KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 26, 2014

Paul Ince ampeleka mwanae Tom Inter Milan

 Tom Ince ameelekea nchini Italia kwa ajili ya mazungumzo na Inter.

Winga huyo ambaye yuko huru baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Blackpool alimalizia nusu ya msimu uliopota kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace ambako alicheza michezo minane tu katika kikosi hicho cha kocha Tony Pulis.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 22 aliwasili Milan jana jioni akiwa na baba yake Paul, ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo kwa misimu miwili wakati wa uchezaji wake wa soka.

Amenukuliwa Paul Ince baba yake ya Tom akisema
"Kwangu mimi ni faraja kurejea tena Italia baada ya miaka yote hiyo na kukutana na marafiki zangu wengi  uwanja wa ndege” Alikuwa akiongea na Sky Sports.

“Nilikuwa na mahusiano maziri na Rais wa zamani wa Inter Massimo Moratti. Najivunia historia yangu nzuri ndani ya Inter naimani na mwanangu atakuwa ni sehemu ya hilo”