Balotelli akijikunja kupiga mpira wa mkunjo uliotonga wavuni. |
Mario Balotelli ameendele kujitengenezea mapenzi zaidi katika klabu yake mpya ya AC Milan kufuatia kufunga bao lake la nne katika michezo mitatu ya kuichezea timu hiyo.
Hapo jana Balotelli alifunga goli lake la nne ambalo ni zaidi ya bao moja ukilinganisha na mabao matatu aliyoifungua Manchester City katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2012-2013.
Mshambuliaji huyo ameanza vema katika kurejea kwake Milan akifunga Goli goli kunako dakika ya 78 ya mchezo kwa mpira wa adhabu ndogo katika dimba la San Siro ambapo Milan ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Parma.
Mpenzi Fanny Robert Neguesha, ambaye ni mwanamitindo kutoka Belgiam alikuwa jukwaani akimshuhudia namna ambavyo Balotelli akipiga mpira huo wa adhabu ndogo ya moja kwa moja kwa umahiri mkubwa ambapo alionekana akikunwa na goli hilo na akikusanya vidole vyake vya mikono miwili na kuelekeza kwa Balotelli akiashiria kuufungua moyo wake.
Mshambuliaji mtaliano Balotelli amefunga goli la nne ndani ya michezo mitatu.
Why always me? Balotelli ashangilia kwa swali San Siro.
Balotelli akishangilia goli lake na Riccardo Montolivo.
Mchumba wa Balotelli Fanny Robert Neguesha afungua moyo wake kwa kiashiria cha mikono yake baada ya fanyastic goli la Baloteli.
No comments:
Post a Comment