UTANGULIZI
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limezifanyia marekebisho kadhaa
baadhi ya Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom ili kuondokana na migogoro isiyokuwa ya
lazima. Mabadiliko haya lengo lake kuu ni kuwa na Ligi iliyo bora zaidi, ambayo
itaweza kuleta ushindani kwa timu
shiriki na pia kutoa burudani zaidi kwa watazamaji, pamoja na kuchochea
wadhamini zaidi kujitokeza kwa ajili ya kudhamini ligi na timu shiriki.
Ligi iliyo bora, itawezesha kupata wachezaji bora watakaounda timu bora ya
Taifa itakayoweza kufanya vizuri katika medani ya kimataifa na pia tutaweza
kupata klabu zitakazotuwakilisha vyema katika mashindano ya kimataifa kwa ngazi
ya klabu. Mafanikio haya yataweza kukuza
na kuendeleza kiwango cha soka katika nchi yetu na pia kuijengea heshima Tanzania
katika ulimwengu wa soka.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linafahamu na linaamini kuwa mpira wa
miguu ni mchezo wenye nguvu, unaopendwa na watu wengi duniani na unaoweza
kuvutia watu wengi kuwekeza iwapo kanuni, taratibu na sheria za mchezo huu
zitafuatwa na kuheshimiwa na pia kanuni za ‘fair play’ zitazingatiwa na
wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi, washabiki, na wengine wote ambao kwa
njia moja au nyingine wanahusika na mchezo wa soka.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linaagiza kilabu, makocha, na waamuzi
kuzisoma kwa makini kanuni hizi na kuhakikisha zinaeleweka na kufuatwa kwa
faida ya mchezo wa mpira wa miguu.
Shirikisho linapenda kuwakumbusha watu wote kuwa soka kama ilivyo
michezo mingine yote inalindwa na sheria pamoja na kanuni. Bila sheria michezo itakuwa ni vurugu
tupu. Shirikisho linaziomba kilabu
kuhakikisha kuwa kanuni hizi pia zinaeleweka vizuri kwa wachezaji na washabiki
wake, kwani itasaidia kuwafanya
wafahamu kanuni na taratibu za mpira wa miguu vizuri zaidi na kwa
kuzifahamu kanuni zaidi, zitawafanya wawe wachezaji bora zaidi na
wataepuka kuadhibiwa kwa makosa ambayo yanaweza kuepukika.
Kanuni na sheria huwekwa kwa ajili ya kuufanya mchezo uwe na ladha katika
kuucheza na pia uwe na ladha katika kuuangalia na hivyo kuufanya uwe na
burudani zaidi. Tukitumia nguvu na
‘spirit’ ya soka inavyotakiwa, tutaweza kujenga jamii na dunia bora yenye afya
zaidi, upendo, amani, furaha na usawa.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania siku zote litahakikisha mchezo wa
soka unakuwa na heshima kwa kusimamia kwa uadilifu kanuni na sheria za mchezo
huu, kutoa adhabu inapobidi, kuelimisha na kuhakikisha siku zote mshindi
anapatikana uwanjani kwa kufuata kanuni na taratibu za mchezo na siyo kwa
kutumia njia chafu zisizokubalika.
MICHEZO NI FURAHA
NA AJIRA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
YALIYOMO
YALIYOMO
Na Kanuni Ukurasa
SURA YA KWANZA
Kuundwa, Matumizi na
Tafsiri
1. Kuundwa 7
2. Matumizi na Tafsiri 7
SURA YA PILI
Daraja, Aina na Namna ya
Uendeshaji Ligi
3. Daraja la Ligi 8
4. Namna ya Uendeshaji wa Ligi
Kuu ya Vodacom 8
5. Uwanja wa Nyumbani na
Ugenini 9
6. Mshindi wa Ligi 9
7. Msimu wa Ratiba ya Ligi 10
SURA YA TATU
Taratibu za Mchezo
8. Taratibu za Mchezo 10
9. Kuahirisha Mchezo 16
10. Waamuzi 16
SURA YA NNE
Huduma ya Kwanza na Bima
11. Huduma ya Kwanza 17
12. Bima 17
SURA YA TANO
Ada ya Ushiriki na
Usimamizi wa Ligi
13. Ada ya Ushiriki na Usimamizi
wa Ligi 18
14. Usimamizi wa Ligi 18
15. Kamati ya Nidhamu 18
SURA YA SITA
16. Kamati ya Rufaa 18
17. Rufani na Utaratibu Wake 18
18. Utaratibu wa Kuwasilisha
Malalamiko 19
19. Ada na Rufaa 20
SURA YA SABA
20. Mgawanyo wa Mapato 20
21. Gharama za Mchezo 21
SURA YA NANE
22. Kujitoa Katika Ligi 22
23. Kutofika Kituoni/Uwanjani 23
24. Kuvuruga Mchezo 24
25. Kupanga Matokeo 25
SURA YA TISA
Udhibiti wa Mienendo na
Adhabu kwa Wachezaji, Waamuzi na Viongozi
26. Uchezaji wa Kiungwana (Fair Play) 25
27. Udhibiti wa Wachezaji 29
28. Udhibiti na Adhabu kwa
Waamuzi 30
29. Udhibiti wa Kamishna 31
30. Udhibiti wa Mtathimini
32
31. Udhibiti wa Walimu 33
32. Udhibiti wa Viongozi 34
33. Adhabu kwa Klabu 35
34. Viwango na Utaratibu wa
Adhabu kwa Wachezaji 36
SURA YA KUMI
Usajili na Uhamisho wa
Wachezaji
35. Kipindi cha Usajili 37
36. Hadhi ya Wachezaji 38
37. Kupata Upya Hadhi ya
Ridhaa 38
38 Kuacha Shughuli 38
39. Usajili 39
40. Vipindi vya Usajili 39
41. Pasi ya Wachezaji 40
42. Maombi ya Usajili 40
43. Hati ya Uhamisho ya Kimataifa 41
44. Kuazimwa
kwa Mkopo Wachezaji wa Kulipwa
41
45. Wachezaji Wasiosajiliwa 42
46. Masharti Maalum Yanayohusu Mikataba kati ya
Wachezaji wa Kulipwa na Klabu 42
47. Usajili na Uhamisho wa Wachezaji 44
48. Uthibitisho wa Usajili 44
49. Majina ya Wachezaji 44
50. Idadi ya Wachezaji 44
51. Klabu/Wachezaji Wanaositisha au kumaliza Mikataba 45
52. Wachezaji Waliopandishwa 45
53. Wachezaji Huru 45
54. Wachezaji wa Kuhamishwa 45
55. Wachezaji Kutoka Nje ya Nchi 46
56. Ngazi za Uthibitisho wa Usajili 46
57. Kutengua Uthibitisho wa Usajili 46
58. Katazo 47
59. Uhamisho wa Mchezaji 47
60. Uhamisho Kwenda Zanzibar 48
SURA YA KUMI NA MOJA
Adhabu Zihusuzo Usajili na Uhamisho
61. Adhabu Zinazohusu Usajili na Uhamisho 49
62. Uhamisho Nje ya Nchi 50
SURA YA KUMI NA MBILI
Mengineyo
63. Mwalimu wa Timu 51
64. Daktari wa Timu 51
65. Timu za Pili na Watoto 52
66. Adhabu zisizokatiwa rufaa 52
67. Udhamini 52
68. Lesseni ya kushiriki ligi kuu 52
69. Utumiaji wa madawa ya
kuongeza nguvu 53
70. Ufafanuzi 53
71. Tafsiri 53
72. Marekebisho ya Kanuni 53
73. Kufuta Kanuni 53
74. Mambo Yasiyomo Kwenye Kanuni
Hizi 54
NYONGEZA
Jedwali la Kwanza
18 (5) Ada za Usajili na Uhamisho wa
Wachezaji
55
19 (B) Mgawanyo wa Ada za Usajili na
Uhamisho wa 56
Wachezaji Kutoka Tanzania
Bara Kwenda Tanzania Zanzibar
SURA YA KWANZA
KUUNDWA, MATUMIZI NA TAFSIRI
KANUNI YA 1
KUUNDWA
Kanuni hizi zimeundwa chini ya Ibara ya 34 (1.K) ya katiba ya TFF ya mwaka
2006 na zitatumika Tanzania Bara.
KANUNI YA PILI 2
MATUMIZI NA TAFSIRI
Katika Kanuni hizi isipokuwa pale ambapo imeainishwa vinginevyo:-
“FIFA” tafsiri yake ni “Federation Internaltionale
de Football Association” ikiwa na maana ya Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya
Mpira wa Miguu.
“CECAFA” tafsiri yake ni: Council of East and Central Africa Football
Associations” ikiwa na maana ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu la Nchi za
Afrika Mashariki na Kati.
“TFF” tafsiri yake ni Tanzania Football Federation”, ikiwa na maana ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.
“Kamati ya Utendaji” maana yake ni Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania.”
“ZFA” tafsiri yake ni: “Zanzibar Football Association”,
ikiwa na maana ya Chama cha mpira wa Miguu Zanzibar.
“FRAT” tafsiri yake ni “Football
Referees Association of Tanzania”, ikiwa na maana ya Chama cha Waamuzi wa Mpira
wa Miguu Tanzania.
“TAFCA” tafsiri yake ni “Tanzania Football Coaches Association” ikiwa na
maana ya Chama cha Walimu wa Mpira wa Miguu Tanzania.
“TASMA” tafsiri yake ni Tanzania Sports Medicine Association ikiwa na maana
ya Chama cha Wataalamu wa Tiba kwa Wanamichezo Tanzania.
‘Sputanza’ Soccer Players Union of
Tanzania tafsiri yake chama cha wachezaji wa soka Tanzania
“Kilabu” maana yake ni kilabu cha mpira wa miguu.
“Timu” maana yake ni Timu ya Mpira wa Miguu
“Mpira” maana yake ni Mpira wa Miguu.
SURA YA PILI
DARAJA, AINA NA
NAMNA YA UENDESHAJI LIGI
KANUNI YA 3
DARAJA LA LIGI
Kanuni hizi ni kwa ajili ya Ligi Kuu.
KANUNI YA 4
NAMNA YA UENDESHAJI
WA LIGI KUU YA VODACOM
Ligi Kuu itashirikisha timu kumi na nne (14) tu yaani timu tisa (11) zilizobaki
toka msimu uliopita na timu tatu (3) zilizopanda daraja.
·
Vilabu vinatakiwa
kusajili timu za vijana TFF kabla ya Ligi kuu kuanza;
·
Timu zitacheza Ligi
ya mikondo miwili nyumbani na ugenini;
·
Timu tatu (3) za
mwisho katika msimamo wa Ligi zitashuka daraja.
KANUNI YA 5
UWANJA WA NYUMBANI
NA UGENINI
(1)
Uwanja wa nyumbani
ni ule uliochaguliwa na timu husika na uwanja wa ugenini ni ule ambao timu
pinzani imekaribishwa kucheza.
(2)
Kutoka na sababu za
kiusalama au uwanja kutofikika au sababu nyingine yeyote ya msingi. TFF kwa
kushauriana na timu husika Endapo timu yoyote haina uwanja wa nyumbani unaofaa
kwa mashindano ya Ligi, timu husika inaweza kuchagua kwa idhini ya TFF, uwanja
mwingine wowote, hata nje ya mji huo au Mkoa ili mradi Uwanja huo uwe jirani na
mkoa wa timu husika ndani ya Tanzania Bara na uwe na sifa zinazokubalika.
KANUNI YA 6
MSHINDI WA LIGI
(1)
Mshindi katika mchezo wowote wa ligi atapatikana kwa
kufunga magoli mengi zaidi ya timu pinzani.
(2)
Mshindi atapata pointi tatu (3)
(3)
Endapo timu zitatoka sare ya aina yoyote, kila timu
itapata alama moja.
(4)
Timu itakayoshindwa itakosa pointi.
(5)
Mshindi katika ligi ni timu iliyopata pointi nyingi zaidi
ya timu zote zilizoshiriki katika Ligi hiyo.
(6)
Ikiwa
timu mbili zitalingana kwa pointi baada ya michezo mshindi atapatikana kwa
tofauti bora ya magoli ya kufungwa na kufunga, na kama tofauti hiyo haitoi
mshindi, mshindi atakuwa ni mwenye magoli mengi ya kufunga, kama pia magoli ya
kufunga hayatoi mshindi; basi mshindi atakuwa ni yule atakayekuwa na pointi
nyingi kwenye michezo miwili iliyohusisha timu hizi mbili, na kama pia michezo
hiyo haitoi mshindi, mshindi atakuwa yule aliyefunga magoli mengi zaidi katika
mchezo wa ugenini uliozihusisha timu hizi mbili, iwapo bado haitoi mshindi,
mshindi atakuwa aliyefunga magoli mengi ya ugenini katika msimu mzima, iwapo
bado haitoi mshindi timu hizi zitacheza mchezo mmoja katika uwanja
utakaochaguliwa na TFF, na taratibu zote za kupata mshindi zitafuatwa kama
mchezo wa fainali.
(7)
Mshindi
wa kwanza wa Ligi atakuwa bingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara na atapewa
kikombe cha ubingwa.
(8)
Mshindi
wa kwanza wa LIGI KUU atawakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya Kilabu
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati.
(9)
Mshindi wa kwanza wa LIGI
KUU ataiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya Kilabu Bingwa Afrika (Champions League). Mshindi wa pili
atawakilisha katika kombe la Mabara kwa vilabu iwapo hakutakuwa na FA Cup.
(10)
Wawakilishi
wa mashindano ya Kilabu bingwa na Kombe la shirikisho watashiriki katika mchezo
wa ufunguzi wa msimu wa ngao ya hisani.
(11)
Timu
yeyote itakayochaguliwa kucheza mashindano yatakayoandaliwa ama kuidhinishwa na
TFF kutokana na nafasi yao katika ligi kuu itawajibika kucheza.
KANUNI YA 7
MSIMU WA RATIBA YA LIGI
1. Kamati ya Utendaji ya TFF itatangaza
tarehe za kuanza na kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu.
2. Ratiba ya Ligi itaandaliwa na
kutolewa na TFF angalau mwezi mmoja kabla ya Ligi kuanza.
3. Ratiba ya Ligi ikishatolewa
haitabadilishwa isipokuwa kama kuna dharura au sababu nzito na za msingi.
