KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 21, 2012

DROGBA AOMBA MUONGOZO WA FIFA JUU YA KUONDOKA SHANGHAI SHENHUA KWA MUDA.



Drogba ataka ruhusa ya FIFA permission kuhama kwa mkopo
Mshambuliaji wa Shanghai Shenhua Didier Drogba ameomba muongozo wa shirikisho la soka duniani FIFA juu ya uwezekano wa kuhama nje ya dirisha la kawaida la mwezi wa Januari akiwa na lengo kupata muda zaidi wa maandalizi ya michuano mikubwa ya mataifa ya Afrika.

Msimu wa ligi wa nchini China ulimazika mapema mwezi huu ambapo kwasasa Drogba anafikiria kupata uhamisho wa muda toka katika klabu yake ya Shenhua kwa lengo la kuimarisha na kutunza uwezo wake mpaka hapo michezo ya michuano ya mataifa ya Afrika itakapo anza Januari 19 mwaka 2013.

Taarifa zinasema bodi ya utawala ya FIFA inafikiria juu ya ombi la mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea.
Taarifa ya FIFA imenukuliwa ikisema
"idara ya huduma za utawala inafikiria juu ya hilo''.

Katika siku za hivi karibu Drogba alihusishwa na kutaka kujiunga na vilabu vya Juventus na Chelsea, lakini hata hivyo inaonekana hilo limeshindikana kutokana na sheria za sasa za FIFA.

No comments:

Post a Comment