KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 26, 2014

Boxing: Uhuni wa Thomas Mashali na Mada maugo kuzipiga kavukavu adhabu yake nini?

Hii ni shida ulingo wa chini yaani kavukavu Mada na Mshali
Kwa kweli si jambo la kushanga kuona wazazi wenye nia njema kwa vijana wao kuwakataza kuingia katika mchezo wa ngumi ikiwa hali iliyojitokeza katika ukumbi wa Friens Corner Manzese litaachwa kimya kimya na kupotezewa kimya kimya bila ya hatua za kinidhamu na kimaadili za mchezo huo hazitachukuliwa.
 
Haikuniingia akilini kuona wachezaji wakubwa kama Mada Maugo na Thomas Mashali ambao wanaheshima kubwa katika masumbwi hapa nchini wakichapana nje ya ulingo na kuvuruga hali ya amani ukumbini hapo kiasi majaji kuachana na hatua muhimu ya kutangaza matokeo kwa kuhofia kuharibu hali ya usalama zaidi.
 
Neno 'Professionalisim' katika Boxing lilipoteza maana yeke kwa mabondia wote wawili kufuatia kushindwa kudhibiti hasira zao na kuvuruga utulivu ukumbini licha ya kwamba alianza kuvuruga hali ya mambo alikuwa ni Mada Maugo kwa kumpiga Mashali ngumi tatu mfululizo baada ya kupishana kauli.
 
Hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani mbaya zaidi mabondia hao walionekana wamelewa walipishana kiswahili mbele ya promota Ally Mwazoa ambaye aliahidi kuwapandisha ulingoni kabla ya mwaka kumalizika.
 
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Thomas Mashali alimgalagaza kwa point Mada Maugo
Wadau hii ni vita Muraaaaa
 NI matumaini kwa wapenda ngumi wote nchini kuona kuwa hatua za kinidhamu zinachukuliwa kwa wanamichezo hao wawili kwa kufuata sheria za mchezo huo na hata kama itaonekana inafaa basi sheria za nchi zihusike kukemea kadhia hiyo ambayo inaonekana kuharibu future ya mchezo huo na kuhatarisha uhai wa mchezo wenyewe.

Nitoe rai kwa mapromota wa mchezo huo hapa nchini kuliona hilo kuwa ni tatizo na kamwe wasitumie aina hiyo ya uchonganishi kama ni njia sahihi ya kuongeza hamasa ya mchezo huo na kuukuza wakidhani itaongeza vipato vyao pale wanapo dhamini.

Kuna viashiria vya wazi kuwa kuna viongozi na mapromota wa mchezo huo wa ngumi wameanza kubuni njia mbalimbali za kuwatenganisha wachezaji wa mchezo huo kwa kuweka uhasama baina yao ili kuongeza hisia kali kukamiana na kuimarisha chachu ya ukuajia wake jambo ambalo si sahihi.

Nawakumbusha tu kuwa huo ni mchezo kama ilivyo michezo mingine ambayo kwa ujumla wake yote ina sheria zake ambazo kimsingi zinatambuliwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani serikali ndio iliyosajili katiba za vyama na mashirikisho ya michezo kama si kamisheni za michezo hapa nchini.

Sitarajii wachezaji hao kupanda ulingoni hivi karibuni bila ya kwanza kutumikia na kumaliza adhabu za utovu wao wa nidhamu ukumbini kiasi kuharibu starehe ya wapenzi wa mchezo huo waliolipa kiingilio na kushuhudia mpambano wa Kalama Nyilawila na Saidi Mbelwa( Pichani juu) ambao nao walimaliza pambano hilo kihuni kwa kuzichapa za nje ya ulingo.

Vinginevyo tafsiri yake ni kuwa mchezo wa ngumi hapa nchini hauna sheria na ni uhuni mtupu haufai kuendelea kushibisha matumbo ya watu wasiojali usalama wa watu na mali zao ambao ndio wadau wakubwa wa mchezo wenyewe.