KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 16, 2013

WAKATI MALINZI AKISUBIRI BUSARA ZA TENGA KUMREJESHA KATIKA KINYANGANYIRO CHA UCHAGUZI TENGA ANASEMA HANA UWEZO HUO.

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leordigar Chilla Tenga akiongea na waandhishi wa habari ka mkutano wake uliofanyika katika moja ya vyumba vya mikutano uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kikubwa ni kwamba rais Tenga amesema wagombea ambao wanaona maamuzi ya kamati ya rufaa hayakuwa ya haki basi wana nafasi nyingine ambayo ni kuomba mapitio mapya ya vielelezo vyake kupitia kamati ya rufaa na pia wanaweza kwenda kwenye mahakama ya michezo ya dunia CAS kupata usaidizi wao kuliko kuacha malumbano yakiendelea. Tenga amesema kimsingi yeye licha ya kuwa ni Rais lakini hana uwezo wa kuingilia maamuzi ya kamati zake ambazo ni kamati huru.
Rais Tenga akijaribu kuongea kwa umakini mkubwa juu ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi na malalamiko ya wadau juu ya kuondolewa na kamati ya rufaa ya uchaguzi kwa jina la mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi ambaye baadaye aliomba mapitio mapya ya rufaa hiyo aliyokatwa dhidi yake, pamoja na malalamiko ya baadhi ya wagombea wengine walioenguliwa.
Rais Tenga akiongea na waandishi wa habari akiwa amezungukwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF.


Bofya chini kusikiliza

No comments:

Post a Comment