KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 30, 2014

29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS AKIWEMO MSUVA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.
 
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.
 
Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
 
Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
 
TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
 
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
 
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
 
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).

TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
    
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).

Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.

RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.

Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.

Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.

Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.

Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.

Javier Hernandez amedhihirisha kuwa yeye ni zaidi ya super-sub Madrid

Javier Hernandez amedhihirisha kuwa yeye ni zaidi ya mchezaji wa akiba (super-sub) ndani ya kikosi cha Real Madrid kufuatia kufunga katika mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Cornella ukiwa ni mchezo wa Copa del Rey Jumatano.

Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico alipewa nafasi katika kikosi cha kwanza na kudhihirisha uwezo ndani ya Real kama ilivyokuwa kwa Manchester United ikiwa ni mara moja tu ndani ya La Liga msimu huu.

Kocha mkuu Carlo Ancelotti amempa nafasi mshambuliaji huyo ya kuonyesha ubora katika Copa de Rey, na kufunga goli ndani ya viunga vya  Estadio Municipal de la Via Ferrea.

Amenukuliwa Hernandez akisema"najituma kupata nafasi na natumia uwezo wangu wote nikiwa na Madrid ," alikuwa akiongea na wanahabari baada ya mchezo.

Del Bosque ampinga Mourinho kuhusu Diego Costa

Meneja wa timu ya taifa ya Hispania Vicente Del Bosque amesisistiza kuwa ataendelea kumtumia Diego Costa katika timu ya taifa licha ya pingamizi la meneja wake wa klabu Jose Mourinho.
Meneja wa Chelsea Mourinho alikosoa kuitwa kwa mshambuliaji wake Costa katika timu ta taifa kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kuwania nafasi ya kutinga fainali ya mataifa ya Ulaya 2016 dhidi ya Slovakia na Luxembourg.
"Diego alikuwa na majeraha kwakuwa alicheza michezo miwili ndani ya siku tatu alipokuwa mbali nasi" amenukuliwa Mourinho.

United kukamilisha mpango wa kudumu na Falcao

Manchester United hatimaye imekubali kutoa kiasi cha pauni milioni £44 kwa mkataba wakudumu kwa ajili ya mshambuliaji Radamel Falcao.

United imekubali masharti ya klabu ya Monaco kuhusu Falcao ambaye alijiunga kwa mkopo wa muda mrefu uliokuwa na thamani ya pauni milion £6 usajili uliofanyika siku ya mwisho ya uhamisho wa kiangazi

Mabingwa mara 20 wa ligi ya England, United, wana uamuzi ndani ya makubaliano ya kimkataba kumsajili kama wataridhishwa na kiwango cha Falcao kutegemeana na afya yake wakati huo.  

Imefahamika kuwa pande hizo mbili huenda zikakubalina katika kufikia mapango huo.
Falcao kwasasa anapokea mshahara wa pauni £240,000 kwa wiki na United imekubali kwa masharti yale yale kukamilisha mpango wa muda mrefu.
Wakala wa Falcao Jorge Mendes, amekuwa na ukaribu na watendaji wakuu wa United huku pia mshambuliaji mwenyewe akionyesha kutaka kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya msimu.Ndani ya mkataba wa sasa wa mkopo wa baina ya United na Falcao, kuna kipengelea kinacho ipa fursa United kutathmini kiwango cha mchezaji huyo na hali ya afya kwa wakati huo kabla ya kuingia makubalino mengine, kufuatia Falcao kuwa katika maumivu ya mguu kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kiasi kusababisha mshambuliaji huyo kuikosa fainali ya kombe la dunia.

Wednesday, October 29, 2014

Alejandro Sabella amemtetea mshambuliaji wake Lionel Messi licha ya kupondwa na Blatter

Bosi wa zamani wa Argentina Alejandro Sabella amemtetea mshambuliaji Lionel Messi akidai kuwa mshambuliaji huyo alijitoa kwa ajili ya taifa lake katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa katika mjadala mpana juu ya uwezo wake alionyesha katika fainali hizo zilizopita huku Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter hapo jana akikaririwa akisema kuwa mshambuliaji huyo hakustahili kushinda tuzo ya mpira wa dhahabu katika fainali hizo
Hata hivyo Sabella ameibuka na kudai kuwa Messi, ambaye ameshindwa kufunga goli baada ya kufunga magoli manne katika michezo mitatu alijotoa kwa kufanya kazi kubwa kwa ajili ya Argentina mpaka kuifikisha fainali alipokubali kucheza katika nafasi ya juu kwa kuwasaidia wachezaji wenzake.
"Messi ni mfano katika timu ya taifa," amesema Sabella mwenye umri wa miaka 59 alipokuwa akiongea na Radio La Red. "Alijitoa kimshikamano na wenzake
Sabella aliachia ngazi kuifundisha Argentina muda mfupi baada ya fainali hizo mjini Rio tangu kufikia mafanikio hayo ndani ya Albiceleste.

