TIMU
ya Simba inatarajia kurejea nchini Jumatano ijayo kutoka mjini Arusha ambako
imeweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Libolo ya Angola.
Mechi
hiyo imepangwa kufanyika Jumapili ijayo (Februari 17) kuanzia saa kumi na nusu
jioni. Uongozi unafanya utaratibu wa kuiwezesha timu kufanya mazoezi katika
Uwanja wa Taifa walau mara moja kabla ya mechi hiyo ili kutoa nafasi kwa benchi
la ufundi kutoa maelekezo mahususi kwa wachezaji kuhusiana na mechi hiyo.
Kocha
na mchezaji wa zamani wa Simba, Talib Hilal, anaelekea Arusha leo ili kuongeza
nguvu ya benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi. Hii si mara ya kwanza kwa
Talib kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la Simba kwani alifanya hivyo pia
miaka kumi iliyopita wakati klabu hiyo ilipocheza na Zamalek ya Misri na
kufanikiwa kuitoa.
Talib
Hilal hajaja kuchukua nafasi ya mtu yeyote kwenye benchi la ufundi. Amekuja kwa
mapenzi yake kwa Simba na mara zote klabu inamkaribisha kwa vile uwezo wake
kitaaluma, uzoefu wake na uwezo wake katika kuhamasisha unakubalika ndani ya
klabu.
Simba SC inaomba washabiki na vyombo vya habari waisaidie klabu kwa
kutotoa taarifa zenye kuashiria migogoro isiyokuwepo. Simba wanawakilisha
heshima na hadhi ya Tanzania
katika mashindano haya.
Unachoomba
uongozi wa klabu ni uzalendo kwa taifa letu walau katika kipindi hiki ambapo
kinachoangaliwa ni utaifa wetu. Uongozi unaomba wadau wake wa vyombo vya habari
kuandika habari za kujenga umoja, mshikamano na uzalendo kwa Watanzania wote
ili hatimaye Simba ifanye vizuri.
No comments:
Post a Comment