SURA YA TATU
KANUNI YA 8
TARATIBU ZA MCHEZO
(1) Kutakuwa na mkutano wa kitaalamu wa
maandalizi kabla ya mchezo (pre-match meeting) ambao utafanyika kabla ya
mchezo. Mkutano huu utafanyika saa 4.00 asubuhi siku ya mchezo. Kwa sababu
maalum, mkutano huu unaweza kupangiwa muda, siku na mahali pengine kama
itakavyopendekezwa na Chama cha Mpira cha Mkoa na kuidhinishwa na TFF. Timu
zinazocheza siku hiyo pamoja na waamuzi na kamisaa wanatakiwa kuhudhuria.
(2) Timu yoyote itakayochelewa kufika
kwenye Mkutano wa kitaalamu wa maandalizi ‘Pre match meeting’ au itakayoleta
watu wasiohusika au wasiokuwa na vitambulisho itatozwa faini ya TShs 100,000/=
na timu itakayoshindwa kufika kwa sababu zisizo za msingi itatozwa faini ya
TShs 200,000/=.
(i)
Taarifa
ya ukiukwaji wa vipengele hivi itawasilishwa na Kamisaa na Msimamizi wa Kituo.
(ii)
Faini
zote zitalipwa mara tu baada ya mchezo kumalizika kwa kukata kwenye mapato ya
timu. Endapo mapato ya timu ya mchezo huo hayatoshi watakatwa kwenye mchezo
unaofuata.
(3) (a) Wafuatao ndio wanaotakiwa kufika
kwenye mkutano wa maandalizi na vitambulisho vyao vilivyotolewa na TFF,
asiyekuwa na kitambulisho hicho hatoruhusiwa kuhudhuria kikao :-
(i)
Mwalimu msaidizi
(ii)
Mtunza vifaa wa Timu
(iii)
Daktari wa Timu.
(iv)
Meneja wa Timu
.
(b) Kila timu inatakiwa kufika na
vitu vifuatavyo:-
(i)
Seti moja ya jezi za wachezaji wa ndani pamoja
na jezi mbili za walinda milango zenye namba kubwa zinazosomeka zinazoanzia na
nambari 1 hadi 52. Endapo rangi za sare za timu zote mbili zitafanana, timu
ngeni italazimika kubadilisha sare yake. Endapo moja ya jezi za timu itafanana
na jezi za waamuzi, waamuzi watalazimika kubadilisha. Taratibu za mabadiliko ni
lazima zijulikane kwenye mkutano wa maandalizi tu.
(4) Jezi ya
mlinda mlango isifanane rangi na jezi za wachezaji wa ndani lakini inaweza
kufanana na jezi ya mlinda mlango wa timu pinzani.
(5) Mchezaji
atakayevaa jezi isiyokuwa na nambari mgongoni ama itakayobandikwa kwa plasta au
kitu chochote kile hataruhusiwa kucheza.
(6) Viwanja
vyote vitakavyotumika kwa michezo yote vitaidhinishwa na TFF.
(7) TFF ina
madaraka ya mwisho ya kuhamisha mchezo au kubadilisha kituo cha mchezo kwa
sababu inazoona zinafaa kwa mchezo au mashindano husika.
(8) Manahodha
wa timu zinazoshindana wanatakiwa kuvaa vitambulisho vya rangi tofauti na jezi
zao kwenye mikono ya jezi zao.
(9) Kila mchezaji
ni lazima avae kizua ugoko “shinguard” kwenye miguu yote miwili.
(10) Wachezaji
wanaruhusiwa kushangilia goli kwa wastani. Ushangiliaji wa kupitiliza, kiasi
cha kupoteza muda hasa kutoka uwanjani na kufanya ishara yoyote isiyokuwa ya
kiuanamichezo au ya kashfa au matusi kwa timu pinzani au watazamaji
hairuhusiwi. Mchezaji/wachezaji watakaofanya vitendo hivyo wataadhibiwa kwa kufungiwa michezo isiyozidi
mitatu au faini ya laki moja au vyote kwa pamoja. Mchezaji atakayevua jezi
kushangilia ataonyeshwa kadi ya njano.
(11) Michezo
yote ya ligi itachezwa kwa vipindi viwili vya jumla ya dakika tisini (90) kila
kipindi kikiwa na dakika arobaini na tano (45) na mapumziko ya dakika
zisizopungua tano (5) na zisizozidi kumi tano (15) kati ya vipindi hivyo.
(12) Timu
zinatakiwa kufika kiwanjani si chini ya dakika (60) kabla ya wakati uliopangwa
kuanza mchezo. Michezo inayoonyeshwa moja kwa moja na Luninga muda utapangwa
kulingana na muda uliokubaliwa na pande zote za mchezo wa siku hiyo na
warushaji.
(13) Timu itakayochelewa kufika kwa mujibu wa
masharti ya Kanuni ya 8 Kifungu cha 12; itatozwa faini ya sh. 300,000/=.
(14) Timu
zitakaguliwa kwenye vyumba vyao vya kuvalia na endapo rangi za sare za timu
zote zitafanana timu ambayo haikufika kwenye kikao cha maandalizi italazimika
kubadili jezi.
(i)
Kila kilabu itasajili TFF rangi ya jezi
zake kwa mechi za nyumbani na ugenini kabla ya kuanza msimu wa Ligi. Kilabu itakayokiuka itatozwa faini ya Tshs.
300,000/=
(ii)
Vyumba vya kuvalia wachezaji vitapangwa na
msimamizi wa kituo, kwa timu ya nyumbani na ugenini. Sehemu ya kufanyia mazoezi
na benchi la wachezaji wa akiba itakuwa upande ule ule wa vyumba vya
kuvalia. Kilabu itakayokiuka itatozwa
faini ya shilingi za 300,000/=.
(iii)
Ni marufuku kwa viongozi kuingia
uwanjani kinyume na taratibu za mchezo kabla, wakati au baada ya mchezo. Timu itakayokiuka kipengele hiki itatozwa
faini ya shilingi 300,000/=.
(iv)
Ni marufuku kwa mashabiki kuingia
uwanjani kabla, wakati au baada ya mchezo. Timu itakayokiuka kipengele hiki
itatozwa faini ya sh. 300,000/=.
(15) Endapo timu
zitakaguliwa na mgeni rasmi kiwanjani kwa kupeana naye mikono, au timu kupeana
mikono zenyewe na waamuzi zitalazimika kufanya hivyo kwa heshima zote zinazostahili. Timu itakayokosa kupeana mkono na mgeni rasmi
na/au msafara unaoongozana na mgeni rasmi, na/au waamuzi na/au timu pinzani kwa
sababu yeyote itatozwa faini ya Tshs. 500,000/=.
(16) Wakati
wa mapumziko, timu zitalazimika kwenda kupumzika kwenye vyumba vyao vya
kuvalia. Timu zinalazimika kupitia
kwenye milango/mageti na siyo vinginevyo.
Timu itakayokiuka itatozwa faini ya Tshs. 500,000/=.
(17) Timu
yoyote hairuhusiwi kuruka ukuta wa nje ili kuingia uwanjani (“Stadium”) ama
kuruka uzio wa ndani unaotenga
watazamaji na Uwanja (“Pitch”), ama kupita katika mlango wowote usio rasmi. Endapo timu itafanya hivyo itatozwa faini ya
sh. 500,000/=.
(18) Pamoja na adhabu iliyoainishwa katika
Kanuni ya 8 (14, 15, 16 na 17), Shirikisho linaweza kutoa adhabu ikiwemo ya timu
husika kupoteza mchezo na kumfungia mchezaji, kiongozi, au shabiki yeyote wa
timu husika kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.
(19) Mwalimu mkuu au mwalimu msaidizi wa timu
anatakiwa kuwasilisha kwa Kamishina wakati wa kukaguliwa orodha iliyo na
wachezaji 18 na viongozi watano ambao wameorodheshwa katika fomu maalumu
iliyoandaliwa na TFF kwa madhumuni hayo. Formu hiyo italazimika kujazwa kwa
unadhifu na ukamilifu.
(20) Timu itatumia wachezaji walioorodheshwa
katika fomu hiyo tu, mchezaji ambaye hakuoorodheshwa hatahesabika kama mchezaji
wa siku hiyo.
(21) Wachezaji wote watatambulika kwa
kutumia vitambulisho vyao vilivyoidhinishwa na TFF; katika mashindano hayo.
Mchezaji yeyote ambaye hatakuwa na kitambulisho hatoruhusiwa kushiriki katika
mchezo.
(22) Iwapo itathibitika bila kujali
kukatwa au kutokatwa Rufaa, kupitia taarifa za mchezo za Kamisaa ama kwa njia
yoyote kuwa timu imechezesha mchezaji/wachezaji ambao si halali au ni batili
kiusajili (non qualified) timu hiyo itapoteza mchezo na ushindi kupewa timu
pinzani.
(23) Timu ambayo itawasilisha fomu isiyo
kamili itachukuliwa kuwa haijawasilisha fomu hiyo.
(24) Endapo timu imeshindwa kuwasilisha
fomu iliyotajwa katika Kanuni ya 8 (20) itakuwa imekiuka Kanuni hiyo na timu
husika itatozwa faini ya Sh. 100,000/= ambazo zitalipwa kutokana na mchezo au
michezo ya timu husika.
(25) Wanaoruhusiwa kukaa kwenye benchi la
wachezaji wa akiba ni wachezaji saba (7) wa akiba na viongozi watano (5) ambao
ni mwalimu Mkuu, mwalimu Msaidizi, Daktari, Mchua misuli na Mtunza vifaa wa Timu.
(26) Mwamuzi atalazimika kutoanzisha
mchezo hadi masharti ya Kanuni ndogo ya (25) ya Kanuni hii yametekelezwa.
(27) Endapo hata baada ya Mwamuzi kuitaka
timu itekeleze masharti ya Kanuni ya 8 (25) timu husika ikashindwa kufanya
hivyo; basi timu hiyo itatozwa faini ya sh. 500,000/=. Mwamuzi ataomba msaada
wa wanausalama kuwaondoa wasiohusika kabla ya kuanzisha mchezo.
(28) Mwamuzi na Kamishna wa mchezo
wanatakiwa kutoa taarifa zao za maandishi kwa TFF, endapo hali iliyoelezwa
katika Kanuni ndogo ya (27) ya Kanuni hii itatokea.
(29) Chama cha Mpira cha ngazi husika
kitapeleka kiwanjani mipira miwili au zaidi yenye sifa zinazokubalika kisheria
itakayotumika kwa ajili ya mchezo. Kila
timu inatakiwa kufika kiwanjani angalau na mpira mmoja wenye sifa hizo hizo.
(30) Ni marufuku kwa timu yoyote kukataa
kuchezea mpira wowote uliochaguliwa na mwamuzi.
(31) Mwamuzi ataanzisha mchezo iwapo tu
kama kuna mipira miwili au zaidi yenye sifa zinazokubalika kisheria.
(32) Endapo timu yoyote itakataa kuchezea
mpira wowote uliochaguliwa na mwamuzi na kusababisha mchezo huo kuvunjika, timu
hiyo itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapata ushindi wa pointi tatu na
magoli matatu.
(33) Endapo timu yoyote itakataa kuchezea
mpira wowote uliochaguliwa na mwamuzi na kusababisha mchezo huo kuchelewa
kuanza na baadaye mchezo ukalazimika kuvunjwa kabla ya dakika tisini (90)
kwisha kwa sababu ya giza timu iliyosababisha mchezo kuvunjika itapigwa faini
ya 500,000/=, itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapata ushindi wa pointi
tatu (3) na magoli matatu (3).
(34) Mwamuzi ataanzisha mchezo iwapo kila
timu ina wachezaji 11. Endapo timu
yoyote haitimizi wachezaji 11, mchezo unaweza kuanzishwa ikiwa tu wachezaji wa
kila timu hawapungui saba (7) mmoja wao akiwa mlinda mlango. Lakini Kanuni hii haitahusu timu iliyosalia
na wachezaji pungufu ya saba kutokana na baadhi yao kuumia au kutolewa nje na
mwamuzi wa mchezo.
(35) Timu inaruhusiwa kubadilisha
wachezaji watatu (3) tu wa akiba kutoka kwenye orodha ya wachezaji saba (7) wa
akiba.
(36) Timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu
pamoja na waamuzi, endapo watapewa na mdhamini, jezi na suti za michezo, timu
pamoja na waamuzi wanatakiwa wahakikishe wanavaa vifaa hivi kwenye michezo yote
ya Ligi Kuu.
(37) Iwapo kutakuwa na mdhamini wa ligi
Kuu, Nembo ya mdhamini itawekwa mikononii .Wadhamini wengine wote nembo zao
zitawekwa mgongoni na kifuwani. Hata hivyo mdhamini binafsi wa klabu ataweka
nembo yake kifuani. Timu itakayokuwa na jezi zake italazimika kuweka nembo ya
mdhamini katika jezi hizo kwa kufuata utaratibu huo na hairuhusiwi kuweka
matangazo ya kampuni nyingine ambayo ina ushindani wa moja kwa moja kibiashara
na mdhamini wa Ligi kuu. Matangazo au mabango ya wadhamini wa klabu yatawekwa kwenye uwanja wa nyumbani
(Timu mwenyeji) tu na si uwanja wa ugenini isipokuwa kwa makubaliano maalum
kati ya klabu ngeni na mwenyeji.
(38) Kila Kilabu kinalazimika kuheshimu
Mikataba ya udhamini inayowekwa na TFF.
Timu itakayoshindwa kutekeleza kipengele namba 36 na 37 cha kanuni hizi
itatozwa faini isiyopungua 1,500,000/= kwa kila mchezo na pia inaweza
kuchukuliwa hatua zingine zaidi zikiwemo kupoteza sifa ya kushiriki Ligi kuu na kufungiwa.
(39) Mwamuzi ambaye hatovaa jezi na suti
ya michezo yenye nembo ya mdhamini ataondolewa katika orodha ya waamuzi
wanaochezesha ligi kuu.
(40) Kilabu chochote kinachotaka kuingia
mkataba na mdhamini kinalazimika kuwasilisha rasimu ya mkataba huo kwa TFF
kabla ya kutia sahihi.
