Meneja wa Manchester United, David Moyes bado anadhamiria kuongoza
klabu hicho kutetea taji lao la Premier licha ya kichapo kingine
mikononi mwa Newcastle Jumamosi.
Kiungo wa Ufaransa, Yohan Cabaye, alifunga bao la ushindi dakika ya
61 na kuwatuza Newcastle ushindi wa kwanza Old Trafford kwa miaka 41.
Janga hilo la kichapo lilifuatia kichapo cha awali cha bao 1-0 kutoka kwa Everton lakini Moyes bado
anashikilia kwamba United wana uwezo wa kuhusika katika harakati za
kunyakua taji la Uingereza.
"Matokeo yangekuwa bora," meneja huyo aliyekufa moyo huku vijana wake
wakiendelea kumiliki nafasi ya tisa, alama 12 nyuma ya viongozi
Arsenal.
"Tulihitaji bao ili kutupa imani lakini hatukubuni kikamilifu," aliongeza.
Alipoulizwa ikiwa United bado wamesalia katika kinyang'anyiro cha
taji, Moyes alijibu, "Nasimama kidete kwamba tutakuwa karibu na
ninatumahi tutakuwa miongoni mwa washiriki musimu ukikamilika."
Huku kurunzi ikimulikwa kwake tangu aridhi Sir Alex Ferguson, Moyes alikiri kwamba utawala mpya umekumbwa na mawimbu makali.
"Tumekosa mbinu za kufunga nyakati zinazofaa na tumeshindwa kutumia
fursa ya kucheza pasi sawa. Tumepoteza mechi mbili 1-0 ambazo matokeo
yalikuwa kinyume na mchezo."
No comments:
Post a Comment