Pages - Menu

Wednesday, November 21, 2012

PEPE ATOA ANGALIZO JUU YA CRISTIANO RONALDO NA MADRID.



Mlinzi wa kati wa Real Madrid Pepe amesema haoni sababu kwanini klabu yake isimuongezee mshambuliaji Cristiano Ronaldo mkataba mwingine mnono endapo wanataka kuimarisha kikosi chao.

Habari zilizo tawala vyombo vya habari msimu huu juu ya Ronaldo kukosa raha ndani ya klabu hiyo zimeonekana kuchagiza juu ya haja ya kuboresha mshahara wake wa sasa wa euro milioni €10.5 wakati ambapo kuna habari kuwa mshambuliaji huyo anafikiria kuelekea kati ya Manchester City au Paris St Germain msimu ujao wa uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa Ureno Pepe, akiongea na vyombo vya habari kuelekea kwenye mchezo wa usiku huu dhidi ya Manchester City amesema anamatumaini  Ronaldo atasalia Estadio Santiago Bernabeu, lakini akaweka angalizo kuwa hilo litategemea na ofa ya klabu yake.

No comments:

Post a Comment