Geoffrey Kizito anaecheza soka Vietnam akipongezwa baada ya kufunga goli pekee la ushindi dakika ya 74 ya mchezo wa Cranes dhidi ya Harambee Stars. |
Timu za taifa
ya Ethiopia na wenyeji Uganda zimefanikiwa kuanza vizuri michezo yao ya mwanzo
ya michuano ya kombe la Challenge iliyoanza hii leo mjini Kampala nchini Uganda.
Hii ni
michezo ya kundi la A ambapo mchezo wa mapema timu ya taifa ya Ethiopia ambao
mwezi Januari watakuwa wakielekea nchini Afrika Kusini waliwachapa Sudani
Kusini kwa bao 1-0.
Mshambuliaji
Yonathan Kebede alifunga bao hilo pekee kunako dakika ya 60 kufuatia mpira wa
krosi kutoka mashariki ya uwanja wa Nambole.
Nahodha Leon
Khamis alipata nafasi mbili nzuri pengine kama angezitumia vizuri basi pengine
wangechomoza na ushindi mnono zaidi.
Hata hivyo
kocha msaidizi wa Ethiopia Seyoum Kebede, amesema pamoja na ushindi huo kikosi
chake kitalazimika kuongeza jitihada zaidi.
“ni vizuri
tumeshinda mchezo wetu wa kwanza wa michuano hii lakini tunalazimika kuongeza
jitihada zaidi”.
Katika mchezo
wa pili ambao Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou alikuwa
akiushuhudia wenyeji Uganda wamefanikiwa kuanza vema kampeni yao ya kutete taji
hilo wakianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Harambee
Stars ya Kenya.
Mchezaji nyota
anayechezea soka nchini Vietnam Geoffrey Kizito alifunga goli hilo pekee zikiwa
zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika.
Goli hilo
lilikuja mfupi baada ya mlinda mlango namba moja wa Uganda ‘The Cranes’ Abel
Dhaira akipelekwa katika gari la wagonjwa baada ya kugongana na mlinzi wa
Harambee stars katika harakati za kuokoa mpira wa shambulizi.
Michezo mingine
ya kundi A itaendelee tena jumanne ambapo Ethiopia wataanza mchezo wa mapema
dhidi ya Uganda na baadaye Kenya kukutana na Sudani Kusinin.
Michuano hiyo
itaendelea tena hapo kesho kwa michezo ya kundi B ambapo mchezo wa mapema Burundi
wataanza na Somalia na baadaye Kilimanjaro stars watakuwa wakishuka dimbani
dhidi ya Sudan.
No comments:
Post a Comment