Pages - Menu

Thursday, December 6, 2012

DAVID LUIZ ANASEMA WACHEZAJI WAKIMFUATA BENITEZI BASI MAMBO YATAKUWA SAFI.

David Luiz, ambaye alifunga goli la ufunguzi la Chelsea katika mchezo ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa 6-1 mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Nordsjælland kule darajani, amesema klabu yake itayachukuliya mashindano ya ligi ya Ulaya(europa league) kwa uzito mkubwa .
 
Ushindi dhidi ya Nordsjælland ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha Rafael Benitez ambapo David Luiz anasema,
"ulikuwa ni mchezo mzuri kwa wachezaji wote kimorali, ubora na ufungaji wa magoli jambo ambalo ni zuri katika siku zijazo.

"Tuna kocha mpya na ana filosofia mpya jinsi tutakavyokuwa wepesi wa kumfuata tutakuwa na timu nzuri"

No comments:

Post a Comment