Bingwa mtetezi wa mashindano ya US Open kwa upande wa wanawake Serana
Williams (pichani juu) ameingia katika robo fainali ya mashindano hayo,
kwa kumshinda Sloane Stephens kwa seti 6-4, 6-1.
Williams sasa atakutana na mchezaji namabri 18 duniani Carla Suarez
Navarro kutoka Uhispania, ambaye alimshinda mchezaji nambari 8 Angelique
Kerber wa Ujerumani kwa seti 4-6, 6-3 na 7-6.
"Ubora wa tenesi ulikuwa
wa juu sana, Sloane ni mchezaji mzuri sana, na nilihisi hivyo lakini
mwisho wa siku ilikuwa mechi ya raundi ya nne na bila shaka ni hisia za
robo fainali kuliko nusu fainali," aliseam Williams baada ya mchezo huo
wa raundi ya tatu.
Kwa upande wa wanaume, mshiriki wa mwisho kati ya 15 wa Marekani
alipoteza, wakati Tim Smyczek, ambaye ni nambari 109 kwa ubora duniani
alipopigwa kwa seti 6-4, 4-6, 0-6, 6-3 na 7-5 na Marcel Granollers
kutoka Uhispania.
Hiyo iliyafanya mashindano ya mwaka huu kuwa ya kwanza
katika historia, kutokuwa na mwanaume hata mmoja kutoka nchi muandaji
katika raundi ya nne.
Granollers ambaye anashika nambari 43 duniani, atakutana na mchezaji
nambari moja duniani Novak Djokovic. Bingwa mtetezi Andy Murray, bingwa
wa US Open wa mwaka 2001, Lleyton Hewitt, mchezaji nambari 5 Tomas
Berdych, Nambari 9 Stanislas Wawrinka na nambari 21 Mikhail Youzhny pia
walifanikiwa kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment