KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 10, 2014

Rockersports video: Maradona amchapa mwandishi wa habari kofi akiwa katika mahojiano nchini Argentina


Diego Maradona huenda akaingia matatizoni kufuatia mshambuliaji huyo wa zamani wa Argentina kumchapa kibao mwandishi wa habari katika mahojiano.

Maradona mwenye umri wa miaka 53 alikuwa akiuulizwa maswali na waandishi mbalimbali wakati akiondoka kwenye ukumbi mmoja wa maonyesho nyumbani kwao Argentina akiwa na mama watoto wake Veronica Ojeda pamoja na mtoto wao wa kiume Diego Fernando Jumamosi.

Taarifa zinasema kuwa maradona alikasirishwa na kitendo cha mwandishi mmoja kumfinyia macho (kumkonyeza)mama watoto wake Ojeda, ndipo alipotoka nje ya gari yake na kumchapa kofi.

Nahodha huyo wa zamani wa Argentina aliyeipa mafanikio mwaka 1986 katika kombe la dunia alimuuliza mwandishi huyo.

‘Kwanini unafanya hivyo kwa mke wangu wakati mimi sijakufanyia lolote baya?’

Tukio hilo limechukua vichwa vya habari katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Argentina na video yake kuonyeshwa mitandaoni.

NB: Nadhani baada ya Video hii kuonekana ni wazi kuwa waandishi wa nchini Argentina hawata mdhihaki tena Maradona.