Bingwa wa Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya
dunia katika mbio za mita mia moja kwa wanaume Usain Bolt wa Jamaica,
anatarajiwa kurejea tena uwanja baada ya kuuguza jeraha la mguu, siku ya
Alhamisi wakati wa mashindano ya mbio za IAAF Diamond League mjini Rome
Italia.
Bolt
alipata jeraha hilo la mguu mwezi uliopita na anatarajiwa kushiriki
katika mbio za mita mia moja ambapo atapamabana na mshindi wa medali ya
shaba katika michezo ya Olimpiki Justin Gatlin.
Mwanariadha wa Uingereza Phillips Idowu ambaye
alikosa kushiriki katika michezo ya olimpiki ya London kutokana na
jeraha vile vile anarejea tena uwanjani kwa mara nyingine tena.
Idowu atapamba na bingwa wa olimpiki Christian Taylor katika mbio hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali..
Mwaka huu Bolt ameshiriki katika shindano moja
pekee la mita mia moja mwezi Mei ambapo alishinda kwa ncha baada ya
mshindi kuamuliwa kupitia camera za video, baada ya wanariadha wa kwanza
kuonekana kumaliza kwa wakati mmoja na muda sawa wa sekunde kumi nukta
sufuri
No comments:
Post a Comment