Harry
Redknapp ameamua kuondoka Tottenham, baada ya kuwafundisha vijana wa Spurs kwa
muda wa miaka minne.
Redknapp ambaye
alichukuliwa kama meneja ambaye angeliweza kuifundisha vyema timu ya taifa ya Uingereza
lakini aliikosa kazi hiyo ambayo chama
cha soka cha Uingereza kiliamua kumpa nafasi Roy Hodgson.
Jumanne wiki
hii Redknapp alikanusha uvumi kwamba tayari alikuwa amejiuzulu kutoka
Tottenham.
Redknapp,
mwenye umri wa miaka 65, amesema kuwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba
wake na klabu hiyo ya White Hart Lane, na inasemekana huenda ikawa kulikuwa na
hali ya kutoelewana kuhusiana na mkataba mpya, baada ya kushauriana na
mwenyekiti wa klabu, Daniel Levy.
Meneja huyo
wa zamani wa Bournemouth, West Ham, Portsmouth na Southampton, sasa ameachana
na klabu hiyo ya mjini London.
Wakati Fabio
Capello alipoiacha kazi ya meneja wa timu ya Uingereza Februari 8 , Spurs
walikuwa katika nafasi ya tatu katika ligi kuu ya Premier.
Alikuwa ameiacha
Arsenal, ambayo ilikuwa inaonekana dhaifu wakati huo, kwa pointi kumi.
Hatimaye
waliachwa nyuma kwa pointi nne na Arsenal, na kukosa nafasi ya kufuzu kwa mechi
za klabu bingwa barani Ulaya.
Redknapp
alipoondoka Portsmouth mwaka 2008, alifanikiwa kuingoza Tottenham hadi katika
mashindano ya klabu bingwa, kwa mara ya kwanza, waliposhiriki mwaka 2010.
Baada ya
kumaliza ligi kuu katika nafasi ya nne msimu uliopita, Tottenham walishindwa
kufuzu, kufuatia Chelsea kupata ushindi katika fainali ya klabu bingwa.
Redknapp
alifikiriwa kwanza wakati meneja kutoka Italia, Fabio Capello alipojiuzulu
mwezi Februari, lakini hatimaye Hodgson ndiye aliyechaguliwa.
Inasemekana
Levy hakufurahishwa na namna Spurs walivyokamilisha msimu, na kupoteza nafasi
nzuri, baada ya kuitangulia Arsenal kwa pointi kumi, na ambayo ilimaliza katika
nafasi ya tatu.
Redknapp
mara kwa mara alikanusha hali hiyo ya kudorora kwa timu yake ni kutokana na
kuhusishwa na kibarua cha timu ya taifa.
Wiki
iliyopita, aliitaka Spurs kupata suluhu juu ya hatma yake, na kusisitiza kwamba
hali ya kutojua kitakachotokea ni jambo ambalo lingeliweza kuwaathiri wachezaji
wa Tottenham.
No comments:
Post a Comment