Tuesday, October 28, 2014

Diego Maradona tena ampiga msichanaVideo ya kushitusha imeonekana mtandaoni ikimuonyesha mkongwe wa Argentina Diego Maradona akimvamia msichana Rocio Oliva kabla ya kumpiga.
Maradona mwenye umri wa miaka 53, ameonekana akianza kwa kumfokea Oliva kabla ya mstaafu huyo wa soka aliyekuwa amelewa kuonekana kumpiga.
Video hiyo iliyotolewa na gazeti la nchini Hispania la El Mundo, ambapo katika tafsiri ya New York Daily News, msichana huyo alisikika akilia kwa kumuomba Maradona aache kumpiga(‘stop, stop, stop hitting me.’)
Taarifa kutoka Amerika ya kusini zinasema Maradona amekuwa akitafadhalisha kuenea kwa kipande hicho cha video lakini amethibtisha kuwa ni yeye aliyefanya kitendo hicho

Carlo Ancelotti amekubali kumpoteza Bale, kwa kiasi cha pauni milioni £90. United wako mawindoni

Manchester United imepiga hatua moja mbele katika harakati zao za kutaka kumsajili mshambuliaji Gareth Bale mwezi Januari baada ya Real Madrid kuripitiwa kutaka kumuweka sokoni mshambuliaji huyo.
United wanaaminiwa kumuweka Bale katika chaguo lao la kwanza wakati wa kipindi cha uhamisho cha mwaka mpya huku pia wakiwa tayari kumlipa kiasi cha pauni £300,000 kwa wiki ili muradi tu ajiunge Old Trafford.
Swali kubwa ni je Madrid kweli wanataka kumuuza ama laa, lakini taarifa nchini Hispania zinaarifu  kuwa Madrid wanafurahia kufanya biashara ya mchezaji huyo.
Inaelezwa kuwa meneja Carlo Ancelotti amekubali kumpoteza Bale, kwakuwa hafikirii kumtumia tena kama mchezaji wa kikosi cha kwanza kufuatia kuvutiwa zaidi na aina ya uchezaji wa Isco.
Madrid wanataka kiasi cha pauni milioni £90 kwa ajili ya kumtoa Bale.

Ronaldo ashinda tuzo Hispania La Liga lakini pia huenda akawa bora mwezi Januari duniani

Cristiano Ronaldo anaelekea pazuri zaidi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or kufuatia kutangazwa kuwa mchezaji bora wa Hispania La Liga huku pia akitajwa kuwania kwa mara nyingine tena tuzo kubwa ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or ikiwa ana tetea nafasi yake ya ubora baada ya kumshinda mpinzani wake Lionel Messi katika ubora wa nchini Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Hispania hapo jana baada ya kufumania nyavu mara 31 katika Ligi ya mabingwa Ulaya.
Huenda ikawa ni pigo kwa Messi, ambaye ameshinda tuzo hizo mara moja katika miaka mitano iliyopita.
Tuzo ya Ballon d'or itatangazwa mwezi Januari. 
Amepongezwa na mwenzake wa Real Madrid Gareth Bale ambaye kupitia ukurasa wake wa tweeter mbali ya Ronaldo pia amewapongeza Keylor Navas, Sergio Ramos na Luka Modric.

Tuzo zingine ni kwamba meneja Diego Simeone ambaye ameiongoza Atletico Madrid mpaka kuchukua taji amepata tuzo ya kocha bora wa mwaka wakati ambapo Sergio Ramos akipata tuzo ya mlinzi bora. 

Tuzo nyingine za La Liga ni kama ifuatavyo

LA LIGA AWARDS 

Best Player Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Best Coach Diego Simeone - Atletico Madrid
Best Goalkeeper Keylor Navas - Real Madrid (formerly Levante)
Best Defender Sergio Ramos - Real Madrid
Best Defensive Midfielder Luka Modric - Real Madrid
Best Attacking Midfielder Andres Iniesta - Barcelona
Best Forward Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Best African Player Yacine Brahimi - Granada
Best South American Player Carlos Bacca - Sevilla
Revelation Rafinha Alcantara - Barcelona (loaned to Celta in 2013-14)
Best Goal Cristiano Ronaldo (vs Valencia) - Real Madrid
Fair Play Ivan Rakitic - Barcelona (formerly Sevilla)

Wakati hayo yakiwa hivyo, Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ndio mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati wachezaji wanaoshindania tuzo la mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or huku mshambulizi matata wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa kuhifadhi taji hiloBale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid kunyakua kombe la kilabu bingwa duniani
Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar
Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich .
Hatahivyo hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa kumng’ata mlinzi wa Italy Giorgio Chiellini.