KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 23, 2012

AHADI NI DENI MANJI ASAINI MAKUBALIANO YA UPEMBUZI AKINIFU NA BCEG JUU YA UJENZI WA UWANJA WA JANGWANI.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji kulia akisaini hati ya makubaliano ya upembuzi akinifu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Beijing Construtcion Geng Hijuan.
Klabu ya Yanga leo imesaini makubaliano ya upembuzi akinifu na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, juu ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa Kaunda katika eneo la makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 
 Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa uongozi na kamati ya utendaji na kujadili juu ya hatua hiyo ambayo kampuni ya BCEG itaanza kazi wiki ijayo na pindi watakapokalmilisha michoro zoezi litakalofuata litakua awawu ya ujeni wenyewe.

"Hiki ni kipindi cha kufanya shughuli za kimaendeleo na hasa kipindi hiki ambacho klabu yetu ipo katika amani na mshikamano kwa viongozi na wanachama, hivyo naamin mara tutakapomaliza suala la uwanja tutaanza pia ujenzi wa jengo la kitega uchumi mtaa wa mafia" amesema 'Manji'.

Naye Mkurugenzi wa shirika la BCEG nchini, bwana Geng Hijuan amesema amefurahi kufikia hatua hiyo na klabu ya Young Africans, kazi waliyopewa sasa wataifanya kwa uhakika mzuri na kutoa makadirio halisi juu ya gharama ambazo zitagharimu kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya BCEG kutoka nchini China ndiyo iliyojenga uwanja wa Taifa wa kisasa jijini Dar es salaam na sasa ndio waliopewa kazi ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Kaunda.

Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemseama, makadirio ya uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu thelathini (30,000) mpaka elfu arobaini (40,000) kutegemea na wataalam watakavyoona, pia utakua na huduma zote za muhimu katika viwanja vya kisasa.

Manji amesema mategemeo ya Kamati yake ya Utendaji ni kuanza kujengwa kwa uwanja huo mapema kabla ya mwezi juni mwakani, ambapo desemba 8 mwaka huu watasubiria kupata baraka za wanachama katika mkutano mkuu.

No comments:

Post a Comment