Drogba akishangilia goli lake huku akipongezwa na Wesley Sneijder muda mfupi baada ya kuingia akitokea benchi. |
Didier Drogba amewakumbusha Chelsea kile wanachokikosa kwa sasa baada ya kurejea katika soka la Ulaya kufuatia kuanza kuandika bao lake la kwanza dakika tano baada kuingia uwanjani akiifungia bao timu yake mpya ya Galatasaray kwa style ileile ya ki-Chelsea.
Mshambuliaji huyo raia Ivory Coast alifunga goli lake la kwanza katika ushindi wa timu yake wa mabao 2-1 ambao ni vinara wa msimamo wa ligi kuu ya nchini Uturuki kule Akhisar Belediyespor, likiwa ni goli la kwanza katika ardhi ya Ulaya tangu fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2012.
Kama ilivyo kawaida ya aina yake ya magoli , Drogba aliruka juu umbali mrefu na kupiga mpira kichwa pembeni kunako dakika ya 68 ya mchezo dakika 5 akitokea benchi.
Didier Drogba alifunga goli ndani ya dakika 5 za kuanza kuichezea Galatasaray.
Drogba aliitumikia Chelsea kwa miaka minane na kuihama klabu hiyo akiwa akiwa kama mkongwe wa klabu hiyo baada ya kuipa ushindi wa taji la Ulaya na taji la FA katika msimu wake wa mwisho wa utumishi wake Stamford Bridge.
Maamuzi ya kusalia kuwepo Madrid kwa Radamel
Falcao na kuendelea kufulia kwa mshambuliaji Fernando Torres ndani ya kikosi cha Chelsea kunawafanya mashabiki wa klabu hiyo kumkumbuka Chelsea pengine angeendelea kuvaa uzi wa rangi ya bluu.
Picha ya Kumbukumbu: Drogba akifunguka bao la kusawazisha kwa njia ya penati katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment