FRANK RIBERY
Kocha wa kikosi cha Bayern Munich
Jupp Heynckes atalazimika kumkosa winga wake Frank Ribery katika mchezo dhidi
ya Arsenal ukiwa ni mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa
Ulaya dhidi ya Arsenal.
Ribery alikuwepo dimbani dakika zote
90 za mchezo wa ligi kuu ya nchini Ujerumani dhidi ya Fotuna Dusseldorf mchezo
uliofanyika mwishoni mwa juma ambapo Munich ilishinda kwa jumla ya mabao 3-2
na yeye ndiye aliyefunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2
kunako dakika ya 73.
Ribery alionekana kulalamika kuwa
anajisikia maumivu ya enka ya mguu wake ya kushoto ambapo baada ya vipimo
kufanya hatimaye klabu hiyo ikathibitisha kumkosa mchezaji huyo katika mchezo
wa jumatano.
kuumia kwa Ribery ni pigo lingine
kwa kocha Heynckes, ambaye pia atamkosa Bastian Schweinsteiger na Jerome
Boateng kufuatia kusimamishwa.
Bayern itakuwa ikilinda ushindi wake
wa kwanza uiliochezwa katika uwanja wa Emirate ambapo waliiibuka na ushindi wa
magoli 3-1.

No comments:
Post a Comment