KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 4, 2014

FIFA yagomea mchezo wa kimataifa wa Uganda na Sudan wakisema ni kinyume na taratibu

Shirikisho la soka duniani (FIFA) imetaka mchezo uliopangwa baina ya Uganda na Sudan kuondolewa katika mpango wa kuchezwa. Katende Malibu, afisa habari wa Uganda Cranes amesema.
"Hatutacheza mchezo wa kirafiki na Sudan kwa amri ya FIFA, hivyo mchezo wetu dhidi ya Ethiopian uko kama ulivyopangwa"
Shirikisho la soka la Uganda(FUFA) lilipanga mchezo dhidi ya Sudan uchezwe Jumanne Novemba 11 2014 ikiwa ni siku mbili baada ya mchezo wao dhidi ya Ethiopia tarehe 9 Novemba 2014
Mchezo wa Ethiopia uliandaliwa na Serikali ya nchi hiyo kupitia wizara mbili za Elimu na Wizara ya michezo na Afya.

Taarifa kutoka Zurich zimesema kuwa michezo miwili ya kujipima nguvu ilikuwa imepangwa kuchezwa kinyume na sheria za FIFA na kwamba hilo halitaruhusiwa ndani ya siku mbili.
Kuelekea mchezo dhidi ya Ethiopia kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic tayari ameshakamilisha orodha ya wachezaji watakaocheza mchezo huo na wengi wakitokea katika ligi ya nchi hiyo "Uganda Premier League".
Wachezaji watano wanaochezea katika ligi za Kenya na Ethiopia pia wamejumuishwa kikosini ambapo Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni atakuwa mgeni wa heshima na hakutakuwa na kiingilio.

No comments:

Post a Comment