Ronaldo De
Lima ambaye kwasasa ana heshima kubwa nchini kwake Brazil amesema kocha wa
zamani wa Barcelona Pep Guardiola ndiye
chaguo lake la kwanza kurithi nafasi ya Mano Menezes aliyetimuliwa kazi hivi
karibuni.
Kocha Menezes
alitimuliwa kazi ijumaa baada ya kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na matokeo
mazuri katika michezo mbalimbali ya timu ya taifa hilo wakati huu ambapo Brazil
ambayo inaandaa michuano ya kombe la dunia 2016.
Japo kwamba Ronaldo
hakubaliani na maamuzi ya kufukuzwa kazi Menezes, amesema itakuwa ni vema
kumsaka kocha ambaye ana vigezo sahihi ambayo ni kama alivyo navyo kocha wa
zamani wa Barcelona Pep Guardiola.
Akiongea na
Globo, amesema.
"kila
mtu anapapara, lakini kila siku unatakiwa kuangalia kwa picha kubwa. Siwezi kufanya
maamuzi hayo, lakini Brazil inahitaji
kurejea tulikokuwa tena,"
"tuna
makocha wakubwa Brazil, na tunahitaji mtu ambaye anaonyesha utulivu ndani ya
timu,
"Guardiola
ni kocha bora duniani kwasasa. Alifanya kazi nzuri Barcelona na anaweza kuwa
chaguo bora kwa Brazil. Hebu tuone kama mashabiki watampenda ama laa"
Rodgers: Liverpool itatwaa mataji muda si mrefu.
Meneja wa Liverpool
Brendan Rodgers amesema miaka michache ijayo klabu yake italeta changamoto mpya
ya kutwaa mataji ya ligi ya England.
Kwasasa Liverpool
iko katika 12 katika msimamo wa ligi kuu ambapo kuelekea kweny mchezo dhidi ya Swansea
City kocha huyo anayetokea Ireland ya kaskazini anasena anamatumaini kuwa
mazuri.
Liverpool haiajawahi
kumaliza ligi kuu ya England ikiwa katika nafasi ya kucheza michuano ya klabu
bingwa Ulaya tangu Rafa Benitez alipokuwa akiiongoza na kwasasa iko nyuma ya
kikosi cha kocha wao huyo wa zamani kwa alama tisa ambapo Chelsea iko katika
nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya England.
Rodgers anasisitiza
kuwa pamoaj na kwamba kujenga kikosi ni muhimu lakini pia ina weza ikato
changamoto muda mfupi ujao na kuwapa raha mashabiki wake.
"sioni
sababu ya kwanini tusitoe changamoto katika kipindi cha miaka michache ijayo. Wakati
mwingine unaweza kudondoka kwa hatua chache kabla ujaanza kujijenga upya"
Kwasasa Luis
Suarez wa Liverpool anaongoza orodha ya wafungaji wa Premier League akiwa
tayari amefunga jumla ya mabao 10 baada ya michezo 12 ya msimu huu ambapo Rodgers
amesema ataendelea kumtumia mruguayi ambaye yuko kwenye fomu.
Ancelotti: Pato anastahili kuchezea Paris
Saint-Germain.
Carlo
Ancelotti amezidi kutia utambi tetesi za Paris Saint-Germain kuwa huenda
waanzisha tena mpango wao wa kumtaka mshambuliaji wa AC Milan Alexandre Pato
akidai kuwa mshambuliaji huyo ana vigezo vyote vinavyotakiwa.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa iliaminika kuwa alikiwa karibu kukamilisha uhamisho wake
wa euro milioni 35 kuelekea Parc des Princes mwezi Januari lakini baadaye
mpango huo ukaonekana kwenda kombo.
Hata hivyo
kuna taarifa kuwa pande mbili hizo zinaelekea kukubaliana kutokana na kile
kinachoelezwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hana raha na
maisha ya soka ndani ya klabu ya AC Milan.
Wakati hayo
yakiwa hivyo, Ancelotti ambaye alimfundisha mshambuliaji huyo kule Rossoneri kati
hya miaka ya 2007 na 2009 ameeleza kuwa nyota huyo kutoka Marekani ya Kusini
anafanana na hadhi ya PSG na shaka yoyote uwezo wake.
"hajawahi
kunipigia simu. Mimi si rafiki yake alikuwa mchezaji wangu nilipokuwa Milan, lakini
kiukweli ana vigezo vya kuichezea PSG"
"ni
mfungaji mzuri lakini hatuwesi kusaini wafungaji wote wazuri duniani. Tuna wachezaji
katika nafasi hiyo kama vile Jeremy Menez, Ezequiel Lavezzi na Zlatan
Ibrahimovic."
Wenger ajitetea baada yua kushindwa
kuwafunga Aston Villa.
Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger amesema kuwa kilicho wafanya washindwe kuifunga Aston Villa na
kwenda sare ya bila mabao ni mchoko.
Washika mtutu
walishinda kutengeneza nafasi dhidi ya Villa na kulazimika kugawana alama moja
kila upande matokeo ambayo yamewaweka mbele kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Chelsea
katika msimamo wa ligi.
Mchezo wa
katikati ya wiki dhidi ya Montpellier ilipelekea meneja huyo kuwapumzisha vijana
wake kutoka katika jiji la London Jack Wilshere, Bacary Sagna na Thomas
Vermaelen katika mchezo huo.
Wenger anaamini
mchezo wa katikati ya wiki ulikuwa ni sehemu ya sababu za vijana wake kucheza
chini ya kiwango jambo ambalo hakulipinga kuwa walikuwa chini ya kiwango.
Arsenal imefunga
goli moja tu katika michezo mitatu iliyocheza ugenini.
Matokeo hayo
yanamfanya wenger kusema
"ni
kweli. Ila sijui sababu ni nini. Tuna timu nzuri ya ulinzi na tuna wachezaji
wazuri wazuiaji sehemu ya kiungo na tuna washambuliaji watatu, lakini hii inaweza
kutokea iliwakutokea huko nyuma ni tofauti unapocheza nyumbani na ugenini."
No comments:
Post a Comment