, 2012

Official: Arsenal yamtangaza Giroud kuwa mchezaji wao mpya

Olivier Giroud
The Gunners wamethibitisha rasmi kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa imekamilisha makubaliano ya kumsajili Mfaransa Olivier Giroud mkataba wa muda mrefu akitokea Montpellier bila kuweka wazi dau lake.
Arsenal ilikuwa ikihusishwa na mfaransa huyo muda mrefu ambapo sasa wameamua kuhangaikia taratibu za uhamisho na tayari amefanikiwa kipimo cha afya yake alicho fanya hapo jana.
Giroud amekuwa na Montpellier katika ligi ya Ufaransa  Ligue 1 na kutwaa taji msimu wa 2011-12. Amefunga jumla ya mabao 21 katika jumla ya michezo 36 na meneja wa Arsenal Arsene Wenger sasa anamsubiri Emirates Stadium kwa mkataba wa muda mrefu.
Giroud anaungana sasa na wafaransa wenzake  Laurent Koscielny, Bacary Sagna, Sebastien Squillaci, Abou Diaby na Francis Coquelin mjini London.

No comments:

Post a Comment