(41) Timu itakayokosa kufika uwanjani na
kusababisha mchezo kutofanyika baada ya kushiriki kikao cha maandalizi ya
mchezo, itatozwa faini ya shilingi 5,000,000/=, kulipa fidia ya uharibifu
wowote unaoweza kijitokeza kushushwa daraja na viongozi waliosababisha
watachukuliwa hatua zaidi za kinidhamu.
KANUNI YA 9
KUAHIRISHA MCHEZO
Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana
na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
(a) Endapo timu ya Taifa ina mchezo.
(b) Endapo timu inashiriki katika
mashindano ya Kimataifa na ina muda usiozidi siku sita kufikia mchezo wa
Kimataifa;
(c) Sababu yoyote ya dharura au/ na yenye
msingi itakayokubaliwa na TFF.
(d) Matukio yasiyotarajiwa wala
kusababishwa na timu husika.
(e) Mchezo wowote ulioahirishwa chini ya
kipengele 9 (a),(b) na (c) utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na TFF
isipokuwa kama utaahirishwa chini ya kipengele 9 (d) utachezwa siku inayofuata
iwapo ratiba inaruhusu.
(f) Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika
kwa sababu ya matukio ya dharura yasiotarajiwa wala kusababishwa na timu
husika, utapangwa kurudiwa kwa muda uliosalia, magoli yaliyofungwa katika
mchezo huo, Kadhalika kadi walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo uliovunjika
zitaendelea kuhesabika.
(g) Taarifa ya maombi ya kuahirisha
mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi si chini ya siku 14 kabla ya siku ya
mchezo, isipokuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu.
KANUNI YA 10
WAAMUZI
Katika mchezo wowote Uamuzi wa Mwamuzi wa mchezo ni wa
mwisho.
Kila Mwamuzi atawasilisha TFF mara tu baada ya mchezo taarifa
ya mchezo aliouchezesha iliyojazwa katika fomu maalum katika muda usiozidi saa
24.
Taarifa ya Mwamuzi iliyotajwa katika Kanuni ya 10 (2)
inatakiwa ijazwe kwa unadhifu na ukamilifu.
Mwamuzi atakayeshindwa kutoa taarifa sahihi ya mchezo kwa
mujibu wa Kanuni ya 10 (2) ataondolewa katika orodha ya waamuzi wanaochezesha
Ligi kuu na atafungiwa kwa muda usiozidi miezi kumi na mbili (12).
Waamuzi wa mchezo watapangwa na TFF na klabu chochote
hakiruhusiwi kumkataa mwamuzi yeyote.
Waamuzi watakaochezesha Ligi ni wale wa Daraja la FIFA na
Daraja la kwanza waliofaulu jaribio la utimamu wa mwili (“Physical Fitness Test”)
na kuteuliwa kuchezesha ngazi ya Ligi Kuu.
Kutafanyika jaribio la utimamu wa mwili (“Physical Fitness Test”)
kila mwaka kabla ya Ligi kuanza ikiambatana na mtihani wa kuandika na
mahojiano.
SURA YA NNE
KANUNI YA 11
HUDUMA YA KWANZA NA BIMA
Chama cha Mpira ngazi husika ni
lazima kihakikishe kuwa katika mchezo wowote wa Ligi Kuu panakuwepo huduma ya
kwanza na gari la wagojwa, kadhalika kihakikishe katika kila mchezo kunakuwepo
na Daktari.
KANUNI YA 12
BIMA
(1) Viongozi na wachezaji wote lazima
wawekewe bima na vilabu vyao hati ya bima iwasilishwe pamoja na fomu za usajili
wa wachezaji. Kilabu kitakachokiuka
Kanuni hii hakitashirikishwa katika michuano yoyote inayosimamiwa na TFF.
(2) Chama cha Walimu wa Mpira wa Miguu
(TAFCA) kihakikishe kwamba wanachama wake wanawekewa Bima na Vilabu husika.
(3) Chama cha Madaktari wa Michezo
Tanzania (TASMA) kihakikishe kwamba wanachama wake wanawekewa Bima na Vilabu
husika.
(4) Chama cha Wachezaji (SPUTANZA) kihakikishe kwamba wanachama wake wanawekewa Bima
na Vilabu husika.
SURA YA TANO
KANUNI YA 13
ADA YA USHIRIKI NA USIMAMIZI WA LIGI
1. Ada ya ushiriki wa Ligi Kuu ni TShs
300,000/=.
2. Kutakuwa na fomu za maombi ya
kushiriki kwenye Ligi, tarehe ya mwisho kuthibitisha itatangazwa na TFF. Maombi
hayo yataambatana na ada ya ushiriki, maombi yasiyo ambatana na ada
hayatapokelewa. Klabu itakayoshindwa kuthibitisha kushiriki hadi kufikia tarehe
ya mwisho ya kufanya hivyo itakuwa imejiondoa yenyewe kwenye Ligi na kujishusha
daraja.
KANUNI YA 14 A
USIMAMIZI WA LIGI
1. Ligi kuu itasimamiwa na chombo maalum
kilichopewa mamlaka hayo na Kamati ya utendaji ya Shirikisho. Kwa kipindi cha
mpito cha kuunda chombo hicho madaraka ya usimamizi wa ligi yatakuwa kwa kamati
ya ligi.
KANUNI YA 15 B
KAMATI YA NIDHAMU
Kamati ya nidhamu itatoa maamuzi kwa
masuala yote ambayo hayaja ainishwa katika kanuni ya sitini na nne (64).
SURA YA SITA
KANUNI YA 16
KAMATI YA RUFAA
Rufaa zote
zinazohusiana na maamuzi ya kamati ya nidhamu zitasikilizwa na kamati ya rufaa:
(1) Ni
marufuku kupeleka malalamiko yoyote dhidi ya TFF kwa masuala yahusuyo soka
katika mahakama za sheria. Klabu au mtu yeyote atakayepeleka malalamiko yake
katika mahakama za sheria atachukuliwa hatua kali ikiwamo kufutwa kabisa
kujishughulisha na mchezo wa soka.
(2) Endapo
mrufani/mrufaniwa hakuridhika na maamuzi ya kamati ya rufaa apeleke shauri lake
‘CAS’
(3) Muda wa
kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa iwapo mrufani au mrufaniwa hajaridhika na
maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ni si zaidi ya siku tano za kazi.
KANUNI YA 17 B
RUFANI NA UTARATIBU WAKE
Rufaa zote
zinazohusiana na Ligi ya Kuu ya Vodacom zitasikilizwa na kamati ya Rufaa ya TFF
chini ya utaratibu ufuatao:
(1) Kamati
ya Rufaa itasiliza rufaa zote zinazopinga maamuzi ya kamati ya Nidhamu na
Usuluhishi ya TFF.
(2) Ni,
marufuku kupeleka malalamiko yoyote
dhidi ya chama cha mpira ngazi
yoyote kwa masuala yahusuyo soka katika mahakama za sheria. Kilabu au mtu
yeyote atakayepeleka malalamiko yake katika mahakama za sheria atachukuliwa
hatua kali ikiwamo kufutwa kabisa kujishughulisha na mchezo wa soka.
(3) Muda wa
kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa iwapo mrufani au mrufaniwa hajaridhika na
maamuzi ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ni si zaidi ya siku tano za kazi
baada ya kupata maamuzi ya kamati ya Nidhamu na Usuluhishi.
(4) Rufani
ya kupinga maamuzi ya kamati ya Nidhamu na Usuluhishi iwasilishwe kwa maandishi
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania sio zaidi ya siku tano za kazi baada ya kupata maamuzi ya kamati
ya nidhamu na usuluhishi na iwe imeambatanishwa na ada ya rufaa pamoja na
vielelezo vyote vya shauri hilo.
(5) Rufani
yeyote itayowasilishwa bila ya vielelezo haita sikilizwa.
(6) Rufani
yeyote ambayo haitalipiwa ada haitasikilizwa.
(7) Rufani
yoyote itakayowasilishwa baada ya muda uliowekwa chini ya kanuni hii,
haitasikilizwa na ada ya rufaa haitarudishwa kwa mrufani.
KANUNI YA 18
UTARATIBU WA KUWASILISHA MALALAMIKO.
(a) Malalamiko
dhidi ya matukio ya mchezo yawasilishwe
kwa maandishi kwa Kamishna wa mchezo au ofisi ya TFF sio zaidi ya masaa 24 baada
ya mchezo kumalizika.
(b) Kamishna
wa mchezo atawasilisha kwenye Sekretarieti ya TFF sio zaidi ya saa ishirini na
nne (24) tangu kupokea malalamiko hayo.
(c) Kamati husika
itaketi kusikiliza na kuyatolea uamuzi malalamiko hayo katika kipindi
kisichozidi wiki moja, baada ya kupata
vielelezo husika. Mlalamikaji atawasilisha vielelezo kuhusu malalamiko yake na malalamiko
yasiyokuwa na vielelezo hayatasikilizwa.
(d) Malalamiko
yoyote yatakayowasilishwa baada ya muda uliowekwa chini ya kanuni hii, hayatasikilizwa.
KANUNI YA 19
ADA ZA RUFAA
Ada ya rufaa katika Kamati ya Rufaa ni TShs 500,000/=
SURA YA SABA
KANUNI YA 20
MGAWANYO WA MAPATO
Kila timu itajihudumia yenyewe, timu zilizocheza zitagawana
asilimia 59 ya mapato ya mchezo baada ya kutoa gharama za awali.
Mgawanyo wa mapato ya mchezo utakuwa kama ifuatavyo:-
Jumla ya Pato xxxx
Toa 18% VAT xxxx
Toa: Usafiri wa ndani na
Posho ya waamuzi, kamisaa,
msimamizi wa waamuzi na
msimamizi wa kituo xxxx
Maandalizi ya uwanja xxxx
Gharama za Tiketi xxxx
Baki ya Pato xxxx
9% Gharama za mchezo; xxxx
9% Msimamizi wa Ligi Kuu xxxx
4.5% FDF; xxxx
15% Uwanja; xxxx
3.5% FA (M) xxxx
29.5%
Klabu ngeni xxxx
29.5% klabu mwenyeji xxxx
3. Endapo timu moja itahamia uwanja wa
Mkoa mwingine mbali ya ule wa nyumbani sehemu ya mapato ya 3.5% ya Chama cha
Mpira cha Mkoa itagawanywa kama
ifuatavyo:
(a) Mkoa unaotoka timu husika utapata
nusu ya 1.75%
(b) Mkoa utakaohusika na uwanja utapata
nusu ya 1.75%
4. Msimamizi wa Kituo atawasilisha
taarifa ya mapato na fedha za mchezo husika kwa TFF katika muda usiozidi masaa
24. Kiongozi au Msimamizi atakayeshindwa kuwasilisha atachukuliwa hatua kwa
mujibu wa Kanuni za TFF.
5. ( i) Gharama
za Waamuzi na kamisaa ni nauli ya kutoka kwenye Kituo alichotokea,
usafiri wa treni Daraja
la Pili, Basi au Meli.
(ii) Usafiri
wa ndani wa Waamuzi kwa ujumla wao Sh. 20,000/= na kamisaa 20,000/=.
(iii) Chakula na malazi 70,000/= kwa kila mwamuzi na kamisaa.
(iv) Mwamuzi wa mezani atalipwa Sh. 50,000/=.
(v)
Kamisaa atalipwa posho ya mchezo Sh. 100,000/=
(vi)
Mwamuzi na wasaidizi wawili (2)
watalipwa posho ya mchezo Sh. 100,000/= kwa kila mmoja.
(vii)
Posho zilizotajwa kwenye kipengele
No . (i) hadi (iv) cha kanuni hii zitalipwa kutoka katika mapato ya
mchezo. Posho zilizotajwa kwenye kipengele No. (v) na (vi) zitalipwa na
mdhamini wa ligi.
KANUNI YA 21
GHARAMA ZA MCHEZO
1. Asilimia 9% ya gharama za mchezo itatumika
kulipia gharama zifuatazo:-
(i)
Gharama
za msimamizi wa kituo.
(a) Msimamizi kutoka nje ya kituo
atalipwa gharama za kula na kulala 70,000/= na nauli kutoka kituo chake na
kurudi.
(ii)
Malipo
ya ulinzi, vijana wanaookota mipira, huduma ya kwanza, vinywaji, wasimamizi,
wauzaji na wachanaji tiketi, matangazo na “stationari”.
(iii)
Msimamizi mkazi atalipwa shilingi laki
moja (100,000/=) za posho na shilingi elfu ishirini (20,000/=) kama usafiri wa
ndani. Msimazi kutoka nje atalipwa shilingi 100,000/=, usafiri wa ndani
shilingi 20,000/= na nauli ya kwenda na
kurudi.
2. Mtiririko wa gharama hizo utaonyeshwa kwenye
Fomu ya Mapato, msimamizi wa kituo atawajibika na usimamizi wa gharama za
mchezo.
Malipo yatalipwa kwa hundi kama Kanuni za fedha zinavyosema
isipokuwa waamuzi na makamisaa.
Iwapo gharama halisi ni pungufu ya 9% zilizokatwa kama
gharama za mchezo, fedha zitakazobaki zitagawanywa nusu kwa nusu kati ya vilabu
na TFF, yaani TFF itachukua 50% na vilabu vitagawana 50% nyingine. Mgawanyo wa fedha hizi unatakiwa uandikwe
kwenye fomu ya gharama za mchezo isainiwe na msimamizi wa kituo kwa niaba ya
TFF na wawakilishi wa vilabu kwa niaba ya vilabu vyao.
SURA YA NANE
KANUNI YA 22
KUJITOA KATIKA LIGI
(1) Endapo Kilabu chochote kina nia ya
kujitoa katika Ligi kwa sababu zozote zile za msingi ni lazima itoe taarifa ya
maandishi kwa TFF kikieleza sababu zinazokilazimisha kilabu hicho kijitoe, siku
thelathini kabla ya ligi kuanza.
(2) Endapo TFF imekubali kujitoa kwa
kilabu chochote, klabu kingine ambacho awali kilikuwemo katika daraja hilo
lakini kiliteremka kwa mujibu wa msimamo wa Ligi, kitarudishwa kuziba
pengo. Kilabu hicho ni kile kilicho
katika nafasi ya juu kuliko vilabu vingine vyote vilivyoteremka daraja katika
msimu huo.
