KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 8, 2013

BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO ATAMBA KUMSAMBARATISHA DAVID CHALANGA WA KENYA USIKU WA MWAKA MPYA.

BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika pambano lake dhidi ya David Chalanga kutoka Kenya, litakalofanyika  Disemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu ambapo pambano hilo litakuwa nila  kufunga mwaka na kufungua mwaka mpya wa 2014 na litakuwa la raundi nane

Pambani hilo litakuwa chachu kwa mabondia hao wanaotamba Afrika Mashariki kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi ambapo mashabikiwa wanalisubiri kwa hamu kubwa kila kona ya Tanzania.

Akizungumzia mpambano huo miyeyusho amesema yeye yupo fiti wakati wowote hata kama mpinzani akitaka kucheza sasa yuko tayari.
 
Katika mapambano ya utangulizi bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka, Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizichapa na Mohamed Kashinde
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

No comments:

Post a Comment