KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

Thiery Henry amvuruga Zlatan Ibrahimavic na maisha ya bata nchini Marekani sasa yuko njia moja

Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 32 wa Paris Saint Germain anafikiria kuelekea katika ligi ya Marekani MLS kufuatia mazungumzo yake na marafiki zake wanaochezea New York Red Bulls ambao wamemdokezea juu ya maisha nchini Marekani.
 Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa huenda akamalizia kazi yake ya soka katika ligi ya nchini humo MLS.
Amekuwa akifanya kazi kubwa na kuisaidia klabu yake inayoshiriki ligi ya Ufaransa ambapo wametwa taji la ligi Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea AC Milan kiangazi 2012. 
Ibrahimovic amekuwa akifurahi uchezaji wake wa mafanikio msimu uliopita ambapo alifanikiwa kumaliza akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akifunga magoli 26 kati ya michezo 33 akicheza chini ya meneja Laurent Blanc.

Mshambuliuaji huyo wa kimataifa wa Sweden hivi karibuni alirefusha kandarasi yake na klabu hiyo ambapo ataendelea kusalia na mwajiri wake wa sasa mpaka 2016.

Katika hatua nyingine , Ibrahimovic amebainisha kuwa atakuwa muwazi kuelekea Marekani kuichezea MLS mkataba wake utakapo malizika na PSG.

“Rafiki yangu Thierry Henry anashughulikia hilo na mara kadhaa nazungumza naye juu ya hilo , katika kipindi cha miaka miwili au mitatu nitaelekea SA.”