KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

Cristiano Ronaldo hamtaki Suarez Real Madrid kisa.....................

Nahodha wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hataki mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kujiunga naye Bernabeu, akisema kuwa hana uhakika ni wapi mshambuliaji huyo atafiti kucheza ndani ya kikosi chao na ni kwa namna gani ataingiza aina yake ya uchezaji ndani ya kikosi chao, Zikiwa ni taarifa zilizo nukuliwa na gazeti la Hispania la El Confidencial.

Baada tetesi za uhamisho wa mwezi Januari kuzimwa kufuatia mshambuliaji huyo raia wa Uruguay kusaini mkataba mwingine na klabu yake, taratibu tetesi zimeanza tena.

Wiki hii bosi wa klabu hiyo ya Real Madrid Carlos Ancelotti tena amempongeza Suarez na kumwita ‘fantastic player’ ingawa amesema haitakuwa busara kuzungumzia uhamisho lakini Ronaldo akiripotiwa kutokuwa tayari kucheza na Suarez.
Kwa jicho la tatu inapendeza machoni mwa watazamaji wakiwemo pamoja Ronaldo, Gareth Bale na Suarez lakini pengine Ronaldo ni kweli anapendelea kuwa sambamba na Karim Benzema hususani baada ya ushindi wa taji la Ulaya.
How Cristiano Ronaldo is helping Liverpool
Liverpool haitaki kujichanganya na vurugu za uhamisho wa Suarez kiangazi kama ilivyotokea msimu uliopita wakati huu ni kwamba Brendan Rodgers anajaribu kuimarisha kikosi kwa ajili msimu ujao Premier League na ligi ya mabingwa.