(3) Kilabu kilichojitoa kitateremka daraja.
(4) Kilabu chochote kitakachojitoa katika
Ligi baada ya Ligi kuanza au kushindwa kucheza mchezo mmoja katika msimu mmoja
wa Ligi kitakabiliwa na adhabu zifuatazo:
(a) Kitateremka daraja na kufungiwa
kucheza Ligi kwa misimu 2. Kamati ya Utendaji ya TFF pia inaweza kukichukulia
hatua zaidi klabu hicho/viongozi au wachezaji iwapo itathibitika kuwa kimejitoa
kwa madhumuni ya kuhujumu msimamo wa Ligi au hujuma nyingine yoyote.
(b) Iwapo klabu zitakazojitoa au
kushindwa kumaliza Ligi kwa sababu yoyote ile zitakuwa ni zaidi ya tatu (3)
kama kanuni za Ligi za timu kushuka daraja zinavyosema; timu zote hizo
zitashuka daraja na timu zaidi zitapanda kutoka daraja la kwanza ili kujaza
nafasi na idadi ya timu za Ligi kuu kuendelea kuwa 14.
(c) Matokeo ya michezo yote iliyowahi
kuchezwa yatafutwa lakini kitakuwepo kwenye orodha ya msimamo wa ligi.
(d) Magoli yaliyofungwa na wachezaji wa
timu iliyojitoa katika ligi yatafutwa na hivyo wachezaji wake hawataweza
kushindana katika ufungaji bora hata kama walifunga magoli mengi lakini magoli
yaliyofungwa na wachezaji wa timu pinzani dhidi ya timu iliyojitoa kwenye ligi
hayatafutwa na hivyo yataendelea kuonekana katika idadi ya magoli yaliyofungwa
na wachezaji hao lakini hayataonekana katika idadi ya magoli yaliyofungwa na
klabu zao
KANUNI YA 23
KUTOFIKA KITUONI/UWANJANI
Timu yoyote itakayokosa kufika
kituoni na kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu zifuatazo:
(a) Itapoteza ushindi na kushushwa madaraja
mawili na matokeo ya michezo yake yote yatafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa
timu zilizobaki kwenye mashindano, na endapo timu ilikuwa kwenye kushuka daraja
timu hiyo husika itashushwa madaraja mengine.
(b) Itatozwa faini ya TShs 3,000,000/=
ambazo kati ya hizo Tshs 1,500,000/= itaenda TFF na TShs 1,500,000/= itaenda
kwa timu pinzani.
(c) Itapoteza haki ya kuchukua sehemu
yake ya mapato ya mchezo huo.
(d) Kiongozi yeyote atakayebainika kuwa
alishiriki, alishawishi au alikuwa chanzo cha mgomo huo atafungiwa kwa kipindi
cha miezi kumi na miwili.
(e) Inaweza ikakabiliwa na adhabu zaidi
kama ambavyo Kamati ya Utendaji itaona inafaa.
(f) Timu yoyote iliyopewa adhabu ya faini
chini ya aya ya (b) ya Kanuni hii haitaruhusiwa kucheza hadi itakapotekeleza
adhabu hiyo kwa daraja ambalo itakuwa ipo.
KANUNI YA 24
KUVURUGA MCHEZO
1. Wachezaji
na viongozi wa timu itakayosababisha mchezo kuvurugika na hatimaye kuvunjwa,
itapoteza mchezo huo hata kama ilikuwa inaongoza kwa magoli na timu pinzani
itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu, iwapo timu pinzani inaongoza
kwa magoli zaidi ya matatu, itabakia na idadi ya magoli hayo iliyokwishafunga.
2. Magoli
yaliyofungwa na wachezaji wa timu iliyosababisha mchezo kuvunjika yatafutwa
lakini magoli yaliyofungwa na timu pinzani hayatofutwa na yataendelea kuonekana
katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wa
kutafuta mfungaji bora.
3. Endapo
itatokea vurugu ya aina yoyote ile na kusababisha mchezo kusimama, mwamuzi
atasubiri kwa dakika zisizozidi kumi na tano, na endapo hali ya vurugu bado
inaendelea mwamuzi atavunja mchezo na kuwasilisha taarifa ya mchezo kwa kamati
ya Usimamizi ya ngazi husika.
4. Timu iliyosababisha vurugu itapoteza
mapato yote ya mchezo.
5. Timu
iliyosababisha kuvurugika kwa mchezo italipa faini ya shilingi 1,000,000/=.
6.
Faini hiyo italipwa kabla ya mchezo unaofuatia.
7.
Mchezaji/wachezaji na kiongozi/viongozi watakao bainika
kusababisha vurugu zilizopelekea mchezo huo kuvunjika watafungiwa kujihusiha
namasuala yote ya mpira kwa kipindi cha miaka mitano.
8.
Endapo uvunjikaji
wa mchezo utakuwa nje ya kanuni ya 22(3), mchezo huo utarudiwa kama inavyoainishwa
katika kanuni ya 9(e) na utachezeshwa na waamuzi wengine katika siku itakayo
pangwa na chombo husika.
KANUNI YA 25
KUPANGA MATOKEO
1. Endapo timu
zozote zitabainika kuwa zimepanga kwa namna yoyote ile matokeo ya mchezo wowote
waliocheza kwa madhumuni yoyote yale zitachukuliwa hatua zifuatazo:-
2. Matokeo ya
mchezo huo yatafutwa; na kila timu itatozwa faini ya shilingi millioni tano
(5,000,000/=).
3. Timu zitateremshwa hadi ligi ya wilaya;
4. Viongozi wa
timu hizo waliohusika na njama za kupanga matokeo watafungiwa kwa kipindi cha
miaka mitano;
5. Iwapo
timu husika itashindwa kulipa faini basi timu hiyo haitapangwa katika mchezo wa
ligi msimu unaofuata.
SURA YA TISA
UDHIBITI WA MIENENDO NA ADHABU KWA
WACHEZAJI, WAAMUZI NA VIONGOZI
KANUNI YA 26
UCHEZAJI WA KIUNGWANA (FAIR PLAY)
Wachezaji wanatakiwa kuzingatia
kanuni za mchezo wa kiungwana ‘fair play’ ndani na nje ya uwanja wa mchezo.
Kanuni 10 za FIFA za mchezo wa kiungwana ni kama ifuatavyo:
i.
Cheza Kiungwana – Ushindi hauwezi kuwa na thamani
iwapo umepatikana katika njia isiyo halali au kwa udanganyifu. Kudanganya ni
rahisi lakini haileti raha ya ushindi. Kucheza kiungwana inahitaji moyo na
tabia njema. Pia hufurahisha zaidi. Mchezo wa kiungwana siku zote una malipo
yake hata kama utapoteza mchezo. Kucheza kiungwana kunakujengea heshima wakati
kudanganya kunaleta aibu. Kumbuka kuwa mpira wa miguu ni mchezo na mchezo
wowote hauwezi kuwa na maana kama hautochezwa kiungwana kwa kuzingatia kanuni
na taratibu ili mshindi halali aweze kupatikana.
ii. Cheza kwa nia ya kutafuta ushindi lakini pia kuwa tayari kukubali
kushindwa – Kushinda
ndiyo lengo la kushiriki katika mchezo wowote ule. Siku zote usijiandae
kushindwa. Iwapo huchezi kwa nia ya kushinda utakuwa unawadanganya wapinzani
wako, unawadhulumu watazamaji na pia unjifanya mwenyewe kuwa ni mjinga. Usikate
tamaa hata siku moja unapombana na wapinzani wenye nguvu zaidi lakini pia
usidharau hata siku moja unapombana na wapinzani dhaifu. Ni kumkosea adabu
mpinzani unapocheza chini ya kiwango chako. Cheza kwa nia ya kutafuta ushindi hadi
dakika ya mwisho lakini kumbuka hakuna anayeshinda wakati wote. Siku nyingine
utashinda na siku nyingine utashindwa. Jifunze kukubali kushindwa. Usitafute
visingizio unapofungwa. Sababu za kweli siku zote zitadhihirika. Wapongezi
washindi bila kinyongo. Usilaumu waamuzi wala mtu mwingine yoyote. Jizatiti
kufanya vizuri zaidi wakati mwingine. Walioshindwa na kukubali wanapata heshima
kubwa kuliko washindi wanaolazimisha.
iii. Heshimu sheria za mchezo – Michezo yote inalindwa na sheria. Bila sheria itakuwa ni
vurugu. Sheria za mpira wa miguu ni nyepesi na rahisi kujifunza. Hakikisha
unajifunza; itakusaidia kuufahamu mpira wa miguu vizuri zaidi. Kuufahamu mchezo
zaidi itakufanya uwe mchezaji bora zaidi. Pia ni muhimu kufahamu madhumuni ya
sheria zilizowekwa. Zimekusudiwa kuufanya mchezo uwe na ladha katika kuucheza
na pia uwe na ladha katika kuuangalia. Kwa kufuata sheria, mchezo wa mpira wa
miguu utakuwa na burudani zaidi.
iv.
Heshimu wapinzani, wachezaji wenzako,
waamuzi, viongozi na watazamaji – Mchezo wa kiungwana unamaanisha kuheshimu wapinzani. Bila ya
wapinzani kutakuwa hakuna mchezo. Kila mmoja ana haki sawa, ikiwemo haki ya
kuheshimiwa. Wachezaji wa timu moja ni wenza. Tengeneza timu ambayo kila mmoja
kwenye timu atakuwa na haki sawa. Waamuzi wapo kuhakikisha nidhamu na mchezo wa
kiungwana unadumishwa. Siku zote kubali maamuzi yao bila ya ulalamishi, na
wasaidie waweze kuwafanya washiriki wote waufurahie zaidi mchezo. Viongozi pia
ni sehemu ya mchezo na wanatakiwa wapewe heshima wanayostahili. Watazamaji wanaufanya
mchezo uwe na msisimko. Wanahitaji kuuona mchezo ukichezwa kiungwana kwa
kuzingatia kanuni, lakini pia wanatakiwa kuwa waungwana na kujiheshimu.
v. Dumisha Maslahi ya mchezo wa mpira wa miguu – Mpira wa miguu ndiyo mchezo
unaoongoza duniani kwa kuwa na wapenzi wengi. Lakini siku zote unahitaji msaada
wa kila mmoja kuufanya uendelee kuwa mchezo wenye kupendwa zaidi. Fikiria
maslahi ya mpira kabla ya maslahi yako mwenyewe. Fikiria ni vipi vitendo vyako
vinaweza vikaupaka matope mchezo wa mpira wa miguu. Zungumzia mambo mazuri ya
mchezo wa mpira wa miguu. Shawishi watu wengine kuuangalia na kuucheza
kiungwana. Wasaidie wengine kupata burudani ya kutosha katika mchezo wa mpira
wa miguu kama unayoipata wewe. Kuwa balozi wa mchezo wa mpira.
vi. Waheshimu wale wanaolinda heshima ya mchezo wa mpira wa miguu – Jina zuri la mchezo wa mpira wa
miguu limeendelea kudumu kwa sababu idadi kubwa ya watu wenye kuupenda mchezo
huu ni wakweli na waungwana. Wakati mwingine mtu hufanya jambo kubwa ambalo
linastahili tulitambue. Watu kama hawa wanastahili kutuzwa na mambo mema
waliyofanya yatangazwe. Hii itashawishi wengine kuiga mifano yao. Saidia
kuendeleza mpira wa miguu kwa kuyatangaza mazuri yake.
vii. Kataa rushwa, madawa, ubaguzi, fujo, kamari na mambo mengine ya hatari kwa
mchezo wetu –
Umaarufu mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu wakati mwingine huufanya uwe rahisi
kuathiriwa na mambo mabaya ya nje. Jichunge na vishawishi vitakavyokufanya
ushawishike kushiriki kwenye kudanganya au kutumia madawa yaliyokatazwa. Madawa
yaliyokatazwa hayana nafasi katika soka wala mchezo mwingine wowote na jamii
kwa jumla. Sema hapana kwa madawa ya kulevya. Saidia kuupiga teke ubaguzi
kwenye soka. Wachukulie wachezaji wote na wengineo kuwa ni sawa bila kujali
dini, kabila, jinsia au utaifa wao. Usivumilie hata kidogo kamari katika
michezo unayoshiriki. Inaporomosha kiwango chako cha uchezaji na inasababisha
hali ya mgongano wa maslahi. Thibitisha kuwa soka haihitaji fujo, hata kutoka
kwa washabiki wako wenyewe. Soka ni mchezo na michezo huleta amani.
viii. Wasaidie wengine kupambana na mashinikizo ya upokeaji rushwa – Wakati mwingine unaweza kusikia
wachezaji wenzako au watu wengine unaowafahamu wanashawishiwa wadanganye kwa
njia moja au nyingine au washiriki katika vitendo visivyokubalika katika mchezo
wa soka. Wanahitaji msaada wako. Usisite kusimama upande wao. Wape nguvu ya
kukataa vishawishi. Wakumbushe wajibu wao kwa wenzao na kwa mchezo wenyewe.
Tengeneza umoja wenye mshikamano, kama ngome ngumu kabisa kwenye mchezo wa
soka.
ix. Wabainishe wale wanaojaribu kuuchafua mchezo wetu – Usione aibu kusimama dhidi ya yoyote
yule ambaye una hakika anashawishi
wengine kudanganya au kushiriki katika vitendo vingine visivyokubalika. Ni
vyema kuwafichua waovu wote ili waweze kuondolewa kabla ya kuleta madhara. Ni
uovu kushirikiana na watu waovu. Usiseme tu hapana, wafichue wanaotaka
kuichafua soka kabla hawajafanikiwa kuwashawishi wengine.
x. Tumia soka kujenga dunia bora zaidi – Soka ina nguvu ya ajabu ambayo inaweza kutumika
kuifanya dunia hii ikawa sehemu bora zaidi ya kuishi. Tumia nguvu hii kudumisha
amani, usawa, afya na elimu kwa wote. Ifanye soka iwe bora zaidi, ipeleke kwa
jamii na utakuwa unajenga dunia bora zaidi.
