KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 8, 2014

HEMEDI AURORA KUJADILIWA NA WANACHAMA WA COASTAL UNION KESHO

Mwakilishi wa wanachama wa Coastal Union,Salim Al Mazrui

MKUTANO mkuu wa dharura wa wanachama kumjadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Aurora kujiuzulu unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii kwenye ukumbi wa Makao makuu ya Klabu ya Coastal Union barabara 11 jijini Tanga.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa nne asubuhi utakaohusisha wanachama hai ambao wamelipia kadi zao na hawadaiwi madeni yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari,Mwakilishi wa Wanachama wa Coastal Union,Salim Al-Mazrui alisema maandalizi ya kuelekea mkutano huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na utakuwa na agenda mbili muhimu zitakazojadiliwa.

Al Mazrui alisema agenda ya kwanza itakuwa ni kujadilia uvumi uliojitokeza wa kujadili kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Hemed Hilal Aurora.

Alisema agenda ya pili itakuwa ni kujadili utendaji wa Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto ndani ya klabu hiyo hasa kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara na kutoa maamuzi.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Coastal Union ya Hemed Aurora
Mwakilishi huyo aliwataka wanachama wa Coastal Union waliokuwa hai kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wenye lango pia la kuangalia namna ya kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kuu.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alithibitisha kupokea taarifa ya mkutano huo na hivyo utafanyika siku ya Jumapili kutokana na wanachama hao kufuata taratibu zote.