Mshambuliaji wa Manchester United Danny Welbeck amesema siku zote alikuwa ni mchezaji mwenye uweledi na kumshangaa aliyekuwa bosi wake David Moyes aliyekuwa akidai kuwa mshambuliaji huyo alikuwa hafanyi mazoezi ya kutosha(kwa lugha ya kisoka zaidi hakuwa Professional).
Moyes,ambaye alitimulia kibaruani na United mwezi Aprili alikaririwa akitoa maneno hayo mwezi Desemba alipomtaka Welbeck kuongeza mazoezi ya ziada.
"Kwakweli alinishangaza sana" amekariri mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England mwenye umri wa miaka 23.
"Kabla hajatoa kauli hiyo nilikuwa nikifanya mazoezi sana, pengine alikuwa hanioni"
Welbeck alifunga jumla ya magoli 11 katika jumla ya michezo 24 aliyoanza huku pia katika msimu wa 2012-13 akiifungia magoli ya kutosha England kuliko klabu yake.
Aliifungia magoli saba timu ya taifa ya England iliyo chini ya Roy Hodgson ukiwa nia wastani wa 0.43 kwa kila mchezo ukilinganisha na magoli mawili aliyofunga katika klabu yake licha ya kushuka uwanjani mara 40 chini ya bossi wa zamani wa United Sir Alex Ferguson ukiwa ni wastani wa 0.05 kwa kila mchezo).

Welbeck, ambaye alifunga jumla ya magoli 11 katika michezo 24 aliyoanza msimu uliopita kwasasa ni sehemu ya kikosi cha kocha wa England Roy Hodgson chenye jumla ya wachezaji 23 ambacho kinajiandaa kueleka kwenye fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Wayne Rooney, Robin van Persie, Javier Hernandez and na mshambuliaji aliyesajiliwa mwezi Januari kwa pauni milioni 37.1 Juan Mata wote kwa pamoja wanagombea nafasi ya kucheza katika safu ya ushambuliaji ya United.
"Nilipenda kucheza mshambuliaji wa kati lakini nilikuwa nikitokea pembeni upende wa kushoto ilikuwa ngumu kwa muda.
No comments:
Post a Comment