Pages - Menu

Friday, July 20, 2012

Higuain apigwa pingu Real Madrid

Gonzalo Higuain
Gonzalo Higuain anajipanga kuingia mkataba mpya na  Real Madrid kufuatia mkutano baina ya baba yake,wakala na mkurugenzi wa Madrid Jose Angel Sanchez mkutano uliofanyika Santiago Bernabeu.
Kwasasa Higuain nyota wa kimataifa wa Argentina yuko katika mkataba na Madrid utakao malizika kiangazi 2016, lakini bado Los Blancos wanataka kumaliza kabisa fununu na uwezekano wowote nyota huyo kupata mawenge ya kuondoka na wanampango wa kumuongezea mashahara euro milioni €3.5 kwa msimu mpaka euro €4.5m.
Alijiunga na Real Madrid akitokea River Plate January 2007, na tangu wakati huo amefunga jumla ya magoli 91 katika ligi kuu ya nchini Hispania La Liga baada ya kucheza mechi 162.

No comments:

Post a Comment