KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

World cup Brazil: Rangi ya bahati ya England ni nyekundu nyeupe majanga tupu

England imeshinda kwa aslimia kubwa ya michezo ya kombe la dunia inapokuwa katika jezi za rangi nyekungu (Picture: Getty)
Why England should wear red for best results in Brazil
Pengine katika kila jambo linalihitaji mafanikio suala la bahati pia lina nafasi yake lakini nafasi hiyo inaweza kuchagizwa na maamuzi ya ambayo yatakwenda sambamba na takwimu.
Kwa upande wa mchezo wa soka hapa nchini Tanzania hivi karibuni kuliibuka sakata la ni aina zipi za rangi zitumike kuiavalisha timu ya taifa inapokuwa katika michezo mbalimbali iwe katika michezo ya kirafiki lakini hata katika michezo ya kimashindano

Kwa upande wa timu ya taifa ya England utafiti mdogo uliofanywa umeonyesha kuwa timu ya taifa ya England maarufu kama Simba watatu ambayo kwasasa iko chini ya Roy Hodgson,imekuwa ikifanya vema katika michezo ya kombe la dunia .
England itaanza kampeni ya fainali hizo dhidi ya Italia Jumamosi ikiwa katika jezi zao mpya nyeupe zilizo tengenezwa na na kampuni ya Nike.
 
Lakini endapo watataka kuanza fainali hizo za kombe la dunia kwa ushindi basi watalazimika kurudi kwenye rangi ya bahati.

Ukifuatialia rekodi yake ya ushindi katika kombe la dunia tangu ushiriki wao wa kwanza mwaka 1950, imebainika kuwa England imeshinda michezo mingi zaidi ikiwa katika jezi nyekundu ikiwa ni pamoja na kutinga fainali ya kombe la dunia mwaka 1966 ambapo ilicheza na Ujerumani Magharibi.

Mara nyingi wakihaha na vipigo na sare wakiwa katika rangi tofauti ilhali asilimia kubwa ya ushindi wao wamekuwa kwenye vazi jekundu kuliko vazi jeupe lililozoeleka zaidi.