KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, May 27, 2014

Taifa Stars na Flames kuumana jioni hii uwanja wa taifa

Timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) zinapambana jioni ya leo katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili.

Malawi tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi hiyo wakati Taifa Stars iliyopiga kambi yake Tukuyu mkoani Mbeya tayari nayo imewasili jijini Dar es Salaam saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Tanzania.

Itakuwa ni mechi ya mwisho ya majaribio kwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kabla ya kwenda jijini Harare kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).

Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi nayo itakuwa inacheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla ya kwenda N’djamena kuikabili Chad.