Rais wa Chama cha soka nchini Malawi (FAM) Walter Nyamilandu amesema chama chake hakina pesa ya kumuajiri kocha wa kigeni kufundisha kikosi cha timu ya taifa ya katika muda huu.
Amethibtisha hilo huku akidai kuwa mpango na kocha raia wa Belgiam Tom Saintfiet ambaye alianza kazi ya kuifundisha timu ya taifa kwa kujitolea mwezi Julai umemalizika.
Nyamilandu amesema makubaliano na Saintfiet kuifundisha The Flames yamemalizika rasmi baada ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Super Eagle ambao The Flames walichapwa bao 2-0 mjini Calabar Jumamosi iliyopita.
No comments:
Post a Comment