Pamoja na kanuni za Fair Play za
FIFA, kadhalika wachezaji wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:
a) Nidhamu –
kudumisha tabia njema nje ya uwanja na wakati wote wa mchezo kwa kucheza bila
ya kuwaumiza au kuhatarisha usalama wa wachezaji wa timu pinzani.
b) Mchezo wa kiungwana – Kutodanganya kuumia au kufanyiwa rafu, kutotumia mbinu zisizo za
kiungwana mchezoni au kujiingiza katika vitendo visivyokuwa vya kiunamichezo
kama vile kutukana kwa maneno, ishara au kujihusisha na vitendo vyovyote vya
kibaguzi.
c) Kutorejeshea – kutorejeshea ‘retaliation’ iwapo
mchezaji atafanyiwa rafu au kukashifiwa.
d) Malalamiko – Ni nahodha pekee ambaye anaruhusiwa
kuzungumza na waamuzi. Iwapo patatokea malamiko yoyote wakati wa mchezo
wachezaji wengine wote wanatakiwa wawe hatua zisizopungua kumi kutoka kwa
mwamuzi.
e) Kumheshimu Kocha – Mchezaji wakati wote anatakiwa atii maagizo ya kocha wake. Mchezaji
anatakiwa akubali kubadilishwa uwanjani na kuadhibiwa kutokana na vitendo vya
utovu wa nidhamu au visivyokuwa vya kiuanamichezo.
f) Kumheshimu nahodha – Mchezaji anatakiwa amheshimu na atii maagizo ya nahodha wake nje na
ndani ya uwanja hususan katika masuala yahusuyo timu na tabia njema kwa jumla.
g) Kuheshimu wachezaji – Mchezaji anatakiwa awaheshimu wachezaji wenzake na awatie hamasa nje na
ndani ya uwanja. Mchezaji anatakiwa asimkashifu mchezaji mwenzake mwenye
kufanya makosa.
h) Kuheshimu wapinzani – Mchezaji anatakiwa awape wachezaji wa timu pinzani heshima yao, awe
tayari kutoa msaada kwa mchezaji aliyeumia na kushikana mikono kabla na baada
ya mchezo.
i) Kuheshimu waamuzi – Mchezaji anatakiwa wakati wote kuheshimu maamuzi ya waamuzi na kutozozana
nao au kutumia lugha ya matusi au kashfa dhidi yao.
j) Kujiheshimu mwenyewe – Mchezaji anatakiwa ajiheshimu
mwenyewe na ajitunze na asitumie madawa yaliyokatazwa.
KANUNI YA 27
UDHIBITI WA WACHEZAJI
(1) TFF itadhibiti mienendo ya wachezaji
kwa kuchukua hatua kama ifuatavyo:-
(a) Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi
nyekundu baada kupata kadi mbili za njano katika mchezo wa ligi hataruhusiwa
kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake.
(b) Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi
nyekundu ya moja kwa moja (straight red) atakosa michezo miwili.
(c) Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi
nyekundu kwa kosa la kupiga/kupigana atasimama kushiriki michezo (3) mitatu inayofuata
ya kilabu yake na atalipa faini ya shilingi za laki (500,000/=) tano za
kitanzania.
(d) Timu ambayo wachezaji wake
wataonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja itatozwa faini ya shilingi
za kitanzania laki tano (500,000/=).
(e) Mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya
njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata.
(f) Kilabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi 3
za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa
pointi 3 na magoli 3, iwapo mchezaji atacheza akiwa anatakiwa kutocheza kwa
ajili ya kadi tatu za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo
kilabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa
maandishi toka TFF.
(g) Mchezaji yeyote atakayefanya jambo
lolote kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kwa kufungiwa michezo isiyopungua
mitatu (3) na faini isiyopunguwa Tshs; 500,000/=:
(i)
Kuto
kujiunga na Timu ya Taifa kwa sababu yoyote isiyo ya msingi .
(ii)
Kupigana/kupiga kabla au mara tu baada
ya mchezo kumalizika.
(iii)
Kumshambulia
mwamuzi, kiongozi, mtazamaji au mtu yoyote
kwa namna yoyote ile, iwe kwa matusi au kwa vitendo.
(iv)
Kufanya
kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani, kukataa kupeana mkono
na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa matusi au kuonyesha
ishara yoyote inayoashiria matusi;
(v)
Kusababisha
kuvurugika kwa amani kiwanjani kabla au baada ya mchezo;
(vi) Kufanya
vitendo vyenye kuonyesha imani za ushirikina na uchawi hadharani; kama vile
kuvunja nazi, kupasua mayai, kufukia hirizi na kumwaga maji ya makombe n.k.
(vii) Kufanya
kitendo chochote kinyume cha maadili ya mchezo wa mpira. Kwa mfano kuruka uzio
badala ya kupita kwenye mlango maalum.
(viii)
Timu
yoyote itakayomchezesha mchezaji aliye chini ya adhabu kwa mujibu wa Kanuni hii
itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi.
(ix)
Mchezaji
sugu atafungiwa kushiriki mashindano yeyote kwa miezi isiyopunguwa mitatu (3)
na faini isiyopunguwa Tshs: 1,000,000/= (milioni moja)
(h) Mchezaji yoyote atakayetakiwa kufanya vipimo
vya dawa za kulevya au kuongeza nguvu, anawajibika kufanya hivyo, endapo atagundulika/atakataa
kuwa anatumia madawa ya kulevya au kuongeza nguvu/kufanya hivyo atafungiwa kwa
kipindi cha miezi kumi na mbili (12).
KANUNI YA 28
UDHIBITI NA ADHABU KWA WAAMUZI
1. Mwamuzi yeyote atakayefanya jambo lolote
kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kama ilivyoainishwa katika Kanuni hii:-
(a) Akishindwa kumudu mchezo kwa uzembe,
woga au kutozingatia sheria kiasi cha kuvuruga mchezo, kuhatarisha amani,
atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita (6) na kisichozidi miezi kumi
na miwili (12).
(b) Akichelewa kwa zaidi ya saa ishirini
na nne (24) kutuma taarifa ya mchezo bila sababu za msingi ataadhibiwa kwa
mujibu wa kanuni ya 10 kipengele cha 4.
(c) Akibainika kuwa anadai hongo au
amepokea/ametoa hongo /au kuhusika na matendo yeyote yanayo ashiria hongo ikiwa
ni pamoja na kutoa taarifa ya mpango wa hongo, kutoa taarifa ya mchezo isiyo
sahihi kwa makusudi atafungiwa miaka mitatu au maisha.
(d) Akishindwa
kufika au akichelewa kufika bila sababu ya msingi au kutotoa taarifa, kwenye
kituo cha mchezo alichopangiwa kiasi cha kusababisha ratiba ya waamuzi
kurekebishwa au mchezo kuahirishwa, ataondolewa kwenye orodha ya waamuzi na
atafungiwa kwa kipindi kati ya miezi 3 - 12.
(e) Akifanya
kitendo chochote ambacho ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uamuzi kama vile
kuhudhuria kikao cha maandalizi ya awali ya mchezo husika/au kuchezesha mchezo
husika akiwa amelewa atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili
(12).
(f) Mwamuzi
atakayemaliza mchezo kabla ya wakati/au atakayeongeza muda wa mchezo bila ya
sababu za msingi atafungiwa kati ya miezi 6 – 12.
(g) Mwamuzi atakaebainika kushirikiana na
Kamisaa kuandika taarifa ili kuficha ukweli ataondolewa katika orodha ya
waamuzi wa Ligi Kuu na atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi 24.
(h) Mwamuzi akitoa visingizio visivyokua
na msingi ili kukwepa mchezo aliopangiwa atondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa
Ligi Kuu na Kamati inaweza kutoa adhabu nyingine itakavyoona inafaa.
KANUNI YA 29
UDHIBITI WA KAMISHINA
1. Kamishina yeyote atakayefanya jambo lolote
kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kama ilivyoainishwa katika Kanuni hii:-
(a)
Kamishna atakayeshindwa kutoa taarifa ya
mchezo ikiwemo taarifa ya mchezaji bora wa mchezo husika au akitoa taarifa isiyokuwa
sahihi, ataondolewa kwenye orodha ya makamishna wa michezo na atafungiwa kwa
kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
(b)
Kamishna atakayeshindwa kutoa taarifa
katika muda wa saa 24 ataondolewa katika orodha ya makamishna wa michezo na
atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita (6).
(c)
Akibainika
kuwa anadai hongo au amepokea/ametoa hongo /au kuhusika na matendo yeyote yanayo
ashiria hongo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya mpango wa hongo, kutoa
taarifa ya mchezo isiyo sahihi kwa makusudi atafungiwa miaka mitatu au maisha.
(d)
Kamishna atakayebainika kukataa kupokea
Rufaa kwa sababu zisizokuwa za msingi kwa njia yoyote ile, atafungiwa kwa
kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
(e)
Akifanya kitendo chochote ambacho ni
kinyume cha maadili ya taaluma ya ukamishina kama vile kuendesha kikao cha
maandalizi ya awali ya mchezo husika/au kusimamia mchezo husika akiwa amelewa
atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili (12).
(f)
Kamisaa atakaye bainika kushirikiana na
mwamuzi kuandika taarifa ili kuficha ukweli ataondolewa katika orodha ya
Makamisaa na atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi 24.
(g)
Kamisaa atayebainika kuendesha kikao cha
matayarisho na viongozi wa timu wasiohusika (kanuni 8(3)) ataondolewa kwenye
orodha ya makamisaa.
(h)
Kamisaa
akitoa visingizio visivyokua na msingi ili kukwepa mchezo aliopangiwa atondolewa
kwenye orodha ya makamisaa wa Ligi Kuu na Kamati inaweza kutoa adhabu nyingine
itakavyoona inafaa.
KANUNI YA 30
UDHIBITI WA MTATHIMINI WA WAAMUZI
(“REFEREE ASSESOR’’)
1. Mtadhimini wa waamuzi yeyote atakayefanya
jambo lolote kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kama ilivyoainishwa katika
Kanuni hii:-
(a)
Mtathimini atakayeshindwa kutoa taarifa
ya mchezo au akitoa taarifa isiyo sahihi, ataondolewa kwenye orodha ya
watathimini wa michezo na atafungiwa kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
(b)
Mtathimini atakayeshindwa kutoa taarifa
katika muda wa saa 24 ataondolewa katika orodha ya watathimini wa michezo na/au
atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita (6).
(c)
Akibainika
kuwa anadai hongo au amepokea/ametoa hongo /au kuhusika na matendo yeyote
yanayo ashiria hongo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya mpango wa hongo, kutoa
taarifa ya mchezo isiyo sahihi kwa makusudi atafungiwa miaka mitatu au maisha.
(d)
Mtathimini atakaye bainika kushirikiana
na mwamuzi/kamisaa kuandika taarifa ili kuficha ukweli ataondolewa katika
orodha ya watathimini na atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi 24.
(e)
Akifanya kitendo chochote ambacho ni
kinyume cha maadili ya taaluma ya utathimini wa waamuzi kama vile kuhudhuria kikao cha maandalizi ya
awali ya mchezo husika/au kufanya tathimini ya mchezo husika akiwa amelewa
atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili (12).
(f)
Mtathimini akitoa visingizio visivyokua na msingi ili kukwepa mchezo
aliopangiwa atondolewa kwenye orodha ya watathimini wa michezo na Kamati
inaweza kutoa adhabu nyingine itakavyoona inafaa.
KANUNI YA 31
UDHIBITI WA WALIMU
1. Mwalimu yeyote atakayefanya jambo
lolote kati ya haya yafuatayo ataadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni hii:-
(a) Akimshambulia mwamuzi, mchezaji au
kiongozi yeyote, kwa maneno au vitendo, kabla, wakati au baada ya mchezo,
atatozwa faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000/-) na kufungiwa michezo
isiyopungua mitatu (3), bila ya kujali adhabu yoyote iliyotolewa na mwamuzi
kiwanjani.
(b) Akitoa kauli au ishara inayoashiria
au kushawishi shari kabla, wakati au baada ya mchezo atatozwa faini isiyopungua
laki tano (500,000/=) na kufungiwa michezo isiyopungua mitatu (3).
(c) Akibainika kuwa anadai hongo au
amepokea/ametoa hongo /au kuhusika na matendo yeyote yanayo ashiria hongo ikiwa
ni pamoja na kutoa taarifa ya mpango wa hongo, kutoa taarifa ya mchezo isiyo sahihi
kwa makusudi atafungiwa miaka mitatu au maisha.
(d) Akijishirikisha na vitendo vyovyote
vile vinavyoashiria imani za uchawi au ushirikina atatozwa faini isiyozidi
shilingi laki tatu (300,000/=) na kufungiwa michezo isiyopungua miwili (2).
(e) Akifanya
kitendo chochote ambacho ni kinyume cha maadili ya taaluma ya ualimu wa mpira
wa miguu kama vile kuhudhuria kikao cha maandalizi ya awali ya mchezo husika/au
kusimamia benchi la ufundi katika mchezo husika akiwa amelewa atafungiwa kwa
kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili (12).
(f) Akibainika kugushi sahihi ya mchezaji
au kufanya tendo lolote kwa lengo la kukamilisha zoezi la usajili kwa
udanganyifu atafutwa katika ordha ya waalimu, leseni yake itatwaliwa na hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
(g) Mwalimu atakayebainika kusababisha
timu kutofika uwanjani na kukosa mchezo, baada ya kuhudhuria kikao cha
maandalizi, atatozwa faini ya shilingi 1,000,000/= na kufungiwa kwa kipindi
kisichopungua miezi kumi na mbili (12).
KANUNI YA 32
UDHIBITI WA VIONGOZI
1. Kiongozi yeyote atakayefanya jambo lolote
kati ya haya yafuatayo, ataadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni hii:-
(a) Akibainika kuwa anadai hongo au
amepokea/ametoa hongo /au kuhusika na matendo yeyote yanayo ashiria hongo ikiwa
ni pamoja na kushawishi waamuzi au wachezaji wa timu yake/timu pinzani
kupokea/kutoa hongo atafungiwa miaka mitatu au maisha.
(b) Akimshambulia Mwamuzi, mchezaji au
kiongozi mwingine yoyote, kwa maneno au vitendo, kabla, wakati au baada ya
mchezo atafungiwa kwa kipindi kisichozidi miezi sita.
(c) Akifanya kitendo chochote
kinachoashiria imani ya uchawi atafungiwa kwa kipindi cha miezi sita.
