Imefahamika kuwa
klabu ya Chelsea inajipanga kumtaja mrithi wa Roberto Di Matteo hii leo.
Di Matteo amefukuzwa
kazi baada ya kichapo kichapo cha mabao 3-0 toka kibibi kizee cha Turin
Juventus ukiwa ni mchezo wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Taarifa zinasema
kuwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich amekuwa akimuhusudu Pep Guardiola lakini
bado haijawa wazi endapo kocha huyo wa zamani wa Barcelona kama anaweza kurejea
katika kazi hiyo ya ufundishaji.
Chelsea ilifanya
mawasiliano na meneja wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez kwa lengo la kumpa
kazi ya muda mfupi.
Bodi ya Chelsea
ilikutana mapema leo na huenda kazi ya mrithi wa Di Matteo ikatolewa kwa
kipindi kifupi kifupi na si kazi ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Di Matteo.
Katika
taarifa iliyotolewa mapema asubuhi ya leo imesema Chelsea inataraji kumtangaza
meneja wake mpya katika kipindi cha muda mfupi ujao.
Chelsea
ambayo inasaka meneja wa tisa tangu klabu hiyo kununuliwa na Abramovich mwaka 2003,
kabla ya mchezo wa jana ilikuwa imekwisha kufanya mawasiliano na Benitez akionekana
kuwa ndiye chaguo sahihi.
Mameja walikuwa
chini ya utawala wa Roman Abramovichni kama ifuatavyo,
Claudio Ranieri: Sep 2000 to May 2004
Jose Mourinho: Jun 2004 to Sep 2007
Avram Grant: Sep 2007 to May 2008
Luiz Felipe Scolari: Jul 2008 to Feb 2009
Guus Hiddink: Feb 2009 to May 2009
Carlo Ancelotti: Jun 2009 to May 2011
Andre Villas-Boas: Jun 2011 to Mar 2012
Roberto Di Matteo: Mar 2012 to Nov 2012.
Di Matteo ambaye
alifanikiwa kushinda mataji ya klabu bingwa na msimu uliopita alikuwa katika
kipindi cha utumishi cha miaka miwili kwa mujibu wa mkataba wake.
Bado mafao
yake hayajafanyiwa kazi lakini vilevile ataendelea kulipwa mpaka hapo atakapo
pata kazi sehemu nyingine.
No comments:
Post a Comment