Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua
Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi.
Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika
kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi
hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza
mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.
Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo
alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya
Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia
ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa
Maendeleo.
Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya
Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba,
Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya
Lindi.
Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Sunday Kayuni picnani juu alimaliza mkataba wake wa ukurugenzi wa ufundi Desemba 31 mwaka jana. |
YANGA, SIMBA ZAPIGWA FAINI MIL 25
Klabu za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh.
milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki
wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya
uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini
ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa
faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu
hizo.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura
kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Tunatoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu
kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya
viwanja ikiwepo viti, na tutachukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki
wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.
RAMBIRAMBI KIFO CHA MSHABIKI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mshabiki Deodatus Mwakyangula
kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya mechi kati ya Yanga na Azam
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea wakati akiwa
uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyomalizika kwa
sare ya bao 1-1.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
RWIZA, LIUNDA KUSIMAMIA MECHI ZA CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua
Watanzania Alfred Rwiza na Leslie Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii
na mwezi ujao.
Liunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe
la Shirikisho (CC) kati ya How Mine ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria
itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka huu) jijini Bulawayo.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na
wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael
na Luelseghed Ghebremichael.
Naye Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland
itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Maseru.
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan
Lengani, Innocent Kaundula, Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka
nchini Malawi.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
No comments:
Post a Comment