(d) Akifanya
kitendo chochote ambacho ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uongozi wa mpira
wa miguu kama vile kuhudhuria kikao cha maandalizi ya awali ya mchezo husika/au
kusimamia shughuli za mchezo husika akiwa amelewa atafungiwa kwa kipindi
kisichopungua miezi kumi na miwili (12).
(e) Akishindwa kutoa taarifa
zinazohitajika TFF kwa mujibu wa maagizo husika atafungiwa kwa kipindi kisichopungua
miezi mitatu (3).
(f) Akitoa taarifa isiyo sahihi kiasi cha
kupotosha maamuzi ya TFF atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na
miwili.
(g) Akitoa matamshi au ishara za matusi
dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya
kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, KILABU au TAIFA atatozwa
faini ya Sh. Milioni moja (1,000,000/=) na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua
miezi mitatu (3).
(h) Kiongozi au Kilabu itawajibika
kufuata na kutii maamuzi au maagizo ya TFF. Kiongozi atakayeshindwa kutii
maamuzi au maagizo hayo atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3)
na kutozwa faini ya Sh. Milioni moja (1,000,000/=). Kilabu itashindwa
kutekeleza maamuzi/maagizo husika itaondolewa kwenye mashindano na kushushwa
Daraja.
(i) Ni marufuku kwa kiongozi wa Kilabu kushutumu
au kutoa matamshi yenye lengo la kumkashifu au kumdhalilisha kiongozi wa
TFF/Chama cha Mpira cha ngazi husika kwenye vyombo vya habari. Kiongozi atakaye
kwenda kinyume na kanuni hii atafungiwa kwa kipindi kati ya miezi sita (6)
mpaka kumi na miwili (12) na faini ya shilingi miliono moja (1,000,000/=).
(j) Kiongozi akibainika kuhudhuria kikao
cha maandalizi ya mchezo kwa kujisingizia cheo kisicho kuwa chake atatozwa
faini ya shilingi 500,000/= na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu
(3).
(k) Uongozi ukibainika kugushi sahihi ya
mchezaji au kufanya tendo lolote kwa lengo la kukamilisha zoezi la usajili kwa
udanganyifu, kiongozi/viongozi husika wa klabu husika atafungiwa/watafungiwa
kwa kipindi kisichopungua miaka mitano na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake/yao.
(l) Kiongozi atakayebainika kusababisha
timu kutofika uwanjani na kukosa mchezo, baada ya kuhudhuria kikao cha
maandalizi, atatozwa faini ya shilingi 1,000,000/= na kufungiwa kwa kipindi
kisichopungua miezi kumi na mbili (12).
KANUNI YA 33
ADHABU KWA KLABU
(1) Kilabu kina wajibu na jukumu la
kuhakikisha kuwa wachezaji, viongozi, wanachama na wapenzi wake wanajiheshimu
na hawajihusishi na vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu kama vile matusi,
vitisho, vurugu, vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina na vitendo
vyovyote vingine visivyokuwa vya kimichezo kwenye viwanja vya michezo. Kilabu
ambacho washabiki wake watafanya vitendo hivyo kitatozwa faini ya TShs.
500,000/=. Mshabiki atakayekamatwa akifanya vitendo hivyo atachukuliwa hatua za
kisheria na atakayepatikana na hatia atafungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi
kisichopungua miezi 3 na kisichozidi miezi 12.
(2) Kilabu kitapoteza mchezo ambao
utavunjika kutokana na vurugu za washabiki wake.
(3) Kilabu pia zitawajibika kulipa
gharama za matibabu na kulipa gharama za mali zilizoharibika kwa waathirika wa
vurugu za washabiki wake zitakazofanyika kabla, wakati au baada ya mchezo.
(4) Kilabu zinatakiwa zihakikishe
viongozi wa kilabu husika waliosimamishwa na TFF kwa sababu moja au nyingine
kujishughulisha na uongozi wa klabu wanatii adhabu zao. Shirikisho litachukua
hatua itakayoona inafaa ikiwemo kuisimamisha klabu kushiriki katika ligi iwapo
klabu hiyo itaruhusu viongozi wake waliosimamishwa kujishughulisha na masuala
ya uongozi ndani ya kipindi cha adhabu.
(5) Kilabu kitakachoshindwa kuleta timu
uwanjani baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mchezo kitatozwa faini ya
shilingi milioni tano (5,000,000/=) na kushushwa daraja na, kiongozi
aliyeshiriki kutoleta timu uwanjani atafungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi
kumi na mbili (12), kutojishirikisha na masuala yote ya mpira wa miguu na
atatozwa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000/=).
KANUNI YA 34
VIWANGO NA UTARATIBU WA ADHABU KWA WACHEZAJI
(1) Kilabu chochote kinaweza kutoa adhabu
yoyote inayostahili dhidi ya mchezaji wake yeyote.
(2) Adhabu zote zitakazotolewa na vilabu
ni lazima zithibitishwe na TFF kabla adhabu hiyo haijaanza kutekelezwa.
(3) Kilabu hakitakuwa na mamlaka ya
kumfungia mchezaji kwa kipindi kinachozidi msimu wa ligi husika au kwa mchezaji
mwenye mkataba, zaidi ya kipindi cha mkataba wake na klabu.
(4) Kilabu hakitakuwa na mamlaka ya
kumfungia mchezaji yoyote nje ya nchi.
(5) TFF, pamoja na kuthibitisha adhabu
yoyote iliyotolewa na klabu, inaweza kufuta, kupunguza au kuongeza adhabu hiyo
ikiwa ni pamoja na kumfungia mchezaji huyo nje ya Nchi.
(6) Kabla Kilabu chochote hakijatoa
adhabu yoyote ni lazima mchezaji anayehusika apewe nafasi ya kujitetea.
(7) Kilabu chochote kitakachotoa adhabu
kwa mchezaji wake na kutuma taarifa hiyo TFF ili adhabu hiyo ithibitishwe,
kitalazimika kutuma TFF vielelezo vyote vinavyohusika ikiwa ni pamoja na
Muhtasari wa Kikao kilichotoa adhabu hiyo.
(8) Endapo mchezaji yeyote anaamini
ameonewa kutokana na adhabu aliyopewa na kilabu chake na ikathibitishwa na TFF,
anarushusiwa kukata rufaa, kupinga adhabu hiyo, kwa chombo husika.
SURA YA KUMI
HADHI USAJILI NA UHAMISHO WA WACHEZAJI
KANUNI YA 35
KIPINDI CHA USAJILI
(1) Usajili wa wachezaji ni suala la
kiufundi kama ilivyo kanuni ya 8 (3). Mwalimu Mkuu wa timu atawajibika kutambua
wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa. Katibu
Mkuu atafanya masuala ya utawala, atakamilisha zoezi la usajili wa wachezaji na
kuwasilisha mikataba na fomu ya majina TFF kwa wakati.
(2) Vilabu vinawajibika kutumia mikataba
iliyotayarishwa na Shirikisho kuhamisha/kuazima na kusajili wachezaji wake,
mikataba mingine yote haitatambulika.
(3) Kutangaza wachezaji ambao kilabu
inasitisha mikataba yao, uhamisho na usajili wa wachezaji utafanywa na walimu
wa vilabu katika kipindi kitakachotangazwa na TFF.
(4) Kutakuwa na vipindi vingine viwili
vya usajili, kipindi cha kwanza kitakuwa baada ya kumalizika Ligi na kipindi
cha pili kitakuwa katikati ya msimu wa Ligi Kuu. Tarehe za usajili wa vipindi vyote viwili
zitatangazwa na TFF. (kanuni Na 37 )
KANUNI YA 36
HADHI YA
WACHEZAJI
WACHEZAJI WA
RIDHAA NA WA KULIPWA
(1) Wachezaji wanaoshiriki katika Soka rasmi
ni wa ridhaa au wa
kulipwa.
(2) Mchezaji wa kulipwa ni
mchezaji mwenye mkataba wa maandishi na kilabu na analipwa zaidi ya gharama halisi anazoingia
kutokana na shughuli zake za soka. Wachezaji
wengine wote wanahesabiwa kuwa ni wa Ridhaa.
KANUNI YA 37
KUPATA UPYA HADHI
YA RIDHAA
1
Mchezaji aliyesajiliwa kama
Mchezaji wa kulipwa hawezi kusajiliwa tena kama wa ridhaa mpaka zipite angalau
siku 30 baada ya mechi ya mwisho aliyoecheza kama wa kulipwa.
2. Hakuna
fidia inayolipwa kwa kupata upya hadhi ya ridhaa. Iwapo mchezaji anasajiliwa upya kama wa
kulipwa katika kipindi cha miezi 30 ya kurudishiwa hadhi ya Ridhaa, Klabu yake
mpya italipa fidia ya mafunzo kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya kanuni ya FIFA.
KANUNI YA 38
KUACHA SHUGHULI
1. Wachezaji
wa Kulipwa wanaomaliza muda wao wa mkataba na wachezaji wa Ridhaa wanaomaliza
muda wao, watabaki kuwa wamesajiliwa katika Chama cha Mpira cha Nchi ambacho
Klabu yao waliochezea mwisho kwa kipindi cha miezi 30.
2. Kipindi hiki kinaanza siku ambayo mchezaji atachezea Klabu
mara ya mwisho katika mechi Rasmi.
KANUNI YA 39
USAJILI
1. Mchezaji lazima asajiliwe na Chama cha Soka ili kuchezea klabu
kama mchezaji wa Kulipwa au wa Ridhaa kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 2 ya
kanuni za FIFA. Ni wale wachezaji
waliosajiliwa tu ndio wanaostahili kushiriki katika Soka rasmi. Kwa kujisajili, ina maana mchezaji anakubali
kufuata Sheria na Kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Mashirikisho na Vyama vya Soka.
2. Mchezaji
anaweza kusajiliwa na kilabu moja tu kwa wakati huo.
3. Wachezaji wanaweza kusajiliwa katika kilabu hadi tatu kwa
kipindi cha tarehe 01 Julai hadi 30 Juni cha mwaka unaofuata. Katika kipindi hicho, mchezaji anastahili
kuchezea Mechi Rasmi katika kilabu mbili tu.
KANUNI YA 40
VIPINDI VYA
USAJILI
1. Wachezaji wanaweza kusajili tu kati moja ya vipindi viwili vya
Usajili vya mwaka vilivyopangwa na Chama cha Soka kinachohusika. Jambo la pekee katika Sheria hii, mchezaji wa
kulipwa ambaye Mkataba wake umekwisha kabla ya Kipindi cha Usajili anaweza
kusajiliwa nje ya Kipindi cha Usajili. Vyama
vya Soka vinaruhusiwa kusajili wachezaji hao wa kulipwa alimradi tu uzingativu
unaotolewa kwa kuaminika kimichezo kwa mashindano yanayohusika. Iwapo kuna sababu za msingi za kuvunjika kwa
mkataba, FIFA inaweza kuchukua hatua za muda ili kuepuka ukiukaji na kwa mujibu
wa Ibara ya 22 ya kanuni za FIFA.
2. Kipindi cha kwanza cha Usajili kitaanza baada ya kukamilika
kwa msimu na kwa kawaida hukamilika kabla Msimu Mpya haujaanza. Kipindi hiki hakizidi majuma kumi na
mawili. Kipindi cha Pili cha Usajili kwa
kawaida kitatokea katikati ya Msimu na hakitazidi majuma manne. Vipindi Viwili vya Usajili kwa Msimu
vitaarifiwa FIFA angalau miezi 12 kabla ya kuanza kutumika. FIFA itaamua tarehe kwa Chama chochote cha
Soka kitakachoshindwa kuwasilisha kwa wakati.
3. Wachezaji watasajiliwa tu itokeapo hali ya upekee kama
ilivyotabiriwa na Ibara ya 6, aya ya 1 ya kanuni za uhamisho wa wachezaji za
FIFA. Iwapo maombi ya Kilabu
yatawasilishwa kwa wakati kwa Chama kinachohusika wakati wa Kipindi cha
Usajili.
4. Masharti yanayohusu Vipindi vya Usajili hayatumiki kwa
mashindano ambayo Wachezaji wa Ridhaa tu wanashiriki. Kwa mashindano ya aina hiyo, Chama
kinachohusika kitabainisha vipindi ambapo wachezaji watasajiliwa, alimradi
uzingativu utawekwa kwa kuaminika kwa mashindano yanayohusika.
KANUNI YA 41
PASI YA
WACHEZAJI
Chama kinachosajili kinawajibika kukipa Kilabu alikosajiliwa
mchezaji pasi yenye taarifa za mchezaji husika, pasi ya Mchezaji itaonyesha
kilabu alikosajiliwa tangu msimu wake wa miezi 12 ya kwanza. Iwapo mwisho wa miezi 12 unaishia kati kati
ya Msimu, mchezaji ataorodhesha katika pasi ya mchezaji kwa klabu aliyokuwa
amesajiliwa katika Msimu uliomalizika katika miezi yake 12.
KANUNI YA 42
MAOMBI YA USAJILI
Maombi ya Usajili wa Mchezaji wa Kulipwa lazima yawasilishwe pamoja na fomu
ya usajili ya mchezaji, nakala ya mkataba wa mchezaji, cheti cha utimamu wa
afya, cheti cha kuzaliwa, historia ya uchezaji wake wa mpira wa miguu baada ya
kutimiza miaka kumi na mbili (12) (player’s passport). Ni ridhaa ya chombo cha
uamuzi kinachohusika kuzingatia marekebisho au nyongeza yoyote ya mikataba
ambayo hayakuwasilishwa ipasavyo kwa chombo hicho.
KANUNI YA 43
HATI YA UHAMISHO YA
KIMATAIFA
1.
Maombi ya ITC
kwa wachezaji wa kigeni wa kulipwa yata wasilishwa kupitia mtandao wa kompyuta
kwa kutumia programu ya “Transfer Matching System” (TMS) baada ya vilabu
vinavyo husika na mchezaji huyo/hao kukubaliana nje ya mtandao.
2.
Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wasio wa
kulipwa yatawasilishwa kwa barua TFF baada ya vilabu vinavyo husika na
mchezaji/wachezaji huyo/hao kukubaliana. Chama cha soka kinachotoa ITC kwa njia
hii kitapeleka nakala FIFA.
3.
