KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 30, 2012

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA:Ronaldinho anataka kucheza kombe la dunia 2014 nyumbani Brazil, Paolo Maldini anasema AC Milan sasa imekuwa kama klabu ya ndondo ya kawaida sana. Zanetti anasema haondoki Italia ng'o baada ya kustaafu anataka kuifundisha Inter Milan. Vidic anasema itamchukua muda kurudia kama alivyokuwa kabla ya majeraha.Barani Afrika Stephen Keshi aacha kitasa wake kwa usamaria wake.



 Ronaldinho Gaucho anataka kucheza kombe la dunia 2014

Ronaldo de Assis Moreira, maarufu zaidi kama Ronaldinho Gaucho, ameweka waji juu ya nia yake ya kutaka kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakacho shiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kikosi hicho ana matumaini ya kuwemo kikosini katika michuano hiyo ijayo ambayo imesalia miezi 18, na anaamini mipango ya kujitengenezea kiwango chake ili kuhakikisha anarejea kikosini si migumu.

Amenukuliwa na waandhishi wa habari akiwa nchini India akisema,

"hakuna kitu kizuri kama kucheza kombe la dunia katika ardhi ya nyumbani mbele ya mashabiki wenu na nisingependa kuikosa fursa hiyo"

"najiamini na bado ni hamu kubwa ya soka na kuipigania nchi yangu ya Brazil kwa ujimla ambayo inapelekea mimi kutaka kurejea katika timu yangu ninayoipenda zaidi.



"nataka kuwa sehemu ya kombe la dunia 2014, litakuwa ni jambo kubwa sana katika maisha yangu na maisha ya wengi nchini Brazil .
 Nataka kurejesha uwezo wangu kwa kiwango cha juu ili nitoe mchango wangu katika timu. Ni jambo la kipaumbele kuhakikisha niko tayari kucheza endapo nafasi itapatikana"


Kiti cha moto cha benchi la ufundi la Brazil (The Selecao) amekabidhiwa kocha wa zamani wa kikosi hicho Luiz Felipe Scolari mwezi November, ambaye aliiongoza kwa mafanikio mwaka 2002 wakati huo Ronaldinho alikuwa ni mmoja wa nyota waliong’ara ndani ya kikosi.

Ronaldinho mwenye umri wa miaka 32 na ambaye kwasasa anachezea Atletico Mineiro ya Brazil ameongeza kuwa

Kombe la dunia lijalo litakuwa ni kipimo kizuri cha ukomavu wa wachezaji waliochipukia kama Neymar na  Leandro Damiao ambao watajiwakilisha duniani kama alivyofanya yeye mwaka 2002, na kusema kuwa atatumia uzoefu wake kuwasaidia.




Paolo Maldini anasema AC Milan sasa imekuwa klabu ya kawaida

Mwasisi wa klabu ya AC Milan ya Italia Paolo Maldini amesema kwasasa klabu yake hiyo ya zamani imekuwa klabu ya kawaida sana ambapo ametofautisha mipango ya klabu hiyo na vilabu vikubwa vinavyong'ara duniani kwasasa.


Maldini alishinda mataji matano ya klabu bingwa Ulaya na taji la ligi kuu ya nchini Italia Serie A mara saba katika kipindi chake cha misimu 25 aliyoichezea Milan.


Maldini anasema kikosi hicho kimeshindwa kuonyesha dhamira ya kweli ya mafanikio katika miaka ya hivi karibuni.

Amenukuliwa na gazeti la 'La Repubblica' akisema

 “nilikuwa katika kipindi kirefu cha kutosha cha miaka miaka 25 .
"nilipofika, nilikuta misingi ya kujenga klabu, Rais wa klabu Silvio Berlusconi alikuja kutufundisha kufikiri zaidi jambo ambalo liko wazi kwa kuwa kawekeza.


"Arrigo Sacchi akafuatia na sote tuliweka akilini kuwa sisi ni alama ya aina ya uchezaji soka duniani , kilikuwa ni kitu cha ajabu.

“taratibu miujiza ile imeondoka na kugeuka kuwa klabu ya kawaida kabisa. Yote hiyo ni kwasababu imeacha utamaduni wa kusambaza ujumbe na wale walioandika historia ya klabu wameacha kutoa ujuzi wao kwa kizazi kilichofuata.

