Kuelekelea mchezo wa jumatano wa ligi ya mabingwa Ulaya kumeibuka minong'ono mjini Madrid juu ya namna ambavyo kocha Jose Mourinho atakavyo panga kikosi kitakacho ikabili Manchester United jumatano.
Madri itakuwa wenyeji wa United mchezo wa vilabu bingwa Ulaya utakaopigwa jumatano uwanja wa Bernabeu.
Bila shaka 'Special One' atajaribu kupanga kikosi cha kwanza ambacho kitapata matokeo mazuri ya uongozi wa mchezo huo wa hatua ya mtoano ya 16 bora, kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Old Trafford.
inavyoonekana ni wazi Jose Mourinho atawapanga kikosi cha kwanza Luka Modric, Michael Essien au kuungana na Diego Lopez, Alvaro Arbeloa, Sergio Ramos, Pepe, Fabio
Coentrao, Xabi Alonso, Sami Khedira, Angel di Maria, Mesut Ozil,
Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Mourinho anaonekana kumpumzisha Pepe aliye majeruhi, Ozil, Alonso, Khedira na Benzema kutokana na kuwaondoa katika kikosi cha ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya 4-1 jumamosi usiku.
Hii inamaana kuwa Michael Essien, Raul Albiol, Luka Modric, Kaka na Gonzalo Higuain watakuwemo kikosini.
Luka Modric akionekana pichani katika mchezo dhidi ya Sevilla ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 lakini huenda asiwemo katika kikosi cha jumatano dhidi ya United.
Mourinho huenda akampa nafasi Michael Essien
(kulia) kama ilivyokuwa katika mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Barcelona.
Pepe kwasasa yuko katika kipindi cha mpito cha kuendelea kupigania kuponya enka yake ambapo alifanyiwa upasuaji na akitumika kwa dakika 25 katika mchezo dhidi ya Sevilla kwa lengo la kujaribu kuona ameimarika kwa kiasi gani baada ya matibabu.
Cristiano Ronaldo, ambaye yuko katika kiwango safi baada ya kupiga 'hat-trick' jumamosi atakuwa akiongoza mashambulizi ya Real dhidi ya klabu yake ya zamani ya Man United.
No comments:
Post a Comment