ITC haihitajiki kwa mchezaji mwenye umri wa
chini ya miaka12
KANUNI YA 44
KUAZIMWA KWA
MKOPO WACHEZAJI WA KULIPWA
1. Mchezaji wa kulipwa anaweza kuazimwa kwa
mkopo kwa kilabu nyingine kwa msingi wa makubaliano ya maandishi kati yake na
klabu zinazohusika. Uazimwaji huo kwa
mkopo utafuata sheria zilezile zinazotumika katika uhamisho wa wachezaji,
yakiwemo masharti ya fidia ya mafunzo na utaratibu wa mshikamano.
2 Kufuatana
na Ibara ya 5, aya ya 3, ya kanuni za FIFA kipindi cha chini cha kuazima kwa
mkopo mchezaji kitakuwa muda kati ya Vipindi Viwili vya Usajili.
3. Kilabu itakayompokea mchezaji kwa msingi wa kuazimwa kwa mkopo
haina haki ya kumhamishia katika klabu nyingine bila ya idhini ya maandishi ya
kilabu iliyomwachia mchezaji kwa mkopo na ya mchezaji anayehusika.
4. Mchezaji anayeazimwa kwa mkopo hatoruhusiwa
kwenda zaidi ya daraja la kwanza.
5.
Kilabu haitoruhusiwa kutoa au kupokea wachezaji zaidi ya watano (5) wa
mkopo katika msimu mmoja.
KANUNI YA 45
WACHEZAJI
WASIOSAJILIWA
Iwapo mchezaji asiyesajiliwa na Chama cha Soka
anacheza mechi rasmi yoyote ya Kilabu, mchezaji huyo atahesabiwa kucheza
kinyume cha sheria. Bila ya kuathiri
hatua yoyote inayotakiwa kurekebisha athari inayosabishwa na kucheza huko,
vikwazo vinaweza kuwekwa kwa mchezaji na/au kilabu. Haki ya kuweka vikwazo hivyo kimsingi iko
mikononi mwa Chama cha Soka husika au mtayarishaji wa Mashindano yanayohusika.
KANUNI YA 46
MASHARTI MAALUMU
YANAYOHUSU MIKATABA KATI YA
WACHEZAJI WA
KULIPWA NA KLABU
1. Iwapo wakala anahusika katika mapatano ya mkataba, naye
atatajwa katika Mkataba.
2. Muda wa chini wa Mkataba utakuwa kuanzia tarehe ya kuanza
kutumika hadi mwisho wa msimu, wakati ambapo muda wa juu wa Mkataba utakuwa
miaka mitano. Mikataba ya muda mwingine
wowote itakubaliwa tu kama inalingana na Sheria za nchini. Wachezaji chini ya umri wa miaka 18
haruhusiwi kuingia mkataba wa mchezaji wa kulipwa kwa kipindi kinachozidi miaka
mitatu, sharti lolote linalotaja kipindi kirefu zaidi halitatambuliwa.
3. Kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa
haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya
makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa.
Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na klabu nyingine
iwapo mkataba wake na Kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi
sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili
utastahili vikwazo vinavyofaa.
4.
Uhalali wa
Mkataba hautahesabiwa mpaka kuwe na matokeo mazuri ya upimaji afya na kutolewa
kwa kibali cha kufanya kazi.
5.
Iwapo mchezaji
wa Kulipwa ataingia katika mkataba zaidi ya mmoja unaohusu kipindi kimoja
masharti yaliyowekwa katika Sura ya IV ya kanuni za FIFA yatatumika.
KANUNI YA 47
USAJILI NA UHAMISHO WA WACHEZAJI
1. ‘Electronic
system’ ya usajili wa wachezaji kwa kutumia Licence+ itatolewa na TFF kabla ya
kipindi cha kwanza cha usajili.
2. Kutakuwa na
leseni ya usajili wa mchezaji yenye nembo ya TFF na ‘Win Africa With Africa’ na
namba maalum itakayotolewa na TFF, ambayo itakuwa na taarifa zote muhimu za
mchezaji husika. (kanuni 38)
3. Kila mchezaji ataonyesha leseni hiyo wakati
wa mchezo.
4. Mchezaji
ana uhuru wa kujisajili na Kilabu kingine katika msimu mmoja iwapo kutakuwa na
maelewano kati ya klabu chake na kile kinachotaka kumsajili.
5. Kilabu kinawajibika kuingia mkataba na
mchezaji wa kuichezea lakini mkataba huo ni lazima uthibitishwe na TFF. Ada ya
kuthibitisha mkataba ni Sh. 50,000/=.
6. Mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi
ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na klabu kingine kabla ya klabu yake
mpya kuafikiana na klabu yake ya zamani. (kanuni na 44 (3)).
7. Mchezaji
anawajibika kusaini Mkataba na Kilabu ili aweze kuidhinishwa na TFF kuchezea
kilabu yake, jina lake litaorodheshwa kwenye Fomu ya Majina (Kanuni ya 40).
KANUNI YA 48
UTHIBITISHO WA USAJILI
TFF itadhibitisha usajili wa timu zote
mbili wakubwa na watoto kwa wakati mmoja, kilabu zinatakiwa kukamilisha na
kuwasilisha kwa pamoja usajili wa timu zote mbili pamoja na majina na mikataba ya
makocha wa timu za wakubwa na vijana katika kipindi cha usajili.
Mchezaji yeyote hataruhusiwa kuchezea
kilabu chochote katika michezo ya Ligi hadi usajili wake umethibitishwa na TFF,
TFF itatoa siku 14 kuwasilisha malalamiko au pingamizi kimaandishi juu ya
usajili tangu kutangazwa majina ya wachezaji wanaombwa kusajiliwa na klabu
husika, baada ya hapo uthibitisho utakaotolewa na TFF ndiyo utakuwa wa mwisho.
TFF haitapokea rufaa yeyote inayohusu usajili kwa mchezaji ambaye hakuwekewa
pingamizi mwanzoni isipokuwa iwapo klabu imefanya udanganyifu wa jina la
mchezaji.
KANUNI YA 49
MAJINA YA WACHEZAJI
Mchezaji
atalazimika kujaza majina yake kamili matatu katika fomu ya usajili
KANUNI YA 50
IDADI YA WACHEZAJI
Kila Kilabu
kitaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi thelathini (30) na wasiopungua kumi
na wanane (18).
KANUNI YA 51
KLABU / WACHEZAJI WANAOSITISHA AU KUMALIZA MIKATABA
Kila Kilabu
kitalazimika kuwasilisha TFF kwa maandishi, majina ya wachezaji watakaositisha
mikataba yao/kuwa huru katika usajili wa msimu wa Ligi/dirisha dogo unaofuata
katika muda wa Uhamisho utakaotangazwa na TFF na kitalazimika kumpa taarifa ya
maandishi mchezaji/wachezaji husika.
KANUNI YA 52
WACHEZAJI WALIOPANDISHWA
1. Kila Kilabu
kitaruhusiwa kusajili wachezaji wa timu yake ya pili (B) ambao walithibitishwa
na TFF katika msimu uliopita.
2. Mchezaji
yeyote wa timu ya pili ambaye hakusajiliwa na kuthibitishwa na TFF katika msimu
uliopita hataruhusiwa kusajiliwa katika timu ya kwanza (A) kama mchezaji
aliyepandishwa au huru.
KANUNI YA 53
WACHEZAJI HURU
1. Mchezaji
yeyote ambaye hakusajiliwa na klabu yoyote ya Daraja lolote katika msimu
uliopita atakua huru, hahitaji uhamisho bali atalipiwa ada ya usajili TFF.
2. Mchezaji
yeyote ambaye kilabu yake imesitisha mkataba wake/au mkataba wake umemalizika,
atakua mchezaji huru na hivyo hatalipiwa ada ya uhamisho isipokuwa ada ya
usajili TFF.
Mchezaji aliyerudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba
wake nje anatakiwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa Kimataifa na hatokuwa
huru hadi atakapokamilisha uhamisho.
KANUNI YA 54
WACHEZAJI WA
KUHAMISHWA
Mchezaji yoyote ambae hajamaliza Mkataba au Mkataba wake haujasitishwa na
Kilabu yake, atakapojisajili na Kilabu kingine ni lazima ahamishwe kuanzia
ngazi ya Kilabu, Wilaya, Mkoa na TFF.
KANUNI YA 55
WACHEZAJI KUTOKA
NJE YA NCHI
Kilabu kinaruhusiwa kusajili wachezaji (wakigeni) wa ngazi ya kimataifa
(wachezaji wa timu za taifa/Ligi Kuu) kutoka nje ya nchi wasiozidi wa tano (5).
Wachezaji kutoka Ulaya na Marekani ya kusini wanaweza kuwa wa daraja la pili na
kuendelea. Kilabu hicho kinaruhusiwa kuchezesha wachezaji wasiozidi watano (5)
wa kigeni katika mchezo mmoja(walioorodheshwa). Wachezaji hao watasajiliwa
baada ya TFF kuhakikisha usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa kimataifa.
KANUNI YA 56
NGAZI ZA
UTHIBITISHO WA USAJILI
Kamati sheria, maadili na hadhi za wachezaji itathibitisha usajili wa wachezaji
wote wa wakubwa na vijana wa kilabu za ligi kuu.
KANUNI YA 57
KUTENGUA
UTHIBITISHO WA USAJILI
Uthibitisho wa usajili wa wachezaji wa klabu za ligi kuu unaweza
kutenguliwa na Kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji endapo
itathibitika kuwa usajili huo umekiuka masharti ya Kanuni hizi.
KANUNI YA 58
KATAZO
Haitaruhusiwa kwa mchezaji yeyote kutia saini mikataba ya vilabu zaidi ya
kimoja kwa wakati mmoja. Mchezaji atakayesaini mikataba ya timu mbili tofauti
kwa wakati mmoja, ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 44 (5).
KANUNI YA 59
UHAMISHO WA
MCHEZAJI
Bila ya kuathiri kanuni za uhamisho na usajili wa wachezaji:-
1. Kilabu
kinaweza kumhamisha mchezaji kutoka kilabu kimoja hadi kingine, kwa madhumuni
ya kumsajili, baada ya ligi kumalizika na/au katika kipindi cha usajili wa
katikati ya msimu. Kilabu kinachotaka
kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu
kingine, kitalazimika kuafikiana na kilabu chake kabla ya kumsajili mchezaji
huyo. Hata hivyo kilabu ambacho kitaruhusiwa kusajili mchezaji katikati ya
msimu ni kile tu ambacho hakijatimiza wachezaji 30 au kile ambacho kimempa
mchezaji wake ITC ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, au kile ambacho mchezaji
wake amehamia kilabu kingine cha ndani kwa mujibu wa Kanuni hii.
2. Endapo
kiongozi wa Kilabu anachohama mchezaji amekataa au amekwepa kuidhinisha
uhamisho wa mchezaji wa madaraja ya chini (ambaye hawajibiki kuwa na mkataba
hivi sasa) ambaye anayetaka kukihama kilabu chake baada ya msimu wa Ligi
kwisha; Katibu wa Chama cha Mpira ngazi ya Wilaya husika ataidhinisha uhamisho
huo baada ya mchezaji aliyeomba kuhama kumthibitishia kwa maandishi kuwa amehamia
Kilabu hicho kipya lakini Katibu wa Kilabu chake cha zamani hataki au anakwepa
kuidhinisha uhamisho wake.
3. Nakala
za barua ya uthibitisho wa mchezaji wa daraja la chini (ambaye hawajibiki kuwa
na mkataba hivi sasa) kwenda kwa Katibu wa Chama cha mpira ngazi ya Wilaya husika ni lazima zitumwe pia kwa
Katibu wa Chama cha mpira cha Mkoa husika na kwa Katibu Mkuu wa TFF.
4. Pamoja
na kupokea nakala ya barua ya uthibitisho kwa mujibu wa Aya ya (3) ya Kanuni
hii, TFF inaweza kumwita mchezaji huyo
na kumhoji kuhusiana na uthibitisho alioutoa kwa Vyama vya mpira vya wilaya na
mkoa na uamuzi wa TFF utakuwa wa mwisho.
5. Ada
za uhamisho wa mchezaji mmoja kutoka Kilabu kimoja hadi kingine kwa madaraja
mbalimbali na mgawanyo wake kwa mamlaka zinazohusika zitakuwa kama
inavyoonekana kwenye jedwali la kwanza lililopo kwenye viambatanisho vya Kanuni
hizi. Ada hizi ni kima cha chini cha ada za uhamisho wa wachezaji kutoka klabu
moja kwenda nyingine lakini klabu yenye mkataba na mchezaji ina haki ya kudai
malipo zaidi kwa ajili ya uhamisho toka kwa klabu kinachomtaka mchezaji wake.
Ada za uhamisho kwa mamlaka zingine hata kwa wachezaji wenye mikataba zitabaki
kama zilivyo.
KANUNI YA 60
UHAMISHO KWENDA
TANZANIA ZANZIBAR
Pamoja na kufuata utaratibu mzima wa uhamisho wa mchezaji kama
ulivyoainishwa katika Kanuni ya 56, ada za uhamisho wa wachezaji wa Tanzania
Bara kwenda Tanzania Visiwani itakuwa ni itakuwa ni kwa mujibu wa makubaliano
baina ya timu zinazohusika kulingana na masharti yaliyomo ndani ya mkataba wa mchezaji
husika na kilabu chake.
SURA YA 11
ADHABU ZINAZOHUSIANA
NA USAJILI NA UHAMISHO
KANUNI YA 61
ADHABU ZINAZOHUSU
USAJILI NA UHAMISHO
1. Mchezaji
yeyote atakayebadili jina lake halisi kwa madhumuni ya kudanganya ili asajiliwe
kinyume cha masharti ya Kanuni hizi atafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya
nchi kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili kuanzia tarehe ya
kubainika.
2. Kilabu
iliyomchezesha mchezaji aliyebadili jina kwa nia ya kudanganya kitalipa faini
ya TShs 1,000,000/= kwa kila mchezo ambao mchezaji huyo alicheza lakini matokeo
ya uwanjani hayatobadilika.
3. Kilabu
kitakachothibitika kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa na klabu hiyo
kitapoteza michezo husika, kitalipa faini ya shilingi milioni moja
(1,000,000/=) na mchezaji husika atafungiwa kwa kwa kipindi kisichopunguwa
miezi kumi na miwili (12) bila ya kujali kukatwa au kutokatwa rufaa.
