Aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Benfica kutoka
Msumbiji Mario Coluna amefariki nchini Msumbuji akiwa na umri wa miaka
sabini na nane.
Coluna aliongoza timu ya Benfica kushinda mataji
kadhaa barani ulaya na vile vile aliichezea timu ya taifa ya ureno
katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1966.
Alipostaafu Coluna alirejea nyumbani ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Msumbiji.
Serikali ya Msumbiji imetangaza kua Coluna atapewa mazishi ya heshima zote za kitaifa.
Kifo chake kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo
cha mwanakandanda mwengine mashuhuri wa Msumbiji Eusebio aliyefariki
nchini Ureno.
No comments:
Post a Comment