Manchester City yapangwa dhidi ya Barcelona hatua ya mtoano ya 16
- Arsenal kukutana dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich
- Shujaa wa zamani wa Chelsea Didier Drogba anarejea kukutana uso kwa macho na Chelsea akiwa na klabu yake ya Galatasaray
- Manchester United yakutanishwa dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki
Kuelekea katika hatua ya mtoano ya vilabu bingwa barani Ulaya, Vihoro, wasiwasi na woga mkubwa umevikumba vilabu vikubwa vya England Manchester City na Arsenal ambavyo vimejikutaa katika ratiba ya mtoano wakikabiliana na vigogo vya Ulaya Barcelona na mabingwa watetezi wa taji hilo Bayern Munich.
Manchester City wako kwenye ratiba ya kukutana na kigogo cha Hispania Barcelona ilhali vinara wa ligi kuu ya England Arsenal wakikabiliana na Bayern Munich.
Kwa mtazamo wa ratiba hiyo ilivyo pangwa wakati Chelsea wakijikuta katika ratiba ya kukutana dhidi ya Galatasaray ni wazi kuwa mchezo huo unamrudisha mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba anarejea kukutana dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea.
Wapinzani wao wakubwa Manchester United wako katika ratiba ambayo kimsingi inaonekana kama rahisi kwa upande wa vilabu vya Engalnd wakipambana dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki.
Droo kwa ujumla wake.
Manchester City v Barcelona:
Ni droo ambayo katika hali ya kawaida ni kwamba Manchester City hawakuwa wakiitaka katika hatua kama hii ambapo Begiristain na Soriano wakati huu wakiwa City. Mchezo mkubwa ' fantastic tie'. Hili ni jaribio kubwa kwa City na maendeleo yao. Michezo yake itapigwa Feb 18 na maridiano itakuwa March 12.
Olympiacos v Manchester United:
Hii inaonekana kama ni droo nyepesi kwa kocha David Moyes, inachukuliwa ni kama United imepata mchezo wa mteremko na wana nafasi kubwa ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Mchezo wa kwanza utakuwa Feb 25, na wa marudiano utakuwa March 19.
AC Milan v Atletico Madrid:
Atletico Madrid itakuwa inakutana dhidi ya mabingwa wa mwaka vilabu bingwa ulaya wa mwaka 2007 Milan. Could be a decent tie. Feb 19, March 11.
Bayer Leverkusen v Paris St Germain:
PSG itakuwa bila shaka imefurahia droo hiii licha ya kwamba imekuwa haina utulivu. Mchezo wa kwanza utakuwa Feb 18 na marudinao March 12.
Galatasaray v Chelsea:
Mchezo huu Didier Drogba na Jose Mourinho wanaonekana kurejea katika mahaba. Sneijder atakuwa akiingia katika michezo hiyo akiwa na kumbukumbu ya kushinda mataji akiwana Inter mwaka 2010 akiwa na pia akiwa na Mourinho. Mchezo wa kwanza Februari Feb 26 na wa marudiano March 18.
Schalke v Real Madrid:
Real Madrid kwao hii ni faraja kubwa wakiiamini kutinga katika hatua itakayofuatahuku mchezo wa kwanza kwanza ukitarajiwa kupigwa Feb 26 na marudiano March 18.
Zenit St Petersburg v Borussia Dortmund:
Timu iliyofika fainali msimu uliopita Dortmund na kufungwana wapinzani wao wakubwa katika soka la Ujerumani Munich watakuwa wakitaraji kusonga mbele. Kikosi cha kocha Klopp kinaonekana kuwa vizuri katika mchezo huo. Mchezo wa kwanza Feb 25 marudiano March 19.
Bayern Munich v Arsenal:
Timu hizi ziliwahi kukutana katika hatua hiyo katika msimu uliopita na wanakutana tena mara hii. Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 Allianz Arena msimu uliopita lakini wakaharibu katika mchezo wa marudiano na kutolewa mashindanoni. Bila shaka wasingependa kuona matokeo kama hayo yanajirudia tena.
Mchezo wa kwanza utakuwa Feb 19 na marudiano ni March 11.

Mesut Ozil na wenzake wanajua kuwa watakuwa wakikabiliwa na mchezo mgumu na wa ufundi mkubwa.

Man City wanaonekana wako sawa lakini wana kazi ya kufanya kuwamaliza wapiznani wao wa hatua ya mtoano Barcelona.
Real Madrid, Paris St Germain na Borussia Dortmund watakuwa ni wenye furaha katika kinyanganyiro chao cha hatua hiyo ya mtoano dhidi ya Schalke, Bayer Leverkusen na Zenit St Petersburg.
AC Milan watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Atletico Madrid, ambao wanapigania taji la ligi nchini Hispania Seria A sambamba na vigogo Madrid na Barcelona.
Droo imefanyika mjini Nyon, na kuendeshwa na katibu mkuu wa UEFA Gianni Infantino, mkurugenzi wa mashindano wa UEFA Giorgio Marchetti na balozi wa michuano ya vilabu ya EUFA Luis Figo.

Drogba anarejea London dhidi ya bosi wake wa zamani Jose Mourinho
No comments:
Post a Comment