HAPA CHINI NI KIKOSI CHA PILI CHA AFRICAN LYON CHINI YA KOCHA ALUKO KIKIPATA MAELEKEZO YA KOCHA HUYO
Wakati ligi kuu ya Tanzania Bara ikipangwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15 kwa viwanja 7 kuwaka moto, timu ya Afrikan Lyon chini ya kocha wake Pablo Velez imejipanga vema kwa ajili ya ligi hiyo ambapo Afrikan Lyon wamepangwa kuanza na mabingwa watetezi Simba.
Akiongea na rockersports katibu wa klabu hiyo Brown Ernest amesema mpaka sasa kocha Veles amekuwa katika hatua za mwisho kutengeneza kikosi cha kwanza kazi ambayo imekuwa ni ngumu kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwa wachezaji hao katika kila eneo.
Brown amesema kupitia michuano ya Super Six kule mkoani Pwani michuano ambayo ilikuwa ikishirikisha timu za majeshi na Lyon kushiriki kama mwalikwa, wamefanikiwa kujenga kikosi imara ambacho kitakuwa moto wa kuotea mbali katika ligi kuu msimu huu.
Amevitaka vilabu vyote vya ligi kuu kujipanga vizuri na kwamba moto utaanza kuwawakia Simba katika mchezo wa ufunguzi Septemba 15 uwanja wa Taifa.
Lyon msimu huu imewasajili wachezaji wapya saba akiwemo Yusufu Selemani , Paul Maona,Simion Shadrack , Bakari Mapakala , Jakson Kanywa , Robert Joseph na Samwel Rogart.
Pia Lyon ina wachezaji wanne toka nje ya nchi akiwemo Bryton Obina( Nigeria) , Hood Mayanja(Uganda) , Salamusasa Obina(Nigeria) na Michael Ndere(uganda).
Lyon inafundishwa na kocha raia wa Argentina Pablo Velez ambaye anapofundisha anapata msaada wa mkurugenzi wa ufundi Charles Otieno.
No comments:
Post a Comment