KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 26, 2014

Michezo ya Madola Glassgow: Nasser Mafuru ashindwa kupanda uliongoni kisa tumbo la kuhara la ghafla.

Bondia Nasser Mafuru wa Tanzania amepoteza mchezo wake dhidi ya Jessie Lartey wa Ghana uzito wa kilo 60 michezo ya Jumuiya ya Madola inayofanyika huko Glassgow nchini Scotland, kufuatia kushindwa kupanda ulingoni kwa kile kilichoelezwa kuwa alipatwa na maradhi ya tumbo ghafla.

Akiongea na Rockersports kocha mzalendo wa mchezo huo John Mwakipesile amesema Mafuru amepatwa na maswahibu hayo muda mfupi kabla ya kupanda ulingoni wakati akipasha mwili joto na na ndipo akashikwa na tumbo la kuhara kabla ya taarifa kupelekwa kwa wasimamizi wa mchezo huo ambao waliumaliza mchezo huo nje ya ulingo.

Jana akizungumza na mtandao wa Rockersports, Mafuru alisema amemuona mpinzania wake kutoka Ghana Jessie Lartey na kwamba asingeweza kufua dafu kufuatia maandalizi yake mazuri.
Timu ya taifa ya Tanzania  ikiwa Scotland
Hiyo inakuwa ni karata ya pili kupotea kwa upande wa Tanzania kufuatia bondia nahodha Selemani Kidunda usiku wa jana kupigwa na mpinzania wake kutoka Nigeria Kehinde Ademuyiyiwa licha ya kuwa vizuri sana wakati wa mchezo.

Usiku huu bondia mwingine mtanzania Fabian Gaudence atapambana na Steven Thanki wa malawi uzito wa kilo 64 kabla ya Ezra Paul kucheza dhidi ya Bye kesho jioni uzito wa kilo 52 naye Mohamed Hakimu akimsubiri Sumit Sangwan wa India jioni uzito wa kilo 81.

Kesho kutwa Emilian Patrick atacheza na Bashiri Nasir wa Uganda kilo 56 naye Hamed Furahisha atababiliana na Paddy Barnes wa Ireland Kaskazini kilo 49.

No comments:

Post a Comment