Licha ya ukosoaji wake mkubwa, mlinzi huyo wa zamani wa Milan mwenye umri wa mika 44 amekanusha kuwa anataka kazi ya ukocha San Siro.



Zanetti anasema haondoki Italia ng'o baada ya kustaafu anataka kuifundisha Inter Milan

Kiungo wa Inter Milan Javier Zanetti anataka kusalia nchini Italia baada ya kustaafu kucheza soka na kusema kuwa ataelekea katika kazi ya kuifundisha Nerazzurri mara baada ya kustaafu.

Raia huyo wa Argentina amesema anaipenda sana nchi yake ya Argentina lakini anataka kuendelea kufanya kazi katika ligi ya soka ya Italia Serie A ambayo alijiunga nayo kama mchezaji mwaka 1995.

Amenukuliwa akisema

"klabu hii imenipatia vitu vingi, maisha yangu sasa yako Italia na nitakapo acha kucheza nitafundisha Inter,"

"kumetulia, nimekuwa safi katika klabu hii katika kipindi chote milia yangu"

Lakini pia amesema nia yake ya kusaidia watoto wa mitaani na wenye maisha magumu nchini kwake itaendelea, isipokuwa hataweza kurejea tena katika ardhi ya nyumbani katika siku za hivi karibuni.



Vidic anasema itamchukua muda kurudia kama alivyokuwa kabla ya majeraha.

Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic anaamini kuwa itamchukua muda mrefu msimu huu kuweza kuponya kabisa majeraha yake yanayo msumbua.

Mlinzi huyo wa kati alikuwa msaada kwa United ilipotengeneza ushindi safi wa mabao 2-0 jumamosi dhidi ya West Bromwich Albion, ambao ulikuwa ni mchezo wake wa pili kurejea kikosini baada ya kukosekana kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka na kusumbuliwa na mguu.



Vidic anayesumbuliwa na mshipa mkubwa wa mguu anasema ana kazi kubwa ya kuhakikisha anachukua tahadhari ya kuhakikisha anaponya kabiza maumivu hayo

"daktari ndiye anayenisamia michezo ninayocheza kwasasa, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita nilikuwa katika ungalizi mkubwa maana wakati mwingine nilikuwa nashtua maumivu. Hii ndiyo hali nanayokwenda nayo.

"nafurahi nimeweza kucheza kucheza baada ya kipindi cha kusimama kwa miezi  mitatu. Jambo zuri niko tena uwanjani na naweza kucheza, pengine nitakuwa nacheza sasa mara kwa mara na kujenga upya uwezo wangu"


Nations Cup 2013: Kocha wa Nigeria akubali ombi la Shittu la kuondolewa kikosini super eagles 

Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi amekubali ombi la mchezaji wa kimataifa wa Nigeria Super Eagles anayechezea klabu ya Millwall, Danny Shittu ya kwamba asimfikirie kumwita katika kikosi chake kitakacho elekea katika fainali za mataifa ya Afrika mwenzi januari nchini Afrika Kusini.



Mlinzi huyo alitaka kuelekeza mawazo yake katika kuisaidia klabu yake ambayo inapiga kufa kupona kupanda daraja la ligi kuu ya soka nchini England ‘English Premier League’.

Afisa habari wa shirikisho la soka la Nigeria Ben Alaiya amesema

"Stephen Keshi amekubali Danny Shittu anaweza kusalia huko katika klabu yake na hatakuwepo katika fainali za mataifa ya Afrika".

Shittu aliitwa katika kikosi cha mapema cha wachezaji 32 wa Super Eagles kikosi ambacho baadaye kitafanyiwa mchujo.

Kabla ya Keshi kumruhusu Shittu, shirikisho la soka ;a Nigeria NFF lilikataa ombi la Shittu.

NFF ilitaka kuishitaki klabu ya Millwall kwa shirikisho la soka duniani FIFA endapo ingegomea kumuachia mlinzi huyo wa kati wa klabu hiyo.

Nigeria iko katika kundo moja na mabingwa watetezi Zambia, Ethiopia na Burkina Faso katika kundi la C.

No comments:

Post a Comment