Mechi ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la
Chalenji kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya
(Harambee Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.
Kwa mujibu wa ofisa wa Cecafa, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa
Uwanja wa Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi.
Mechi hiyo itachezwa JumanneDesemba 10.
Kilimanjaro Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda
(The Cranes) kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya
michuano hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la
Mombasa.
Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana
mabao 2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati
katika mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd
na nahodha Kelvin Yondani.
No comments:
Post a Comment