4. Leseni
ya usajili ya mchezaji iliyochafuka, kufutwafutwa au kunjwa kiasi cha kupoteza
uhalisia wake na kuleta mashaka hakitakubaliwa.
5. Kilabu
chochote kitakachowasilisha Usajili wake baada ya tarehe itakayotangazwa na TFF
hautapokelewa na kitahesabika kuwa kimejiondoa chenyewe kwenye Ligi na
kitashuka daraja.
6. Kiongozi
yeyote wa TFF atakayeweka saini inayotofautiana na saini yake halisi kwenye fomu/mkataba
ya/wa usajili kwa madhumuni yoyote yale, atafungiwa kuongoza mchezo wa mpira
kwa kipindi cha miaka mitano.
7. Kiongozi
yeyote wa FA au Kilabu atakayetoa taarifa za zisizo sahihi na kupotosha Kamati
ya Utendaji ya FA ngazi husika katika maamuzi yake, kuhusiana na usajili,
atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
8. Kiongozi
yeyote wa TFF au Kilabu atakayekataa au atakayekwepa bila sababu ya msingi,
kusaini fomu/mkataba ya/wa Usajili kwa madhumuni ya uhamisho atakabiliwa na
adhabu ya kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
KANUNI YA 62
UHAMISHO NJE YA
NCHI
1. Mchezaji
yeyote anaruhusiwa kuhamia Kilabu kingine nje ya Nchi baada ya kupata kibali
cha Kimataifa (ITC).
2. Kabla
TFF haijatoa kibali, mchezaji
analazimika kupata idhini ya Kilabu chake cha hapa Nchini.
3. Maombi
ya kibali cha TFF na idhini yeyote itakayotolewa na Kilabu ni lazima vifanywe
kwa maandishi.
4. Kilabu
kinachotaka kumhamisha mchezaji na kilabu kinachohusika na mchezaji huyo vitakubaliana
kuhusu gharama za uhamisho.
5. Endapo
itatokea kutokubaliana kati ya pande hizo mbili kutokana na sababu yoyote ile
TFF itaingilia kati na kutoa uamuzi kwa kuzingatia sheria na kanuni za TFF, CAF
na FIFA.
6. TFF
itatambua kumalizika au kuvunjika kwa mkataba wa mchezaji na klabu yake ya nje
baada ya kupata ITC kutoka kwa Chama cha Soka cha Nchi alipokuwa akicheza.
7. Barua
ya uthibitisho kutoka kwa Chama cha Soka cha nje ni lazima iwe na Nembo ya
Chama husika, jina kamili, cheo na saini ya afisa mhusika katika Chama hicho.
Uhamisho wa
kimataifa unaombwa na kutolewa kwa chama cha
cha mpira cha kitaifa pekee kwa niaba ya kilabu, na si kwa mchezaji au
kiongozi wa kilabu.
SURA YA 12
MENGINEYO
KANUNI YA 63
MWALIMU WA TIMU
1. Kila Kilabu
kinapaswa kuajiri mwalimu wa timu mwenye ujuzi wa kutosha na anayetambuliwa na
TAFCA, na mkataba wake kusajiliwa TFF.
2. Mwalimu wa
klabu ya Ligi kuu anatakiwa awe na Stashahada au cheti cha ngazi pevu ya
ufundishaji.
3. Mwalimu
toka nje atathibitishwa kwanza na TFF kabla ya kuingia mkataba na kilabu na
kupewa kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini.
4. Mwalimu
atatakiwa kuwa na Leseni ya Daraja la A toka TFF kuweza kufundisha kilabu cha
ligi kuu.
5. Mwalimu wa
timu ndiye mkuu wa shughuli zote za timu kuanzia usajili wa wachezaji, uandaaji
wa timu, usimamiaji katika mashindano na kadhalika.
6. Kilabu
ambacho kitasitisha mkataba wa mwalimu wake wakati ligi inaendelea, kitatozwa
faini ya T.sh 500,000/= kwa kila mchezo kitakachocheza bila mwalimu mwenye sifa
kwa mujibu kanuni 61 (2) ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Baada ya mwezi mmoja
klabu hiyo itapoteza sifa ya kuendelea na michezo ya ligi kuu.
KANUNI YA 64
DAKTARI WA TIMU
Kila Kilabu kinapaswa kuajiri daktari wa timu mwenye
ujuzi wa kutosha na anayetambuliwa na TASMA na kuthibitishwa na TFF.
KANUNI YA 65
TIMU ZA PILI NA
WATOTO
1.
Kila Kilabu
kinatakiwa kusajili na kudumisha timu za pili au za watoto,kuzichezesha katika
michezo ya utangulizi timu ikicheza nyumbani na kushiriki katika mashindano ya
vijana yanayoandaliwa na TFF, ikiwa ni sharti la kushiriki Ligi na kwa manufaa
ya kilabu na kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu kwa ujumla. Endapo Kilabu itashindwa kutimiza sharti hili
atakabiliwa na adhabu zifuatazo;
i.
Faini ya shilingi
laki tano itatozwa kwa klabu husika.
ii.
Ikikosa michezo
mitatu mfululizo ya Ligi klabu husika itashushwa daraja.
iii.
Kila Kilabu
kitaruhusiwa kusajili wachezaji wa timu za watoto/vijana wasiyopungua 18 na
wasiyozidi 22 wenye umri usiyozidi miaka 20.
iv.
Kilabu zinatakiwa
ziwe zimekamilisha usajili wa timu za watoto katika kipindi cha usajili.
v.
Wachezaji watano tu
katika orodha ya wachezaji kumi na nane wa timu za vijana ndiyo watakao
ruhusiwa kutumika katika mchezo mmoja Ligi Kuu.
vi.
Usajili na uhamisho
wa timu za watoto utazingatia kanuni za Ligi Kuu.
vii.
Waraka maalumu
utatolewa kuhusiana na usajili wa wachezaji wa timu za watoto ambao utasomeka
pamoja na kanuni hizi.
KANUNI YA 66
ADHABU ZISIZOKATIWA
RUFAA
1.
Adhabu zote kwa
mujibu wa kanuni zifuatazo za ligi kuu hazitakatiwa rufaa katka ngazi yeyote ya
mashindano. Kanuni hizo ni;
(a) KANUNI: 8 (Utaratibu wa mchezo)
(b) KANUNI: 25 (Udhibiti wa wachezaji) isipokuwa 25. (g) na
(h).
(c) KANUNI: 26 (Udhibiti wa waamuzi) isipokuwa 26. (c)na (e).
(d) KANUNI: 27 (Udhibiti wa makamishina) isipokuwa 27. (c) na
(e).
(e) KANUNI: 28 (Udhibiti wa watathimini wa waamuzi) isipokuwa
28. (c) na (e).
(f) KANUNI: 29 (Udhibiti wa waalimu) isipokuwa 29.
(c),(e),(f) na (g)
(g) KANUNI: 30 (Udhibiti wa viongozi) isipokuwa 30.
(a),(d),(f),(g),(h),(i),(k) na (l).
(h) KANUNI: 31 (Adhabu kwa Vilabu).
KANUNI YA 67
UDHAMINI
TFF itajitahidi kutafuta mdhamini/wadhamini wa Ligi Kuu, kila Kilabu
kitalazimika kuheshimu na kuzingatia kikamilifu masharti yote yanayotakiwa
kutekelezwa na Kilabu chenyewe, timu yake, wachezaji wake au Viongozi
wake. Yaliyomo ndani ya Mkataba
/Mikataba hiyo kama itakavyoelezwa na TFF. Timu itakayoshindwa kutekeleza
masharti haya kama itakavyoelezwa na TFF itatozwa faini isiyopungua Tshs.
1,500,000/= na pia inaweza kuchukuliwa hatua nyingine ikiwemo kuondolewa kwenye
mashindano na /au kufungiwa.
KANUNI YA 68
LESENI YA KUSHIRIKI
LIGI KUU.
Vilabu vya ligi kuu vinatakiwa kuwasilisha maombi ya kupatiwa leseni TFF
katika muda utakao tangazwa na Kamati ya Utendaji ya TFF.
1.
Ilikupewa leseni
muombaji anatakiwa awe nasifa zifuatazo;
a.
Katiba ya klabu
iliyosajiliwa,
b.
Watendaji wa klabu,
c.
Ofisi isiyo
hamishika,
d.
Mpango wa
maendeleao wa soka la vijana,
e.
Mwalimkuu wa timu
aliye na shahada ya daraja B ya CAF
f.
Ripoti ya ukaguzi
wa mahesabu ya klabu yake
g.
Uwanja wake wa
mazoezi
2.
Kamati ya Sheria,
maadili na Hadhi za wachezaji ya TFF ndiyo itakayo toa leseni ya kushiriki ligi
kuu.
3.
Iwapo klabu
haikuridhika na maamuzi ya kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji,
klabu inatakiwa kuwasilisha rufaa yake ya kupinga maamuzi hayo kwenye kamati ya
rufaa ya TFF katika kipindi kisichozidi siku tatu (3) za kazi baada ya kupokea
uamuzi wa kamati ya sheria, maadili an hadhi za wachezaji.
4.
Ada ya kukataa
rufaa ni shilingi milioni moja, Tsh. 1,000,000/=
5.
Maamuzi ya kamati
ya rufaa juu ya suala la kutoa leseni kwa vilabu vinavyo shiriki ligi kuu ni ya
mwisho.
KANUNI YA 69
UTUMIAJI WA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU
Mchezaji yoyote atakayetakiwa kufanya
vipimo vya dawa za kulevya au kuongeza nguvu, anawajibika kufanya hivyo, endapo
atagundulika/atakataa kuwa anatumia madawa ya kulevya au kuongeza nguvu/kufanya
hivyo atafungiwa kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12).
KANUNI YA 70
UFAFANUZI
Kwa minajili ya kufafanua Kanuni hizi TFF itakuwa inatoa WARAKA kila
inapoonekana inafaaa kufanya hivyo kwa lengo la kuleta ufanisi katika
utekelezaji wa Kanuni hizi.
KANUNI YA 71
TAFSIRI
Kikao cha juu kuliko vyote kwa ajili ya tafsiri ya Kanuni hizi kitakuwa
kamati ya utendaji ya TFF na uamuzi wake utakuwa wa mwisho
KANUNI YA 72
MAREKEBISHO YA
KANUNI
Kamati ya utendaji ya TFF inaweza kurekebisha Kanuni hizi kila inapotokea
haja na sababu za kufanya hivyo.
KANUNI YA 73
KUFUTA KANUNI
Kanuni hizi zinaweza kufutwa na Kamati ya Utendaji ya TFF pekee.
KANUNI YA 74
MAMBO YASIYOMO
KWENYE KANUNI HIZI
Mambo yote yasiyokuwemo kwenye Kanuni hizi yataamuliwa na Kamati ya
Utendaji ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za FIFA na CAF.
Kanuni hizi zimepitishwa kwa Azimio la Kamati ya Utendaji ya TFF
iliyokutana tarehe 20 Julai 2009.
______________________ ___________________
L. C. Tenga A.
Oseah
RAIS KATIBU
MKUU
____________________
TAREHE
NYONGEZA
JEDWALI LA KWANZA
(KANUNI YA 18 (5) A
FOMU YA MGAWANYO WA
MAPATO
KANUNI YA 18 (1),
(2), (3), (4) NA (5)
KIASI
|
JINA
|
SAHIHI
|
|
Toa VAT 18% ya makusanyo
|
|||
Toa: Posho ya kujikimu, kwa waamuzi na kamisaa 70,000/=x5
|
|||
Usafiri wa ndani kwa waamuzi wote shs. 20,000/= na kwa
kamisaa shs. 20,000/=.
|
|||
Posho ya mchezo kwa waamuzi wa tatu na kamisaa shs.
100,000/= kila mmoja na mwamuzi wa akiba shs. 50,000/=
|
|||
Posho ya msimamizi wa kituo shs. 100,000/=
|
|||
Gharama za tiketi
|
|||
Baki ya pato
|
|||
9% Gharama za mchezo: (Rejea fomu ya gharama za mchezo)
|
|||
(Isizidi 5,000,000/=)
|
|||
9% TFF (T)
|
|||
4.5% FDF (T)
|
|||
15% Uwanja
|
|||
3.5% FA (M)
|
|||
29.5% klabu ngeni
|
|||
29.5% Klabu mwenyeji
|
|||
JUMLA
|
JEDWALI LA PILI
(KANUNI YA 18 (B))
FOMU YA MGAWANYO WA
GHARAMA ZA MCHEZO LIGI KUU YA VODACOM
KANUNI YA 19 (1),
(2) NA (3)
KIASI
|
JINA
|
SAHIHI
|
|
Gharama za
msimamizi wa kituo
|
|||
(i)
Msimamizi mkazi
atalipwa posho 100,000/= na nauli ya
ndani 20,000/=
|
|||
(ii) Msimamizi kutoka nje ya kituo atalipwa
posho shs.
100,000/=, nauli ya ndani 20,000/=
gharama za kula na
kulala shs. 70,000/= na nauli kutoka
kituo chake na
kurudi
|
|||
(iii)
Malipo ya ulinzi, ball boys, huduma ya kwanza, vinywaji,
wasimamizi, wauzaji na wachanaji
tiketi.
|
|||
(vi) Baki
ya pato iwapo gharama za mchezo ni pungufu 9%
|
|||
Klabu
ngeni 25%
|
|||
Klabu
mwenyeji 25%
|
|||
TFF 50%
|
|||
JUMLA
|
ADA ZA USAJILI NA
UHAMISHO WA WACHEZAJI
Ada za Uhamisho za Wachezaji Kutoka Daraja Lolote Kwenda Ligi Kuu Itakuwa
Kama Ifuatavyo;
KLABU
|
TFF
|
FA (M)
|
FA (W)
|
JUMLA
|
55,000.00
|
25,000.00
|
20,000.00
|
||
MGAWANYO WA ADA ZA
USAJILI NA UHAMISHO WA WACHEZAJI KUTOKA TANZANIA BARA KWENDA VISIWANI.
KLABU
|
TFF
|
FA (M)
|
FA (W)
|
JUMLA
|
300,000.00
|
120,000.00
|
80,000.00
|
||
No comments:
Post a Comment