Pages - Menu

Friday, November 30, 2012

Mancini wasiwasi na mashaka tele kuwakosa ndugu wawili akina Toure mwezi januari.


Bosi wa Manchester City Roberto Mancini amekumbwa na hofu kubwa ya kuwakosa wachezaji wake ndugu wawili toka familia moja Yaya na Kolo Toure ambao wanatarajiwa kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya  Ivory Coast katika fainali za mataifa nchini Afrika kusini .

Michuano hiyo imepangwa kuanza januari 19 na kumalizika Februari 10 na hivyo huenda wakakosekan katika michezo kadhaa ya klabu yao ya City.

Kama ilivyo kwa kiungo Yaya na mlinzi Kolo, kiungo mwingine Adbul Razak huenda naye akaitwa katika kikosi hicho cha Ivory Coast.

"ningependelea wasiende katika michuano hiyo lakini ni ngumu, tutahitaji kuongea na meneja" amesema Mancini.

"kama tutamkosa Yaya, Kolo na Abdul, pamoja na kwamba hatumiki katika ,michezo mingi itatuwia vigumu kupata mchezaji mchezaji wa kubadilisha endapo tutapa majeruhi."

Yaya ambaye ameitumikia Ivory Coast michezo 67, anatajwa kuwa ni miongoni mwa viungo bora duniani na ni ngumu kwa kocha wa Tembo Sabri Lamouchi kumuacha kiungo huyo katika kikosi chake kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment