Vilabu viwili vilivyo wahi kuwa mabingwa wa klabu bingwa Ulaya kwa nyakati tofauti vimekutana katika mchezo maalumu wa kumuaga kiungo wa zamani wa vilabu hivyo Anderson Luís de Souza maarufu Deco mchezo ambao ulifanyika jana na kuhitimisha safari ya kiungo huyo mkubwa kabisa aliyewahi kutokea dunia katika karne 21 Deco ambaye rasmi ameachana na mchezo wa soka
Mchezo huo uliwaleta kwa pamoja nyota kama Lionel Messi, Eidur Gudjohnsen, Benni McCarthy na Paulo Ferreira, ulimalizikwa kwa pande hizo mbili ambazo Deco aliwahi kuzichezea kwa mafanikio kumalizika kwa sare ya bao 4-4, ambapo Samuel Eto'o alifunga mabao 2 Deco mwenyewe akifunga goli la 4 na la kusawazisha kwa upande wa Porto ambako alicheza kipindi cha Pili.
Deco alichezea vikosi vyote katika mchezo huo maalum ambapo aliuufanya kuwa mchezo wa kusisimua akifunga dakika ya 89 na kuufanya kuwa mpira wake wa mwisho kuugusa akiwa uwanjani kama mchezaji.
Anderson Luís de Souza Deco alizalwia Agosti 27 1977) ambapo mbali ya kuvichezea vilabu hivyo pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na amemalizia soka take katika klabu ya Fluminence.
No comments:
Post a Comment