KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 19, 2014

USAJILI: OFA MBILI ZA UKWELI KWA ASHLEY COLE HIZI HAPA

Ashley Cole baada ya kuachwa na Mourinho Chelsea anategemea kujiunga na Barcelona au AC Milan
Imefahamika kuwa mlinzi wa kushoto wa zamani wa England Ashley Cole yupo kati mipango ya ama kujiunga na Barcelona AC Milan.
Cole, ambaye amekuwa huru baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu amepata ofa ya vilabu hicyo viwili.
Barcelona wako katika mpango wa kusaka mlinzi wa kushoto ambapo wamekuwa wakimtegemea mlinzi raia wa Brazil Adriano pekee mpaka kumalizika kwa msimu uliopita.
 Imeendelea kuwa katika matatizo ya nafasi hiyo tangu kuondoka kwa Eric Abidal aliye uzwa katika klabu ya Monaco kiangazi iliyopita ambapo sasa meneja mpya wa klabu hiyo Luis Enrique amekuwa akimuwinda Cole.
Milan pia wamekuwa katika shida wakisaka mchezaji mpya wa nafasi hiyo hususani baada ya kuwasili kwa meneja mpya Filippo Inzaghi ambaye amechukua nafasi ya Clarence Seedorf kama kocha mpya.
Wengi ndani ya Chelsea wanaamini kuwa Cole, ni mlinzi bora wa kushoto wa muda wote hakupewa heshima iliyostahili kutoka kwa Jose Mourinho msimu uliopita.

Offers: At the age off 33, the former England defender believes he has plenty to offer
Akiwa umri wa miaka 33, Cole anaamini ana mengi ya kutoa kama mchango wake katika soka

Licha ya kupewa nafasi katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya hususani mchezo dhidi ya Atletico Madrid kule Vicente Calderon, bado alishindwa kumshawisho Mourinho kuendelea naye.
 Akiwa na umri wa miaka 33 Cole anaamini bado ana mengi ya kutoa kama mchango wake na amekuwa katika matarajio ya kusalia katika Barclays Premier League.
Alistaafu katika timu ya taifa ya England kufuatia kocha wa England kupendelea kumtumia  zaidi Leighton Baines na beki wa kushoto wa Southampton  Luke Shaw katika kombe la dunia.