Ni pigo lengine kwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani,
Joachim Löw. Podolski hatacheza tena mwaka huu wa 2013. Bastian
Schweinsteiger, Mario Götze na Ilkay Gundogan pia wameumia.
Jeraha kwenye goti alilolipata mchezaji wa safu ya mashambulizi ya timu
ya taifa ya Ujerumani, Lukas Podolski, ni baya zaidi kuliko ilivyohofiwa
hapo awali.
Hii ina maana mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal London
hatacheza hadi mwezi Desemba mwaka huu.
Daktari wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani, Hans-Wilhelm
Mueller-Wohlfahrt, amemfanyia uchunguzi Podolski mjini Munich na
kugundua amekatika ukano wa mvungu wa goti la mguu wake wa kushoto.
"Kwa
bahati mbaya sitaweza kucheza kwa muda mrefu, kama miezi mitatu,"
Podolski ameliambia gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild.
Podolski atakosa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia la kandanda nchini
Brazil mwakani zilizosalia mwaka huu.
Alitolewa uwanjani akiwa kwenye
machela dakika ya 50 ya mechi kati ya klabu yake ya Arsenal na
Fernerbahce Istanbul wiki iliyopita, wakati ilipofikiriwa angekuwa nje
ya uwanja bila kucheza mechi yoyote kwa wiki hadi 10.
No comments:
Post a Comment