Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa
Kimataifa (ITC) ya mchezaji George Odhiambo, raia wa Kenya aliyejiunga
na klabu ya Azam.
George Odhiambo(blackaberry) |
Hati
hiyo imetolewa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) ambapo
Odhiambo alikuwa akicheza nchini humo kabla ya kutua Azam kwa ajili ya
msimu wa 2012/2013.
Klabu
nyingine zinazosajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania zinatakiwa
kuhakikisha zinakamilisha uhamisho wao (transfer) kabla ya Julai 30
mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho kufanya hivyo.
Kanuni
ya 41 ya Ligi Kuu kuhusu ITC inasema: “(1) Maombi ya ITC kwa wachezaji
wa kigeni wa kulipwa yatawasilishwa kupitia mtandao wa kompyuta kwa
kutumia program ya ‘Transfer Matching System-TMS’ baada ya klabu
zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana nje ya
mtandao.
(2)
Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wasio wa kulipwa yatawasilishwa
kwa barua TFF baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji
hao kukubaliana. Chama cha Soka kinachotoa ITC kwa njia hii kitapeleka
nakala FIFA. (3) ITC haihitajiki kwa mchezaji mwenye umri chini ya miaka
kumi na mbili (12).”
Tunapenda
kuzikumbusha klabu kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 53 ya Ligi Kuu,
wachezaji wa kigeni ni lazima wawe wanachezea timu ya Taifa au klabu za
Ligi Kuu huko wanakotoka.
Kanuni
hiyo inasema: “Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wa ngazi
ya kimataifa ambao ni wa timu za Taifa na Ligi Kuu kutoka nje ya nchi
wasiozidi watano (5). Wachezaji kutoka Ulaya na Marekani ya Kusini
wanweza kuwa wa daraja la pili na kuendelea, na klabu inaruhusiwa
kuchezesha wachezaji walioorodheshwa wasiozidi watano (5) wa kigeni
katika mchezo mmoja. Wachezaji hao watasajiliwa baada ya TFF kuhakikisha
usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa
kimataifa.”
No comments:
Post a Comment